Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
WATU watatu wanashikiliwa na Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa tuhuma za kumpeleka mtoto wa miaka mitatu baa na kumywesha bia huku wakimchukua video na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP, Debora Maligilimba, ilisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo, Aprili 24, majira ya saa sita mchana, katika baa moja Kijiji cha Nyaligongo, Kata ya Mwakitolyo.
Kamanda Magiligimba alisema, kitendo hicho ni ukatili dhidi ya mtoto na matumizi mabaya ya kimtandao na kwamba waliomnywesha bia walisikika wakimwambia amalize wampe nyingine.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Godius Katisha (32), mkazi wa Mwakitolyo ambaye ni mmiliki wa baa hiyo, Alphonce Pima (32), mkazi wa Mwakitolyo na Oscar Makondo (35), mkazi wa Mtaa wa Mayila Mjini Kahama.
Kamanda Magiligimba alisema baada ya tukio hilo kuonekana kwenye mitandao ya kijamii, kikosi kazi cha askari wa uhalifu wa makosa ya kimtandao waliwakamata watuhumiwa hao akiwamo Katisha ambaye ni baba mzazi wa mtoto huyo.
Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Kamanda Magiligimba aliwataka wananchi kuheshimu haki za mtoto na yeyote atakayeenda kinyume hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Juzi baada ya video hiyo kusambaa kwenye makundi ya mtandao wa Whatsapp, wananchi waliomba hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa wahusika ikiwamo kuwafikisha mahakamani pamoja na kuifunga baa hiyo.
Chanzo: Nipashe