Mimi binafsi, nafanyia shughuri zangu stand hiyo ya Shinyanga. Huyo Ajenti aliyefariki, ni kutoka Mwanza. Hivyo, alikuwa AMELISINDIKIZA hilo basi, lakini mpaka walipokuwa wamefika hapa SHY, alikuwa hajakamilisha kukabidhi hesabu zake, ili arudi Mwanza.
Kwa wasiofahamu mazingira ya Stand hii, wanaweza wakamlaumu Marehemu. Stand hii, ina askari, ambao wana chumba chao. Pia, Trafiki nao wana chumba chao, ambacho kipo kwenye geti la kutokea magari, ambapo ndipo alipokanyagiwa marehemu. Kwenye picha hiyo, huo ukuta wenye maandishi, kwa kushoto ndipo ulipo mlango wa hao Trafiki. Na pia, hapo ndipo ulipo mnyororo wa kuzuia magari kabla ya kutoka.
Lakini, ni kawaida magari kuingia na kuondoka kwa kasi, huku hao polisi wakishuhudia. Hapo alipokanyagwa marehemu, ni ndani ya stand.
Binafsi, nishashuhudia watu wakiuwawa na mabasi, hii ajali ni ya tatu. Mwaka jana, kuna mtu aligongwa kwenye mlango wa kuingilia na kufa, na mwingine alikanyagwa hapo hapo alipokanyagwa mtu leo.
Na imekuwa ni kawaida, mabasi kuwaacha abiria ambao wameenda kujisaidia, kwani yanakuwa na haraka, na kwa vile yanafukuzana.
Sina shaka, hao Trafiki na polisi wao wangekuwa wanatimiza wajibu wao, yaani mabasi yaingie na kuondoka kwa mwendo wa taratibu ndani ya stand, hizi ajari zingeweza kuepukika.
Sent using
Jamii Forums mobile app