Shinyanga: Ajenti wa Basi la Kisibo akanyagwa na Basi hilo na kufariki hapo hapo wakati akirukia kwenye Basi hilo

Shinyanga: Ajenti wa Basi la Kisibo akanyagwa na Basi hilo na kufariki hapo hapo wakati akirukia kwenye Basi hilo

Mbona hao raia wamevaa gloves mzee baba, punguza chuki aisee, wameleta gari Ile pemben pale na hiyo machela,gloves, sasa na kubeba iwe kesi!???
Ni kweli, wananchi walifanya ubinadamu ukizingatia aliyefariki ni mwenzao pasipo kutathmini hatari wanayojiwekea pengine kutokana na ufinyu wa elimu. Hao waliovaa sare sasa tunaamini wao kidogo wana elimu na uzoefu wa matukio kama hayo na wanajua wazi tahadhari zinazopaswa kuchukuliwa pindi litokeapo tukio kama hilo na pengine ndio maana wameishia kuangalia kwa macho bila kushiriki kwa vitendo. Kwa kuwa wameonekana kutambua tahadhari zinazopaswa kuchukuliwa walishindwa hata kukimbia Pharmacy ya karibu hapo kupata Gloves ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeah ni bahati mbaya, karibia stendi zote wanafanya hivyo, kifo chake kilikuwa kimefika
The Humble Dreamer,
Wakati mwingine ni bahati mbaya tu maana mtu hiyo ni kazi yake ya kila siku, tusikike mbali kwa vile amekufa mtu. Inawezekana kabisa muda wa kifo chake umefika na kwa vile hatujui mambo ya kifo na siku ya kufa tunaweza kuongea mengi wakati ni mambo ya kawaida na bahati mbaya pia pole kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanaume aliyetambulika kwa jina moja la Athumani amefariki dunia mara baada ya kukanyagwa na gari hilo katika stendi kuu ya mabasi ya Shinyanga, mwili wake umepelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Taarifa zinasema kua Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Dar es Salaam lilimkanyaga Ajenti Athumani wakati akirukia kwenye Basi hilo na kisha kuangukia uvunguni mwa Basi na kukanyagwa na kufariki dunia hapo hapo.

View attachment 1400793

Polisi wako pembeni wanaangalia tu.

Pia wanaoonekani pichani wakimsaidia marehemu ni wananchi wakawaida sana, mashaka yangu ni je, wana uelewa wa kutosha juu ya maambukizi ya magonjwa ama virusi pindi ikitokea ajali ilihali wenye mavazi mazuri wamesimama wakitazama kama viongozi waelekezi tu?.....

Ushauri: Hii tabia ya kurukia gari au kushuka kwenye gari wakati gari hilo likiwa kwenye motion ni hatari sana. Watu wengi hufanya hivyo ili kuokoa muda au kuonyesha wepesi ila fahamu unahatarisha uhai wako. Ni vema usubiri gari lisimame ushuke.
Rest in peace brother Athuman, last week alinikatia tiket ya kuja dar pale nyegezi daah[emoji24]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio style zao wengime mpaka sasa ni vilema wamekanyagwaga miguu
Kifo bwana ,Hakina Hodi kabisa.


Inawezekana Marehem alikua ameshazoea kabisa kuruka namna hiyo!!


Pumzika kwa Amani ndugu.

"What is yours will always be yours no matter what "
 
Back
Top Bottom