rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 18,360
- 26,244
Shirika la umeme la Zanzibar limekiri kudaiwa na shirika la umeme TANESCO deni la shilingi bilioni kumi lakini limesema halitalipa bali deni hilo litalipwa na Serikali ya muungano.
Limesema Serikali ya muungano inadaiwa na Serikali ya Zanzibar kwa hiyo watakatana hukohuko.
Kwanza haijulikani ni deni gani ambalo Serikali ya muungano inadaiwa na Zanzibar. Pili kwa muda mrefu inasemekana Zanzibar imekuwa haichangii gharama za kuendesha Serikali ya muuungano. Tatu kama kweli Serikali ya muungano inadaiwa na Zanzibar ni vema ikaweka hadharani deni hilo.
Watanzania bara tumekuwa tukipandishiwa umeme huku upande wa pili hawalipi hapo ndio utaona umuhimu wa serikali tatu.
Chanzo: Habari ya ITV