Shirika la Reli Tanzania wamepata wapi pesa za kununua Magari ya kifahari ilhali hawaliingizii taifa faida yoyote zaidi ya kutoa huduma?

Pengine ni magari ya wakandarasi😅😅
 
Pale unapokuta maskini anaishi Luxury life kuliko wewe tajiri tena unampa na misaada😅😅
 
We lipa tozo,sie huku tunakula kwa urefu wa kamba,manunuzi yanafanyika serikalini Ili watu wapige Cha juu,na kwa jinsi mama asivyojua kitu,hiki ni kipindi Cha kuupiga mwingi,ni kutembelea ma V8 tu,kwenye mashirika ya umma,wakubwa waandamizi wanajikopesha tu pesa ya umma,
 
Treni daladala pugu station kwa siku walliingiza milioni 20 kwa siku
Ukitoa gharama za uendeshaji wanabakia na kiasi Gani za kununua Magari zaidi ya mia ya thamani inayopindukia milioni 300 Kila Moja?
 
Mimi nashauri tuendelee Kama Watanzania kutoa tozo kwa moyo,nguvu,akili na maarifa yetu yote ili viongozi wetu na wasaidizi wao waendelee kuishi maisha mazuri!
 
Mkuu ruzuku ya kununua V8 zaidi ya mia siyo mchezo.
Mkuu nchi yetu ni ngumu sana. Kwa kifupi fedha zingekuwa zinatumika bila ufisadi au matumizi yasiyo na lazima basi tusingehitaji msaada wowote na shule na hospital zingekuwa bure na huduma bora kabisa. Na awamu hii ukiambiwa fedha zinavyopigwa basi unaweza kuzimia. Na mwenyewe amekaa anatumbua mi-macho tu.
 

Acha kupotosha watu mzee gari zote unazoziona zina namba RAC zote ni gari ambazo zinatumika kwenye mradi wa SGR.

unaweza kuziona za ufahari lakini kumbuka huko kwa wenzetu ni bei ya mbuzi tu na zote hizo zimeingia kwa msamaha wa kodi
 
Mkuu ngoja nikuambie neno, ili usilete kuchongea watu bila sababu. NI kwamba katika sheria ya manunuzi ya serikali inasema kabisa magari gani yanapaswa kununuliwa, na huwa ni hizo Landcruiser na Pick up double cabin. Wakati fulani ilikuwa ni Land Rover Defender 110. Kwa hiyo hawa watu hawajiamulii, bali ni sheria inawapeleka kununua hayo magari. Bila hiyo sheria ungekuta wananunua Range Rover, Lexus, Jeep, BMW X5, Mercedes GLS nk.

Kuna wakati mradi wa EU hapa nchini walipata matatizo kwa kuwa wao walitaka kuagiza magari ya Ulaya, lakini sheria ikawa inawabana kununua magari ya Japan kulingana na sheria ya manunuzi ya Tanzania. EU wakaona kama wanalazimishwa kuwa promote Wajapan wakati fedha ni za Ulaya.

Kwa hiyo usimlaumu mtu wa serikalini au shirika la umma kununua hizo V8
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…