Shinyanga: Rais Magufuli amuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi RPC na RCO, pia aagiza meneja wa TRA kusimamishwa kazi

Shinyanga: Rais Magufuli amuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi RPC na RCO, pia aagiza meneja wa TRA kusimamishwa kazi

Mkuu unazungumzia mfanyabiashara wa kiwanda cha vinywaji vikali vya SHUJAA or something!
 
Cybercrime ni mfanyabiashara gani kaleta hili soo?

Kuna vijana wamesota wiki mbili rumande kwenye issue hii related na ukwepaji kodi na stika halafu wametoka kwa mlango wa uani.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya RFA saa nne, Rais Magufuli amemwagiza IGP kuwasimamisha kazi na kuanzisha uchunguzi wa tuhuma za uhujumu uchumi dhidi ya RPC na RCO wa shinyanga
Aidha amemwagiza kamishna mkuu wa TRA kumsimamisha meneja wa Tra wa mkoa huo pia kwa tuhuma za uhujumu uchumi.

Hata hivyo tuhuma husika hazikuelezwa.
 
Inaonekana umefurahi sana hadi unaandika kisukuma hapa.
 
Rais Magufuli amemuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi Kamanda wa Polisi wa mkoa na Afisa upelelezi wa mkoa wa Shinyanga kutokana na tuhuma za kuhujumu uchumi.

Kadhalika Rais Magufuli amemuagiza Kamishna mkuu wa TRA kumsimamisha kazi Meneja wa TRA mkoa wa Shinyanga kwa tuhuma za kuhujumu uchumi.

Mwisho Rais Magufuli amemuagiza Waziri mkuu mh Majaliwa kuunda tume ya kuvhunguza sakata hilo mara moja.

View attachment 1270514

Leo Jumamosi tarehe Novemba 23, 2019 sisi wafanyabiashara wa Shinyanga tumefurahi sana kupata taarifa za hatua kali zilizochukuliwa dhidi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga (RPC) ACP Richard Abwao na RCO wake SSP John Rwamlema ambao wamesimamishwa kazi baada ya kuonesha utovu wa nidhamu kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.

Tumeamini kweli Serikali ina mkono mrefu na hasa kipindi hiki cha Rais Magufuli ambaye hataki mchezo kabisa linapokuja suala la maslahi ya nchi.

RPC na RCO wa Shinyanga kwa kushirikiana na Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Bw. Jumbe Lazarous Samson wamefanya madudu mengi ambayo yamesababisha hasara kubwa sana kwa serikali. Hata hili la kumuachia mfanyabiashara aliyekuwa anakwepa mabilioni ya kodi ya serikali kwa kubandika stika zilizopitwa na wakati katika vinywaji vikali ni moja ya matukio mengi ya uhujumu uchumi unaosababisha upotevu mkubwa wa fedha za Serikali yanayofanywa na wafanyabiashara wenzetu mbalimbali lakini kila ukitoa taarifa kwa TRA au polisi hakuna hatua zinazochukuliwa.

Tulishangazwa sana tulipoona mkuu wa mkoa na kamati yake ya ulinzi na usalama ya mkoa wamefanya kazi kubwa ya kumkamata mtuhumiwa aliyekuwa anakwepa kodi kupitia biashara ya vinywaji vikali lakini polisi hawachukui hatua zinazostahili.

Kuna taarifa kuwa walipofikishwa polisi, RPC na RCO wake walikuwa wakishirikiana na mtuhumiwa kukwepa mkono wa sheria kwa kujipanga kuharibu kesi ambayo ina ushahidi wa wazi na ambayo serikali imepoteza mapato makubwa.

Kwa hiyo tuliposikia kwamba jambo hili limefika kwa mkuu wa nchi na hatua zimechukuliwa kuwaondoa katika nafasi zao tumepata matumaini kuwa serikali hii ya Magufuli haitaki mchezo.

Tunaamini kuwa watuhumiwa hawa watachunguzwa kwa undani kwa sababu tunafahamu matajiri wengi wakiwemo wakandarasi na wageni hasa wachina ambao wamekuwa wakileta jeuri na hata Mkuu wa Mkoa akiagiza wakamatwe polisi wanawaachia na wanarudi mtaani wakitamba.

Bila shaka baada ya kuondolewa kwa vigogo hawa sasa mkoa wa shinyanga utakuwa shwari, mkuu wa mkoa ataheshimiwa na maagizo yake yatatekelezwa kuliko ilivyokuwa ambapo baadhi ya maafisa wa serikali katika mkoa walikuwa wanajiona wao ni wakubwa kuliko mkuu wa mkoa ambaye ameteuliwa na Rais kumwakilisha hapa Shinyanga.

Tunamuomba IGP Sirro awaangalie makamanda wa polisi wake na maafisa wa polisi katika mikoa wengi wamekuwa miungu watu, wanajiona wao ndio wakuu wa mikoa, hawataki kuheshimu mamlaka ya mikoa

Ni sisi wafanyabiashara wa Shinyanga.
Novemba 23, 2019
Sirro naye anapaswa kutumbuliwa.Yeye hakuona madudu ya maofisa wake mpaka Rais atoke Dodoma ayaone?He is part of the problem.He should also go.
 
Ilitakiwa tume iundwe kimya kimya wakawachunguze kabla hawajastopishwa kikazi
 
Abwao huyu ni mchaga wa machame kwao na mbowe ,hawa wachaga na wizi ni unyayo na soks ,hata yule RPC wa kagera aliyepigwa chini kwa rushwa naye ni mchaga pia

State agent
kuna ulazima gani kuandika mambo usiyojua? acha ONGO Mkuu
 
Abwao huyu ni mchaga wa machame kwao na mbowe ,hawa wachaga na wizi ni unyayo na soks ,hata yule RPC wa kagera aliyepigwa chini kwa rushwa naye ni mchaga pia

State agent
Abwao ni mjaluo
 
Hii habari pamoja na kuwa kubwa lakini haina muendelezo wowote hadi leo.

Mtuhumiwa hatajwi lakini taarifa zilizopo ni kwamba hayupo mikononi mwa polisi (alitoroka)
 
Kuna watu walishajihakikishia kuishi bila kusumbuliwa hapa bongo!!
 
Back
Top Bottom