Shinyanga: Polisi wafanikiwa kuzuia ndoa ya binti aliyefaulu kwenda kidato cha tano

Shinyanga: Polisi wafanikiwa kuzuia ndoa ya binti aliyefaulu kwenda kidato cha tano

Ikiwa ni tofauti ya siku mbili tangu kuadhimishwa siku ya mtoto wa Afrika ilikwend ana kauli mbiu ya Mpe nafasi msichana boresha sheria ya ndoa na kuchagizwa na mabango yenye jumbe mbalimbali kama USINIPE MUME NIPE ELIMU.

Huko mkoani Shinyanga hali ni tofauti kabisa kwani imejitokeza tukio la kuozeshwa binti aliyefaulu na kuchaguliwa kwenda kidato cha tano. Wazazi wameona ni bora mtoto huyo akaolewe na kukatiza ndoto zake za kuendelea na maso.

=====
Jioni ya jana timu ya wataalam mbalimbali ikiambatana na Mhe Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christine Mndeme na vyombo vya DOLA wamefika katika kijiji cha Mwawaza na kufanikiwa Kuzuia NDOA ambayo Bi Harusi ni Mwanafunzi aliyechaguliwa kuingia kidato cha tano ila wazazi wake wakaamua KUMUOZESHA Sasa Hawa Wazazi watajua kuwa Shinyanga ya Mndeme ni ya ELIMU na SIYO kuoa WANAFUNZI.

Wampe na hela ya kuendea shule kabisa.
 
Nikikuuliza nionyeshe Id yake yoyote inayomtambulisha kama mwanafunzi sjui utanipa hoja gani.....

Id yake ya Uanafunzi ime-expire tarehe 31/12/2022 na mpaka sasa hana Id yoyote inayomtambulisha kama mwanafunzi wa shule flani......, Kwa mantiki hyo tayari anatambulika kama Raia wa kawaida mwenye haki zote za Msingi....

Hivyo kuingilia ndoa yake ni kama kuingilia uhuru wake na mawazo yake kwa Ujumla hivyo itampelekea kupata matatizo ya kisaikolojia mfano kutojiamini na kujiona mnyonge na asiye na thamani.

Mkuu wa Wilaya anapaswa kuwajibika kwa kumlipa fidia muathiriwa...

Nitafutieni namba za familia yao tukapande kizimbani tujibishane kidogo[emoji28]
Kwani bila ID mtu hawezi kuwa mwanafunzi ?
Na ID ya mtu huwezi sambaza kwa mtu mwingine,hivyo ukihitaji taarifa zake,shule anayosoma,nenda tu kwao utazipata vizuri,
 
Kwani bila ID mtu hawezi kuwa mwanafunzi ?
Na ID ya mtu huwezi sambaza kwa mtu mwingine,hivyo ukihitaji taarifa zake,shule anayosoma,nenda tu kwao utazipata vizuri,
Kama huwezi kupata taarifa zake bhas usije na hoja dhaifu ya kwamba ni mwanafunzi......,

Sema ni mwanafunzi ukiweza kuniletea Id au barua ya Mkuu wa Shule anayosoma kumtambulisha kama mwanafunzi wake pamoja na Maendeleo ya masomo yake hasa matokeo ya Muhula wa kwanza uliomalizika June 2023. Ukishindwa kunipa hvy vitu bhas huna haki wala kigezo chochote cha kumuita mwanafunzi.
 
Kupata taarifa za mtu hasa ID na kusisambaza ni jambo ambalo haliwezekani kufanyika kamwe,utasambazaje ID ya mtu wakati ni taarifa yake binafsi,kama unataka ushahidi na kuwatetea hao wanaoa wanafunzi ,tukutane mahakamani tukupe ushahidi,lakini humu,sahau kupata ID yake
 
Bhas hata Mahakamani kwenyewe twende halafu nitakuja na Id yake iliyoisha muda na wewe njoo na Id ambayo iko active
 
Bhas hata Mahakamani kwenyewe twende halafu nitakuja na Id yake iliyoisha muda na wewe njoo na Id ambayo iko active
Safi njoo na ID iliyoisha muda uje useme huyo siyo mwanafunzi,over
Tutakupa mke wako uondoke nae.
 
Nimeiona hii video ya binti kuvamiwa kwenye harusi-nimeshangaa sana.

Hivi kulikuwa na ulazima gani wa kuvamia harusi huku ukiwa na polisi wengi namna ile tena wenye silaha nzito?

Je ulipokuwa unafanya tukio hilo hukufikiri kuhusu athari za kisaikolojia atakazobaki nazo huyo binti-ambaye wewe unaona kama unamsaidia?

Haujawatendea haki hao watoto pamoja na wazazi wao.

Ni kosa wamefanya lakini utaratibu uliotumika kusolve tatizo utaharibu zaidi kuliko kujenga.

Hilo tukio litamuathiri binti muda mrefu na huenda likasabisha akaichukia zaidi hiyo shule yenyewe.

Ingekuwa vema ungezuia hili tukio kabla au baada na si wakati linaendelea ili kulinda saikolojia za hao watoto au hata wakati linaendelea lakini kwa utaratibu unaofaa.

Nimeuliza swali hili Mkuu, ila kuna popoma flani limekuja likaandika ujinga ujinga kwenye hoja yangu! Nadhani tunatakiwa kusolve tatizo bila kutengeneza tatizo.
 
Back
Top Bottom