Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
1F70230F-13AA-4521-B56F-33278A4DC9F4.png


Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 30, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 30, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 0
Wanasema lengo ni kuongeza maudhui hivyo hapo inakubidi kuandaa mada tofauti na mwanzo ili kuongeza maudhui
I do ask again!
Randomly naandika mada then naposti humu je siwezi kutumia mojawapo ya mada zangu nilizoweka humu. Since it's still my ideas.
Asante
 
Ngoja nifanye kitu nipate hata simu ya mkononi aiseee

Maudhui ya mapenzi, michezo na uchawi haya hayatakiwi?
 
Biashara
Nchi inahitaji kuwepo kwa usawa katika makadirio ya Kodi na kuwawezesha vijana mikopo mbali mbali ili kuongeza wigo wa walipa Kodi kuliko kuisambaza hivi bado tabaka la chini wanaumia zaidi

Elimu
Elimu inabidi isiingiliwe na wanasiasa kwani wamekuwa wakitoa miongozo isiyo na tija na kuwachanganya walimu kitukinachopelekea mtaala wa elimu kupwaya na kutoendana na maisha halisi hvy mabadiliko ya mitaala ifanywe na wataalamu na asilimia kubwa wakiwepo walimu kwani ndio wanaoutekeleza na uhimize vitendo zaidi kuliko kukaa darasani

Kilimo
Serikali itoe ruzuku kwanye zana za kuzalishia Kama mbegu na mbolea kumsaidia mkulia, pia kuwa jirani na wakulima kujua changamoto zao pasipo kusahau masoko ya mazao yanayozalishwa hakuna masoko ya uhakika ambapo huathiri uzalishaji na elimu ya kilimo Cha kisasa itolewe kwa wingi kudhibiti uharibifu wa mazingira

Siasa
Kuwepo kwa siasa Bora inayoelekeana na uhalisia na yenye usawa yenye kutokinzana na matakwa ya wananchi

Afya
afya isiingiliwe na wanasiasa kwani ni sekta nyeti ubadhirifu wa madawa ufuatiliwe na serikali kwa ukaribu zaidi
 
Hapana, lazima liwe ni andishi jipya ambalo halijachapishwa KOKOTE.

Asante
Your signature Maxence, may be problematic. In fact it is problematic!

It cannot be open ended as such: "I may not agree with what you say, but I will defend to the death your right to say it!"

There has to be limits in some instances.
 
JF, home of Great Thinkers.

Kushiriki na kushinda hili shindano itabidi fikra na mawazo sahihi yatumike.

JF inachukua sura na mueleo mwingine kabisa. Hongereni Maxence Melo na timu nzima ya JF.

Pia kwa washiriki nafikiri sio mbaya JF ikawa na namna ya umiliki wa hayo mawazo ya takayoletwa kwa ushindani ili ikiwa itafaa, vyombo, taasisi au wadau mbalimbali watakaotaka kutekeleza kwa yale yenye mwelekeo huo, ifanyike hivyo.

Kila la kheri
 
Back
Top Bottom