Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
1F70230F-13AA-4521-B56F-33278A4DC9F4.png


Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 30, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 30, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 0
Samahani naomba kuuliza, hiyo makala ukishaiandika unaipost wapi ili uwe mmoja kati ya wanaoshinda
Bonyeza hii link
ina makala yangu ambayo nimeandika ikishafunguka juu kabisa bonyeza sehemu imeandikwa "Story of change" ikifunguka bonyeza "post thread" Andika kichwa cha habari cha makala yako alafu andika makala yako. Ukimaliza itume kwa kubonyeza chini kabisa kwenye "post thread"
 
Nimesoma, nikasoma tena sasa najiuliza je, naweza kuandika wazo zaidi ya moja? Je, naweza kuandika kupitia Komputa alafu nika atachi hapa? Pia nimewaza ila so kwa umakini je, haya mawazo yatakua wazo mtandaoni au yatakua na Usalama kwa watumiaji wengine? Tafadhali Sana Ndugu msomaji mwenzangu tusaidiane hapa.
 
Nimesoma, nikasoma tena sasa najiuliza je, naweza kuandika wazo zaidi ya moja? Je, naweza kuandika kupitia Komputa alafu nika atachi hapa? Pia nimewaza ila so kwa umakini je, haya mawazo yatakua wazo mtandaoni au yatakua na Usalama kwa watumiaji wengine? Tafadhali Sana Ndugu msomaji mwenzangu tusaidiane hapa.
iNGIA KWENYE STORY AMBAZO ZIMESHAANDIKWA UTAJIFUNZA KITU
 
Nashukuru kwa taarifa nzuri kwa jamii; naam nikiwa sehemu ya jamii husika sitapenda fursa hii inipite. Naanza kuifanyia kazi kuanzia sasa; ewe mwenyezi Mungu/Allah/God naomba unisimamie, uniongoze katika kukamilisha hili na kupata matokeo chanya.

Nawashukuru pia waandaaji wa jambo hili.
 
Nashukuru kwa taarifa nzuri kwa jamii; naam nikiwa sehemu ya jamii husika sitapenda fursa hii inipite. Naanza kuifanyia kazi kuanzia sasa; ewe mwenyezi Mungu/Allah/God naomba unisimamie, uniongoze katika kukamilisha hili na kupata matokeo chanya.

Nawashukuru pia waandaaji wa jambo hili.
Karibu mkuu.

Usisite kuuliza ukikwama popote
 
Mkuu kwnye kipengele cha taarfa kwangu nimeona kwmba "YOU HAVE AWARDED TROPHY" ni ikasema "post a message somewhere to get your trophy's" ,pia nimeona kwmba machapisho Yangu yepata likes nyingne 250,nyingne zaidi ya 500 ,nyngne wanasema imewavutia watu zaidi ya 500, SASA sijaelewa Yani kwasbbu Mimi sina uelewa mkubwa Sana kwhye hivi vitu naomba nisaidie msaada nielewe zaidi mna nimepost machaposhao Yangu mawili ..
 
Nyie watu kumbe kuna hela yangu na imekaa kisiri hivi.
 
Jamani tunaanzia kuandika wapi hizi story zetu mbona sioni au kwa sms umuhimu ndio tunaandika story
 
UJUMBE KUHUSU MABADILIKO KIMAISHA

Nini maana ya kubadilika kimaisha?
maana yake ni namna au jinsi binadamu anatoka hatua moja kwenda hatua nyingine kimaendeleo katika nyanja zote za kimaisha kiuchumi,kijamii,kisiasa na kiutamaduni.


MAMBO MAKUU YA KUZINGATIA ILI UBADILIKE KIMAISHA NI YAFUATAYO:
1.Elimu
2.ujuzi ama kipaji ulichonacho
3.mtaji
4.fursa
5.masoko
6.nguvu kazi

1.ELIMU
Elimu ni jambo la msingi sana katika maisha ya binadamu ambapo humsaidia katika mambo tofauti katika jamii anayoishi nayo na kuwa mchanganuo mzuri wa mawazo katika kila jambo ambalo anahitaji kulifanya katika nyakati tofauti katika maisha ,pia humsaidia mtu kuishi vizuri na jamii anayoishi nayo ,pia elimu husaidia kutumia vizuri kipaji ama ujuzi ulionao.

2.UJUZI AMA KIOAJI ULICHONACHO
kila binadamu katika maisha ameejaaliwa kipaji binafsi kama vile kucheza mpira,kuendesha biashara mabalimbali,kubuni mitindo mbalimbali katika maisha pia kuwa na ujuzi katika kuendesha shughuli mbalimbali katika maisha hivyo kila binadamu anatakiwa kutambua na kukithamini kipaji binafsi alicho jaaliwa katika kufanya mambo tofauti ambayo huweza kumletea maendekeo katika maisha na hicho kipaji kwa namna moja ama nyingine huweza kumsaidia mtu kupiga hatua kimaendeleo endapo atakitumia vizuri katika maisha yake ya kila siku hivyo tunatakiwa kuthamini kipaji tulicho nacho hicho kipaji kinaweza kuwa msaada mkubwa sana na kumfanya mtu apige hatua kimaendeleo katka maisha.

