Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
1F70230F-13AA-4521-B56F-33278A4DC9F4.png

Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 30, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 30, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 0
Mkuu Maxence Melo naamini kabisa hili zoezi litaleta tija sio tu kwa mawazo bora lakini pia kuifanya JF iheshimike na kupata wanachama zaidi.

Nimenukuu hiyo sehem nikitaka kujiridhisha Je, kuna haja ya haya machapisho ya washiriki kuwekwa kwenye hiyo mitandao mingine ya kijamii iliyotajwa hapo juu ili kuongeza wigo wa watu wengi kusoma na ikiwezekana wapigie kura machapisho wanaoona wao yana tija?...
Kwa hii screenshot, ni wazi upo via PC.

Angalia PEMBENI mwa mjadala husika (1st post) utaona sehemu imeandikwa VOTES) ndipo ubonyeze mshale wa kwenda juu.

View attachment 1870627
Mkuu Melo naomba ufanyie kazi maoni ya mdau.
Si wote tunaotumia web browser.. tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu mdau ni kwamba sehemu ya kupiga kura inakaa kwenye kona ya juu kulia, kama alivyoonyesha mkuu Maxence Melo kwenye reply yake hapo juu. Lakini kuna baadhi ya browswer nadhani kura zinakuwa chini ya post kama inavyoonekana hapo chini. So kama hupati vote options juu kulia mwa post, basi utazipata chini ya post kama ifuatavyo (kutegemea na aina ya browser au kifaa unachotumia): 👇
1627405752246.png
 
Ndugu mdau ni kwamba sehemu ya kupiga kura inakaa kwenye kona ya juu kulia, kama alivyoonyesha mkuu Maxence Melo kwenye reply yake hapo juu. Lakini kuna baadhi ya browswer nadhani kura zinakuwa chini ya post kama inavyoonekana hapo chini. So kama hupati vote options juu kulia mwa post, basi utazipata chini ya post kama ifuatavyo (kutegemea na aina ya browser au kifaa unachotumia): [emoji116]
View attachment 1870682
Mkuu mimi natumia app,na watumiajo wengi tu tunatumia app hatutumii hiyo browser.
Basi wangesema wapiga kura ni wanaotumia browser pekeyake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mimi natumia app,na watumiajo wengi tu tunatumia app hatutumii hiyo browser.
Basi wangesema wapiga kura ni wanaotumia browser pekeyake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa app sijui vizuri mkuu. Lakini unaweza kuangalia hizo sehemu nilizoeleza kama unaweza kuona option ya kupiga kura; otherwise inabidi utumie PC walau kwa muda tu ili uweze kupiga kura na baada ya hapo utaendelea na utaratibu wako wa app.
 
Basi hili zoezi siyo rafiki na halitakuwa fair maana watu wengi tunashindwa kupiga kura.

Siwezi kutumia kingine zaidi ya App.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jambo wakuu!

Wakuu naomba mnisaidie kuboost uwezekano wa kushinda zawadi kupitia andiko langu hili hapa chini. Najuta kuandika kwa kiingereza; naona wadau wanalipita tu kama vile hawalioni. Kiingereza hakijawahi kumuacha mtu salama. Afadhali kumbe ningeandika kwa Kiswahili ningeeleweka kuliko kuandika lugha ya mabeberu. Tafadhali naomba mnipigie kura kwa kubonyeza kitufe hiki hapa kama kinavyoonekana; hata kama huelewi kiingereza, wewe gonga hapo unipigie kura mkuu. Tazama hadi sasa nina kura 0!!! Asa mimi nashindaje wakati hili shindano nimelikami? Please assits hali mabaya!!!!!

Asante kwa msaaada wako, ubarikiwe sana.

1627488089872.png
 
View attachment 1871934
Nimekupa kura mkuu, unaweza ukalibadilisha kwenda kiswahili kama una muda lakini
 
Asante kwa kunipa kura na kwa ushauri mujarabu mkuu. Ubarikiwe sana. 🙏 🙏

Sijui kama masharti ya shindano yanaruhusu hasa kwa kuwa tayari nimeishaipost mtandaoni. Anyway, tusubiri wenyewe waje tuone kama wanaweza kunifanyia huo wepesi. CC Maxence Melo
 
Safi na Hongereni JF.

Ninachotaka kujua, ukiandika andishi kwa jina la kubuni, je ukitangazwa mshindi utatangazwa kwa jina hilo la kubuni ama kwa jina lako halisi?

Nashauri, ishu ya kupiga kura iwe nafasi ya pili. Kwa sababu huenda mtu akashinda kwa sababu ya Ushawishi wake jukwaani. Hivyo kuleta upendeleo. Wachambuzi na wataalam walete maandiko matano yaliyofanya vizuri kisha yapigiwe kura.
nakuunga mkono nafikiri ni mwanzo kama watakuja endelea baadae waboreshe ukijulikana unapigiwa tu kura,na kura zinaombwa ila je issue yako ina mantiki na unatetetea vipi hoja yako
 
View attachment 1850745

Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 15, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 15, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
In shaa Allah!
 
Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
Jamani eeh mi sijalewa hapo 👆👆👆👆
 
Naombeni msaada nikipost makala zangu kwenye Stories of change hazikai zinaenda kwenye forums nyingine naomba msaada nifanyeje
 
Samahani naomba kuuliza, hiyo makala ukishaiandika unaipost wapi ili uwe mmoja kati ya wanaoshindana
 
Samahani naomba kuuliza, hiyo makala ukishaiandika unaipost wapi ili uwe mmoja kati ya wanaoshinda
 
Ni wazo zuri kabisa. Ila kama mshindi atapatikana kwa kupigiwa kura; basi rikiboy na maudhui yake 'kimasihara' atashinda asubuhi.

Jamii ya watanzania inapenda zaidi burudani na mizaha kuliko mijadala na maudhui serious.
wangeacha judges tu kura utakuta watu wanachagua diwani au mbunge wa kawaida kiutendaji yani kama bahati bahati mtu mjengoni
 
Back
Top Bottom