Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
1F70230F-13AA-4521-B56F-33278A4DC9F4.png


Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 30, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 30, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 0
Kama jamii forum wasipokuwa makini kwenye uchaguzi was story bora, nahisi watampa zawadi mtu asiyestahili.

Kuna mnyamwezi kaandika kitu cha hatari ila wanyabe wanapita kama hawaoni... so far nyuzi nyepesi ndo zinapigiwa kura
Sasa ukianza kusema wachukue chache, swali watazipataje hizi chache? Jibu ni kupitia kura zetu 40% na kura za majaji 60%... Acha wananchi wafunguke.. tena na huu ugumu wa maisha kuna watu wataandika stories of change, wengine hisia zao, wengine malalamiko, wengine mawazo ya biashara, wengine watacopy somewhere na kupaste..

Yaani tarajia vurugu za kutosha na hiyo ndiyo democrasia kama mtandao ulivyojipambanua kuipigania... so let them be free... Judges will work out to get the best top 3... Majudges jiandaeni kwa kazi ngumu lakini mwisho wa siku tunahitaji zipatikane the best 3 stories of change... Na ikiwezekana zitachapishwa kwenye majarida kwa idhini ya wenye nazo ili kunufaisha hata wasiopo humu jamiiforum
 
Wakuu
Tuliambiwa shindano hilo lilianza tarehe 14 na kufika kikomo 15

sasa tunaitafuta tarehe 17 bila majibu yoyoete na ukiangalia kura hazikufungwa jana kipindi nikiwa miongoni mwa wenye kura nyingi

Naandika hivi sasa bado kura zinaendelea kupigwa kinyume na masharti na sheria za shindano,, naona kuna dalili zisizonzuri

Kwanini mpaka sasa mshindi hatangazwi?
Umesoma vizuri kweli boss?
 
Kuhusu chanjo ya corona

Rais mama yetu alitutaarifu kuhusu chanjo zilizoletewa na watu waafya ila tunajiuliza hii chanjo niyakwetu au ya nchi nyingine?
Tunaaza kujua mataifa ya uwarabuni walikaa na mama yetu kiongozi wetu mama Samia kwamazungumzo ya kuhusu chanjo ya kupigana na corona.

Mama yetu kakubali chanjo kunaukakasi hapo kwa watanzania ambao wengi class niempty apoapo tunaambiwa ukitaka kuchanja chanjo lazima usaini.

Apo tunajiuliza kutukandamiza au kutookoa haaaaaa bitucheke watanzania wengi tutakaa tu tuone viongozi wanavyotaka kutoongoza kiboya tunataka kiongozi makini mwenye hekima ambaye hawezi kuongea bila kuchunguza mama yetu anatakiwa ajue wananchi wanamtegemea na wanamjali sana sisi tunaimani nae, form ya chanjo hiyo ni yakingereza mmm watanzania wengi hawajasoma nisawa na( mtoto mdogo ampige mzazi) kwanini wasiandike kwakiswahili kama wanataka kutuokoa kwenye janga hilo kweli atupo makini kabisa siamini kabisa kuwa waziri alifikilia hivyo au Rais wetu alikaa kabisa kuja kutuambia tupige chanjo kwakujaza kwa form ambayo inamaandishi ya kingereza simajanga hapo.

Rais mama Samia tunaomba ichunguze chanjo na hata form iwe ya maneno ya kiswahili tunakuamini sana hatamimi mwanachi nakuamini na tunakuamini.
 
Mbona sielewi shindano
kama maelekezo yote hayo yame tolewa na bado max ameendelea kufafanua yale yanayo ulizwa na wadau humu lakini una ona bado huelewi chochte basi ni kheri ukawa Mpenzi msomaji tu
 
Nikweli kuhusu kutengenezwa chanjo ya corona Dunia inaangaika kuhusu corona ila shirika la afya who linaangaika kufafanua kuhusu chanjo inavyotengeneza.

Vipi ni viungo vinavyotengeneza chanjo sasa hapa tujue Chanjo hiyo inajumuisha vipande vidogo vya vijiumbe vinavyosababisha magonjwa au chembechembe zinazounda vipande vidogo vidogo.
 
Mimi napenda kuwa mshindi wa kwanza, na wa pili na wa tatu na pia nipate lap top na simu. INAWEZEKANA bwana.

Muhimu makala zangu ziwezeshe jamii na umma kujitambua, kubadilika, kuacha mazoea. Tena jamii ijue kuwa kuona ni kuamini. Iwe hapa KAZI TU. Zawadi baadaye, na sio muhimu sana kivile. Ila JF nawapongeza kwa hamasisho hili.

Nitajaribu.
 
Imeelezwa kwa uwazi kabisa (soma palipoandikwa ZINGATIA). Wewe andika kadiri uwezavyo, huenda ni miongoni mwa maandiko yako mojawapo likashinda.

Hata mtu angekuwa na ID 20, haziwezi kushinda zote. Wakati wa kufanya uamuzi washindi watakuwa contacted.

Asante
vp maandiko yake matatu yakishika nafasi tatu za juu.. mtamnyima zawadi zake wakati mumeruhusu wwenyewe?
 
Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo
Mkuu Maxence Melo naamini kabisa hili zoezi litaleta tija sio tu kwa mawazo bora lakini pia kuifanya JF iheshimike na kupata wanachama zaidi.

Nimenukuu hiyo sehem nikitaka kujiridhisha Je, kuna haja ya haya machapisho ya washiriki kuwekwa kwenye hiyo mitandao mingine ya kijamii iliyotajwa hapo juu ili kuongeza wigo wa watu wengi kusoma na ikiwezekana wapigie kura machapisho wanaoona wao yana tija?

Pili, maelezo ya kupiga kura yako wazi na yanajitosheleza, lakini nimeona watu wanachanganya ku like na kupigia kura chapisho...nafikiri hapo washiriki wanaweza kuwahamasisha wapiga kura namna ya kupiga kura.

Lakini kuna changamoto moja hasa kwa wanaotumia App, wanadai upigaji kura haupo rafiki. Situmii app lakini kuna wadau wametoa hayo malalamiko, mnaweza kuliangalia ikiwa lina ukweli na lipatiwe ufumbuzi.

Vinginevyo, niwatakie kila la kheri kwenye safari hii itakayoleta mabadiliko ya fikra za watu na kuleta chachu ya maendeleo kwa jamii.

Shukran
 
Spika mh Ndugai amesema na bunge kuhusu makato ya tozo ya miamala kwa njia njema kwa kutekeleza miradi ya maendeleo ili ikifika 2025 Tanzania ipige atua kimaendeleo. Wanao pinga nivema wakatoa mawazo mbadala ya nini kifanyike
 
Back
Top Bottom