Shinyanga: Mwalimu wa Madrasa atuhumiwa kulawiti wanafunzi 10

Shinyanga: Mwalimu wa Madrasa atuhumiwa kulawiti wanafunzi 10

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mwalimu wa Madrasa katika msikiti wa Mohamed Shunu uliopo Mtaa wa Shunu Kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama, aliyefahamika kwa jina moja la Faidhi anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za kuwalawiti wanafunzi 10 wa madrasa kwa nyakati tofauti kwa kuwarubuni kuwapa Sh 1000 na Sh 500

Akizungumza na EATV Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi, amethibitisha mwalimu huyo kukamatwa ambapo baada ya kufanya vitendo hivyo vya ukatili kwa watoto kuanzia umri wa miaka sita hadi 11 alitoroka na kukimbilia Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma na walipofuatilia wamemkamata na amerudishwa Kahama kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kamanda Magomi amesema Mwalimu huyo aliwarubuni watoto hao kwa kuwapa Sh 1000 na wengine Sh 500 kisha kuwafanyia kitendo hicho ambacho ni kinyume na maadili na kuwataka wazazi na walezi kuwafichuwa watu wanaowafanyia vitendo vya kikatili watoto wao badala ya kuwaficha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Shunu Manispaa ya Kahama, Joseph Kaliwa amesema alipata taarifa kutoka kwa wananchi siku ya Ijumaa juu ya kulawitiwa watoto na kushirikisha viongozi wengine ndipo walipoanza kufuatilia na kuandaa kikao cha wazazi ili kupata maelezo ya kina kisha watoto wote walikwenda kufanyiwa uchunguzi hospitali ya Rufaa Kahama na kubaini wameingiliwa.

Chanzo: EATV
 
Uku padri/mchungaji uku ostadhi/sheikh uku walimu watoto wetu tutawapeleka wapi aisee
 
Ingekuwa ni mtuhumiwa wa dini fulani wa upande wa pili hasa dhehebu lile, comments zingejaa waruhusiwe kuoa ...

Lakini huyu waleo utakuta ana mke zaidi ya mmoja na kafanya haya.

Anyway hatua kali zichukuliwe juu yake, haya mambo ni utashi wa mtu tu na hayafungamani na dini yoyote.
 
Na matokeo ya sensa wanaume n wachache laki ln ajabu kuna pumbav Lina kazana kufir**n[emoji26][emoji706][emoji706]
 
Halafu hao watoto wakikuwa na hiyo tabia ya kupenda kuingiliwa kwakuwa wamezoeshwa tunawasakama huku mtaani, ulezi kwa watoto wetu wa kiume umekuwa mgumu sana, inahitajika nguvu kubwa sana kuwalinda katika makuzi.

Watu kama huyo Sheikh na wengine wenye hizo tabia hukumu ya kunyongwa isingeepukika ili kuwa funzo.
 
Mungu tulindoe watoto wetu kila kona ni matatizo jamani. Sio kanisani sio msikitini sio mashuleni sio majumbani.

😭😭😭 Aiseh hapana
 
Halafu hao watoto wakikuwa na hiyo tabia ya kupenda kuingiliwa kwakuwa wamezoeshwa tunawasakama huku mtaani, ulezi kwa watoto wetu wa kiume umekuwa mgumu sana, inahitajika nguvu kubwa sana kuwalinda katika makuzi.
Watu kama huyo Sheikh na wengine wenye hizo tabia hukumu ya kunyongwa isingeepukika ili kuwa funzo.
Ndio basi tena washakua mashoga hao, kwenye list ya wanaume hawapo tena yaan wanaume 10 tumeshawapoteza tayari kwenye ile million 30,345,653 kumi washaleftishwa na Hostadhi mmoja

Hili kosa la kulawiti adhabu yake ilibidi iwe Kali sana
 
Back
Top Bottom