Shirika la Fedha Duniani (IMF) laahidi kuipatia Tanzania fedha itakayoihitaji

Shirika la Fedha Duniani (IMF) laahidi kuipatia Tanzania fedha itakayoihitaji

mnyalilungulu

Senior Member
Joined
Sep 27, 2019
Posts
170
Reaction score
114
3 (1).JPG

Mkurugenzi Mkazi wa IMF Tanzania, Jens Reinke akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam. ​

Mkurugenzi Mkazi wa IMF nchini Tanzania, Jens Reinke ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamamba Kabudi leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Aidha Reinke, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua madhubuti inazozichukua katika kukabiliana na janga la Covid-19 ili kuepusha madhara ya kiuchumi na kijamii.

Mazungumzo hayo pia yamelenga miradi ya maendeleo, msamaha wa madeni kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, ushirikiano baina ya IFM na Tanzania, biashara na utalii.

Kwa upande wake, Prof. Kabudi ameishukuru (IMF) kwa msamaha wa madeni ambao umetolewa kwa Tanzania na nchi nyingine, fedha zitakazoziwezesha nchi hizo kuendelea kukabiliana na Covid-19.

"Tumeongelea mambo mbalimbali yanayohusu ushirikiano hasa katika kuimarisha uchumi wetu baada ya janga la covid 19, usirikiano kati ya Tanzania na IMF unafahamika na tumekubaliana baadhi ya mambo ambayo tutayafanyia kazi kwa kina ili tuweze kuimarisha uchumi wetu baada ya corona hasa katika sekta ya utalii, biashara na miundombinu," amesema Prof. Kabudi.

Chanzo: IPP Media
 
Tutaelewana tu Tanzania ni nchi huru na yenye ushawishi mkubwa kwa mataifa ambayo ni marafiki wa Tanzania. IMF wanafahamu nguvu ya Tanzania hasa katika kanda hii, tupo vizuri na wao wanafahamu ukimwona simba kalala usichezee mkia wake.
 
Kwenye psychology hii tunaiita 'positive/ negative reinforcement', mbumbumbu wa lumumba hamuwezi kuelewa hii.

IMF inawapa matumaini na masharti fulani fulani, ukitii unapewa msaada (zawadi ya utii), usipo tii unanyimwa msaada ambao ulikwisha upigia mahesabu (adhabu ya ukaidi).

Kwa kutumia mbinu hii masikini yeyote lazima arudi kwenye mstali na atii maagizo ya wakubwa
 
Kwenye psychology hii tunaiita 'classical conditioning', mbumbumbu wa lumumba hamuwezi kuelewa hii.

IMF inawapa matumaini na masharti fulani fulani, ukitii unapewa msaada (zawadi ya utii), usipo tii unanyimwa msaada ambao ulikwisha upigia mahesabu (adhabu ya ukaidi).

Kwa kutumia mbinu hii masikini yeyote lazima arudi kwenye mstali na atii maagizo ya wakubwa
Tuliza kichwa ndo uandike,ona sasa ujinga ulioandika!
 
Kwenye psychology hii tunaiita 'classical conditioning', mbumbumbu wa lumumba hamuwezi kuelewa hii.

IMF inawapa matumaini na masharti fulani fulani, ukitii unapewa msaada (zawadi ya utii), usipo tii unanyimwa msaada ambao ulikwisha upigia mahesabu (adhabu ya ukaidi).

Kwa kutumia mbinu hii masikini yeyote lazima arudi kwenye mstali na atii maagizo ya wakubwa
Wacha uongo Tanzania walishasema kama hutaki kufuta madeni sisi tutaendelea kukulipa tu na hatuna wasiwasi. JFYI Tanzania ina uwezo wa kulipa deni lake kila mwezi kiasi cha USD 300,000 na kuendelea kuwekeza kwenye miradi yake ya kimkakati.

Kuweza kukopa madeni mapya nk. IMF wanafahamu Tanzania ikifanikiwa tu biashara yao itakufa siku za usoni. Vile vile wanafahamu ndio itakuwa mwisho wa mtu mweupe komwonea mwafrika. The bigger picture is bigger than what you think! Come out of that small box. JPM is showing Africans how is done and the white men is worried.
 
