Shinyanga: Rais Magufuli amuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi RPC na RCO, pia aagiza meneja wa TRA kusimamishwa kazi

Shinyanga: Rais Magufuli amuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi RPC na RCO, pia aagiza meneja wa TRA kusimamishwa kazi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Rais Magufuli amemuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi Kamanda wa Polisi wa mkoa na Afisa upelelezi wa mkoa wa Shinyanga kutokana na tuhuma za kuhujumu uchumi.

Kadhalika Rais Magufuli amemuagiza Kamishna mkuu wa TRA kumsimamisha kazi Meneja wa TRA mkoa wa Shinyanga kwa tuhuma za kuhujumu uchumi.

Mwisho Rais Magufuli amemuagiza Waziri mkuu mh Majaliwa kuunda tume ya kuvhunguza sakata hilo mara moja.

IMG_20191123_202810_790.jpg


Leo Jumamosi tarehe Novemba 23, 2019 sisi wafanyabiashara wa Shinyanga tumefurahi sana kupata taarifa za hatua kali zilizochukuliwa dhidi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga (RPC) ACP Richard Abwao na RCO wake SSP John Rwamlema ambao wamesimamishwa kazi baada ya kuonesha utovu wa nidhamu kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.

Tumeamini kweli Serikali ina mkono mrefu na hasa kipindi hiki cha Rais Magufuli ambaye hataki mchezo kabisa linapokuja suala la maslahi ya nchi.

RPC na RCO wa Shinyanga kwa kushirikiana na Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Bw. Jumbe Lazarous Samson wamefanya madudu mengi ambayo yamesababisha hasara kubwa sana kwa serikali. Hata hili la kumuachia mfanyabiashara aliyekuwa anakwepa mabilioni ya kodi ya serikali kwa kubandika stika zilizopitwa na wakati katika vinywaji vikali ni moja ya matukio mengi ya uhujumu uchumi unaosababisha upotevu mkubwa wa fedha za Serikali yanayofanywa na wafanyabiashara wenzetu mbalimbali lakini kila ukitoa taarifa kwa TRA au polisi hakuna hatua zinazochukuliwa.

Tulishangazwa sana tulipoona mkuu wa mkoa na kamati yake ya ulinzi na usalama ya mkoa wamefanya kazi kubwa ya kumkamata mtuhumiwa aliyekuwa anakwepa kodi kupitia biashara ya vinywaji vikali lakini polisi hawachukui hatua zinazostahili.

Kuna taarifa kuwa walipofikishwa polisi, RPC na RCO wake walikuwa wakishirikiana na mtuhumiwa kukwepa mkono wa sheria kwa kujipanga kuharibu kesi ambayo ina ushahidi wa wazi na ambayo serikali imepoteza mapato makubwa.

Kwa hiyo tuliposikia kwamba jambo hili limefika kwa mkuu wa nchi na hatua zimechukuliwa kuwaondoa katika nafasi zao tumepata matumaini kuwa serikali hii ya Magufuli haitaki mchezo.

Tunaamini kuwa watuhumiwa hawa watachunguzwa kwa undani kwa sababu tunafahamu matajiri wengi wakiwemo wakandarasi na wageni hasa wachina ambao wamekuwa wakileta jeuri na hata Mkuu wa Mkoa akiagiza wakamatwe polisi wanawaachia na wanarudi mtaani wakitamba.

Bila shaka baada ya kuondolewa kwa vigogo hawa sasa mkoa wa shinyanga utakuwa shwari, mkuu wa mkoa ataheshimiwa na maagizo yake yatatekelezwa kuliko ilivyokuwa ambapo baadhi ya maafisa wa serikali katika mkoa walikuwa wanajiona wao ni wakubwa kuliko mkuu wa mkoa ambaye ameteuliwa na Rais kumwakilisha hapa Shinyanga.

Tunamuomba IGP Sirro awaangalie makamanda wa polisi wake na maafisa wa polisi katika mikoa wengi wamekuwa miungu watu, wanajiona wao ndio wakuu wa mikoa, hawataki kuheshimu mamlaka ya mikoa

Ni sisi wafanyabiashara wa Shinyanga.
Novemba 23, 2019
 
Yeye aendelee kuchukua hatua wenzake wako kimya wamechukua ndege
 
Naona watu wengi hawajaona dhima kuu ni hilo swala la kupokea gawio ambalo kimsigi ilibidi lifanyike jumatatu sema sababu kesho ndo siku ya kupiga kura anataka ku shift attention ili jumatatu magazeti yaripoti kuhusu gawio badala ya kuripoti watu wachache watakao kuwepo kwenye vituo vya kupiga kura hahaha
 
Rushwa, Uhujumu Uchumi
Utakatishaji Wa Fedha
Police Kwanini Mnamuangusha Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Kumbe huyu RPC ni mchaga hongera zao kwa wizi hata yule wa kagera aliyetumbuliwa kwa kusafirisha kahawa usiku kimagendo kwenda Uganda alikuwa mchaga

Wako wapi mramba na ,mgonja na yona walikaa jela wakati wa jk

State agent
 
Hayo sasa ni maamuzi ya "kizembe"

Hivi hawa akina Bashite, wenye makosa makubwa zaidi, ni kwanini hataki kuwatimua kazi??
Fanya wewe kama una mamlaka kama alivyofanya mheshimiwa au kuna jamaa yako kati ya hao wahujumu uchumi?
 
ACP Richard Abwao na SSP John Rwamlema karibuni uraiani..

msijisikie wanyonge sana

nakutabirieni pia nyie sio wa mwisho,bado kuna na wengine na tabia kama zenu watafukuzwa...mjifariji

Zaidi hii ni rotation..

Tunzeni zile 'hela zetu' japo zitaisha..

hamtatetemekewa tena,muanze kujifunza kupanga mistari benki,na kukaa siti za nyuma na kusalimia 'binadamu' wenzenu.

Meneja wa TRA ume fail mno,japo utakuwa umeingizwa mkenge na hao mapoti.

TIMAMU.
 
Back
Top Bottom