Shinyanga: Mume aua mkewe na kisha kujilipua ndani ya nyumba kwa Petroli baada ya Wazazi wake kuvunja Ndoa yao

Haya matukio yamekithiri sana sijajua tatizo ni msongo wa mawazo au ni nini mpaka mtu anawaza kifo ni better option.
Ni jambo la kuangaliwa kwa jicho la tatu hali
Iyo minyororo alitoa wapi

Watoto watatu jamaa alikuwa bado hajaridhika tu kuuachia mzigo na wengine wahangaike nao.
Ndiyo ujue kwamba kuna wanawake wanaqualify kuwa wake. They have all good characters. Kutunza nyumba, kupika, politeness, heshima kwa mume na majirani nk
 
Wenslausi James (30) na Betha Kasimili (25), ambao ni wakazi wa kijiji cha Busongo kata ya Mwamashele wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga, wamefariki dunia baada ya mwanaume huyo kujilipua kwa moto kwa kutumia mafuta ya Petroli, kwa madai ya wazazi wa mwanaume kumkataa mwanamke.

Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga, Kamishina msaidizi wa Polisi, Jackson Mwakagonda, tukio hilo limetokea June 14 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi.

Mwakagonda amesema wanandoa hao walikuwa wamezaa watoto watatu, lakini wazazi wa mwanaume walimkataa mke wake, na kuamua kuuvunja mji pamoja na kurudisha mahari nyumbani kwao na mwanamke.

Aidha, amesema baada ya mji huo kuvunjika, ndipo mwanaume akasikia kuwa mke wake anataka kuolewa, na kuamua kwenda nyumbani kwa kina mwanamke akiwa na dumu la mafuta ya Petroli lita tano, na kisha kuingia chumbani kwa mwanamke na kufunga mlango na kisha kuanza kugombana.

“Mwanaume huyu alimchoma kisu cha ubavuni mke wake, na kisha kumfunga minyororo na kumwagia mafuta ya Petroli, kisha na yeye kujimwagia Petroli akawasha kiberiti na kujilipua moto, ambapo waliteketea pamoja na nyumba,” amesema Mwakagonda.

Aidha Kamanda ametoa wito kwa wazazi, kuacha kuingilia ndoa za watoto wao, pamoja na wanandoa kuacha kujichukulia sheria Mkononi, na pale penye migogoro bali watafute ufumbuzi kwa kufuata sheria.

Chanzo: Dar24

Yaani watu wamekaa wana watoto watatu mnavunja ndoa? Huu sio upuuzi ni nini?
 
Nadhani Wazazi walichokitafuta kwa Muda mrefu wamekibapa.
 
Mtoto kwa baba hakui,
Wameshazaa watoto 3 ndio munarudisha mahari?
Haya mulee yatima sasa
Anakuwa akifikisha miaka 18 mnakuwa wote watu wazima, hata maongezi yanatakiwa yabadilike yawe ya kushauriana wote na siyo amri hapo tatizo huyo kijana miaka 30 hakuwa na maamuzi yake na misimamo yake na hao wazazi walimchukulia mtoto na siyo mtu mzima mwenzao.
 
"pamoja na kurudisha mahari nyumbani kwao na mwanamke" mwanamke anarudishiwa mahari kwan yeye ndo alitoa hiyo mahari, mahari inatakiwa irudishwe kwao na mwanaume
 
Back
Top Bottom