Lazima tupinge maana huu ni urafi. Haiwezeni donor country kama Tanzania kulialia njaa na kuomba misaada tena kwa maadui wetu wa uchumi hao mabeberu.

yesu wa CCM amekua akisema viongozi waridhike. Kwanini donor country tunageuka ombaomba kwa mabeberu wakati sisi ni nchi tajiri!??
Chadema watapinga
 
Hivi Hilo jicho kabudi ndo kuwatisha hao watu au..😂😂😂😂
 
Kwenye psychology hii tunaiita 'positive / negative reinforcement', mbumbumbu wa lumumba hamuwezi kuelewa hii.

IMF inawapa matumaini na masharti fulani fulani, ukitii unapewa msaada (zawadi ya utii), usipo tii unanyimwa msaada ambao ulikwisha upigia mahesabu (adhabu ya ukaidi).

Kwa kutumia mbinu hii masikini yeyote lazima arudi kwenye mstali na atii maagizo ya wakubwa
Duh, mateka wa Mbowe ni mtaalam wa psychology!
 
Hivi ni shirika la fedha au ni shirika la usimamizi wa fedha.
 
Wacha uongo Tanzania walishasema kama hutaki kufuta madeni sisi tutaendelea kukulipa tu na hatuna wasiwasi. JFYI Tanzania ina uwezo wa kulipa deni lake kila mwezi kiasi cha USD 300,000 na kuendelea kuwekeza kwenye miradi yake ya kimkakati. Kuweza kukopa madeni mapya nk. IMF wanafahamu Tanzania ikifanikiwa tu biashara yao itakufa siku za usoni. Vile vile wanafahamu ndio itakuwa mwisho wa mtu mweupe komwonea mwafrika. The bigger picture is bigger than what you think! Come out of that small box. JPM is showing Africans how is done and the white men is worried.
Kwa mujibu wa taarifa toka kwa JPM malipo ya USD laki 3 kila mwezi sawa na (TZS 694.2 bn) na kwa mwaka ni sawa na USD 3.6mil (sawa na TZS 8.33 Tril )

Kwa lugha rahisi sana, kwenye kila tril moja ya makusanyo ya TRA ya mwezi, 694 bn goes to IMF ku-service deni.

Yet, wakati wa Covid19 wanataka kutokopesha fedha ili kukidhi mahitaji ya muda mfupi ambayo hayana uhusiano moja kwa moja na kuzalisha mali au kuongeza thamani hasa kwenye mazao ya kilimo ambako ndiko mnyororo wake wa thamani una multiplier effect kubwa.

Mathalani, mwaka huu bei ya ufuta imeanguka. Kwanini serikali (wizara za kilimo, viwanda na biashara, uwekezaji na fedha) ingetoa bank guarantee ili wenye investment project za kuchataka mafuta ya kula na mafuta ya kujipaka (essential oil) na mashudu kama chakula cha wanyama;
rejea hapa chini nimetoa mfano wa business model ya ufuta
Rais atavunja Bunge la JMT mwezi Juni. Tuko wapi na tunafika lini nchi ya asali na maziwa?

Kuna mazao ya kimkakati kama korosho, kahawa, chai, mkonge, pamba; kwa serikali kutoa bank guarantee inaweka vijana wake kwenye kila investor ili ku-monitor kila process ili investor asi-divert fund.

Uzalishaji ukianza ndani ya muda mfupi, tax base itakuwa kubwa na likely in the course of servicing the loan, pia kuna fedha nyingine zinabaki ndani kujenga uchumi na kuongeza vyanzo ajira kwa vijana.

Chonde chonde, tunaomba JPM urejee sehemu ya speech yako kwenye SADC summit ili mimi na yule mwenye investment project, tupate project financing ili tuchakate mazao ghafi ya kimkakati na ku-export final produce kutoka Tanzania.

Watanzania wenye akili tuna imani kubwa sana na JPM na with a big picture, tuna nafasi ya kufanya mengi makubwa pale serikali yako ikitushika vijana mkoni na kujenga legal framework ya kuruhusi project investment financing isiwe complecated

Shalom
 

Attachments

  • JPM SPEECH OPENING SADC.mp4
    11.2 MB
Back
Top Bottom