3.MTAJI
mtaji ni kitu na jambo la muhimu sana ili mtu aweze kupiga hatua ama kubadilika kimaendeleo mtu anaweza akawa na elimu ,kipaji lakini akakosa mtaji ni sawa na kushindwa katika maisha hivyo tunatakiwa kutengeneza mtaji kwa mbinu ama njia tofauti tofauti moja uwezo binafsi wa mtu wenyewe,udhamini ama kuwezeshwa na watu au taasisi mbalimbali ikiwemo serikali ,pia kupata mikopo kutoka mabenki mbalimbali hivyo vyote vinaweza kumsaidia mtu kwa namna moja ama nyingine aweze kupata mtaji ili aweze kuendesha shughuli mbalimbali katika maisha na hicho kipato atacho pata kutokana na huo mtaji huweza kumsaidia kupata huduma mbalimbali ambazo binadamu anahitaji kuzipata katia maisha hasaa huduma za afya na nyingine nyingi ambazo binadamu anastahili kuzipata katika maisha ya kilasiku.

4.FURSA
pia fursa ni jambo la msingi sana katika maisha ya binadamu anapohitaji kupiga hatua ama kupata maendeleo katika maisha hivyo kama binadamu tunatakiwa kuwa waibuaji wazuri wa fursa katika jamii , hizo fursa tunaweza kuzitumia katika kuendesha shughuli mbalimbali katika jamii pia kutokuwa wategemezi wakubwa upande wa ajira kwa sababu tukizitumia vizuri fursa ambazo zipo katika jamii basi itakuwa ni msaada tosha kwetu ili tuweze kupiga hatua au kupata maendeleo chanya katika jamii hivyo kila mtu sehemu anapoiona fursa ni jambo la msingi sana kuitumia kwa maana ya kwamba tunaweza kubadili maisha yetu kuwa misha bota na yenye maendeleo katika maisha yetu kila siku hivyo fursa ni jambo la msingi sana.

5.MASOKO
Hili pia ni jambo la muhimu sana ili tuweze kupiga hatua katika maisha yetu ya kila siku na kuwa maendeleo pia katika kuishi kwetu masoko ni kitu muhimu sana kwa sababu vile vitu ambavyo tutakuwa tumeweza kuvizalisha katika shughuli mbalimbali nani mhusika wa kutafuta masoko ? jibu ni kwamba mtu wa kutafuta masoko ni mzalishaji wa bidhaa mwenyewe au mtu binafsi pia serikali inaweza ikawa chanzo kikubwa kutafuta masoko ndani ya nchi pia kutafuta masoko nje ya nchi ili raia waweze kupata masoko mazuri ambayo yatakuwa na tija katika mauzo husika na kuweza kuwapatia.wananchi kupata kipato kizuri kulingana na uzalishaji waliofanya bidhaa husika ,hivyo srwikali ina wajibu mkubwa sana kuweza kuwasaidia wananchi ili kuweza kupata wateja kwa.maana ya masoko yenyewe ili mwananchi anapofanya shughuli yoyote ya uzalishaji aweze kupata faida na kipato ambacho kitakuwa msaada katika kuendesha shughuli zao za kilasikuna kuwa na maisha bora na yenye tija ya kimaendeleo katika kuishi kwao.

6.NGUVU KAZI
Hili pia ni jambo la msingi sana kwa mtu anaye hitaji kupiga hatua katika maisha kwa ntu yeyote anayehitaji kupiga hatua na unahitaji kuendesha shughuli kubwa za uzalishaji kiuchumi unahitaji kuwa na nguvu kazi ambapo unaweza kuajili watu wenye elimu mbalimbali na wasio na elimu pia kwa kazi zisizo hitaji elimu maalumu ya kazi husika hivyo hawa waajiriwa wanaweza kusaidia katika maisha na kuweza kuendesha shughuli kisahihi na kwa maendeleo zaidi pia kutengeneza faida juu ya hughuli husika unayohitaji kuifanya. Ahsante
 
MAMBO YAKUZINGATIA HASA VIJANA
UMRI KUANZIA 18_40
1.matumizi mazuri ya mda
2.kuwa makini na sayansi na teknolojia kuitumia kwa maana inaweza kuleta maendeleo chanya katika maisha yetu na jamii kwa ujumla
3.kuwa makini kuhusu jambo la mahusiano pamoja ikiwemo na ndoa zenu
4.nidhamu
5.kukwepa uchochezi pia kutumiwa vibaya na wanasiasa kwa maana ya kuleta maendeleo hasi kwa jamii bali tunatakiwa kuwa watu wa mfano katika kuiongoza jamii
6.kuendelea kuitunza amani tuliyonayo
7.uzalendo
 
Back
Top Bottom