Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 879
- 814
Hivi hapa Shinyanga kuna kiongozi wa mazingira? Viongozi wa mkoa wako wapi? Na wamafanya nini? Wale wa Wilaya vipi?
Kusema ukweli sisi wananchi wa Shinyanga tumekuwa tukiteseka kwa muda mrefu na maji machafu ambayo yamekuwa yakitiririka kutoka ndani ya kiwanda na kuja hadi kwenye makazi ya watu na mbaya zaidi ni kwamba yale maji yana harufu kali ambayo hata kwa sekunde hauwezi kuivumilia.
Yale maji yanatokana na uzalishaji wa kiwanda sasa yakitoka nje huwa na harufu kali kiasi kwamba yale maji yakigusa hata jani linaweza kukauka papo hapo, sasa yale maji yamekuwa yakitiririka na kuingia kwenye baadhii ya vyanzo vyetu vya maji.
Juzikati kwenye Mitaa ya Ngokolo, Kolandoto kuna Wanawake zaidi ya 10 ambao walikuwa wanalalamika mimba zao walizokuwa nazo kutoka sababu ya kutumia maji ambayo yamechanganyikana na maji machafu yanayotiririka hadi kuingia kwenye baadhi ya visima vilivyochimbwa na Wananchi.
Sisi Wananchi wa maeneo haya jirani tumeshawahi kulalamika haya kwa maafisa mazingira lakini kuna Afisa mmoja mazingira aliishia kufukuzwa kazi kutokana na shinikizo la wenye kiwanda hadi kwenye mamlaka zake za uteuzi.
Kiufupi Viongozi wengi wa serikali kwenye mkoa huu ni kama "wamewekwa Mfukoni" na jamaa na hakuna anayeweza kusimama mbele yake na kumueleza kuhusu maji hayo machafu anayoelekeza kutiririka hadi kuyakuta makazi ya watu.
Alienda mbali zaidi na kutishia kwamba ikitokea Mwandishi wa habari ameandika kuhusu maji hayo machafu ambayo hutiririka bila mpangilio basi Mwandishi huyo atapotea mara moja na haoni shida kufanya hivyo ili biashara yake iendelee kiukweli tunaumia sana.
Sasa mimi niliyeamua kuandika haya huenda maisha yangu yakawa hatarini zaidi endapo JF wakiamua kuniweka hadharani lakini kusema ukweli ipo haja kwa Serikali kutuangalia sisi wakazi wa Shinyanga na kadhia hii ya haya maji machafu.
Nasikia Viongozi wetu wa Kimkoa hawawezi kumwambia lolote eti kwakuea ni Mlipa kodi namba moja wa mkoa, hilo halizuii yeye kutimiza majukumu yake.
Tunaiomba Serikali kupitia kwa watu wa mazingira kuhakikisha yale maji machafu yanayotoka mule jambo yamadhibitiwa, maana hata ukiwa kwenye gari lako ukiwa umefungua kiyoyozi harufu inapenya hadi unafungua vioo, kiukweli hii haikubaliki.