Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
1F70230F-13AA-4521-B56F-33278A4DC9F4.png


Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 30, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 30, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 0
Vipi kama mtu akitumia ID yake kisha akatangazwa mshindi, atatakiwa atoe picha na contacts ili atangazwe kwenye hizo social media. Ile process ya mshindi kupatikana, kutangazwa na kupokea tuzo yake hakuhusishi kuvunja usiri wa anonymous ID kama sera kuu ya JF.

Isije fika mwisho nikajua kumbe mfano mshindi ni ID: Hazchem Plate, jina: Jumanne Kalenga ambaye ni kaka yangu na huwa anachangia uzi wa kimasihara.

Hapa tujue tunakuja na hizi ID au tunaunga mpya. Maxence Melo
 
Mkuu Maxence Melo naomba ikiwezekana WOTE tutumie numbers kuhide identities zetu, kuna watu wana influence kubwa humu topics zao zinatambaa replies na kuna wengine tumezoea madongo, please weka fair playground
Ilitakiwa washindi wasiamuliwe na kura maana kuna watu wana ID nyingi watajipigia kura ili kulamba huto tumilion 5 twa billionaire melo
 
Asante kwa fursa hii, Lakini nina wasiwasi kama mshindi atapatikana kwa kura basi siyo kwamba linataftwa andiko bora bali lenye kura nyingi.

Ikumbukwe kuwa mtu anaweza kuwa na Andiko bora ila asipate kura. Nashauri, wataalamu wapitie na kuangalia ni nani kaandika andiko bora lenye kugusa mahitaji ya jamii zetu.

Asante
 
Hivi ule mchezo wa thread kufutwa hapa haupo?

Maana hilo suala sidhani kama mmeliongelea.
 
Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika na pia uamuzi wa jopo la wataalamu wa lugha, uandishi na ushirikishaji jamii.
Lugha ya malkia itakuwa na tatizo hili hapa; ikiwa ni pamoja na uandishi katika eneo la sayansi na teknologia ambako wasomaji wengi wanaweza kupata ugumu wa kushiriki katika maeneo hayo.

Kiujumla wake, ni wazo zuri kabisa.
 
Back
Top Bottom