Uchaguzi 2020 Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake

Nawaza kwa mbali,
Ivi ndio CHADEMA wametinga IKULU KIMASIHARA TBC itaendelea kufanya kazi kama miaka yote?
Watageuka wapambe hata Zambia ilikuwa hivyo hivyo baada ya Michael Chilufya Sata kushinda vyombo vya habari vyote vilivyokuwa against yeye kesho yake viligeuka na kuanza kumpamba na kuponda chama tawala.
 
Mi sina chama lkn walichofanya CHADEMA ni upuuzi, walitakiwa kuwaacha waendelee na kazi yao. Kwa tendo lile ilikuwa ni hatari kwa usalama wa vyombo vyao na wakijua watangazaji pia. TCRA wana sheria na kanuni za maudhui, TBC hawataki kuingia mgogoro wa kulipishwa faini na TCRA.
 
tbc acha lawama , mnasema mnafuata maudhui ,ok sawa nakubali ila elewa nafikili hamkutakiwa kwenda maana kumbuka hiki ni kipindi cha kampeni watu watamwaga nyongo sana , sasa leo mlitia fora watu wakianza kumwaga nyongo mwajifanya kuweka uchambuzi , raha ya siasa ni wana siasa kumwaga nyongo ili mladi usiwe umbea au kumsingizia mtu , au kumtukana mtu, niwashauri achana na mikutano ya chadema basi ,mbona tangu mwanzo mlikua hamuonyeshi kipi leo kimewapeleka
?
 
Asiwalaumu Chadema, watazamaji ndiyo tulitaka wafukuzwe kwani hatukuwa Tayari kuwasikiliza wao badala wahusika wa mkutano. Kuhusu maudhui wasijifanye wao ni watabiri, wanawezaje kujua kitakachosemwa, sheria inahusu kilichoandaliwa na si anachokitamka mtu ghafla na hakukua na neno lolote baya.
 
Mbowe alikosea pale ilikuwa wapewe dakika tano tu,kumi tano zilikuwa nyingi sana.
Hata hivyo iwe fundisho .....Kamanda wa anga alipaswa ndio apeperushe bendera kwa ujasiri ambao ameuonesha
 
Mheshimiwa Daktari Ayoub Ryoba,
Mengi ya kufurahisha na ya karaha yamefanywsa na TBC tumeyapokea kabla ya uongozi wsako na sasa kipindi cha uongozi wako.

Binafsi nilikupenda nilipokuwa nasoma makala zako na kukusikiliza katika radio na vipindi kadhaa vya runinga namna ulivyokuwa unachambua hoja kama mtu mwenye mawazo huru. Nilijivunia wewe, kama ambavyo nimeendelea kujivunia Jenerali Ulimweengu.

Lakini, kilichofanyika leo..kilichofanywa leo na wqafanyakazi wwalio chini yako (nashindwa kuamini kwamba ulikuwa huoni kilichokuwa kinafanywa). Umeyaona, ukanyamaza kimya. Umeona reaction ya wananchi, bado umenyamaza kimya. Dr Ayoub, utu uzima busara...kuomba radhi nao ni uungwana.

Kilichotokea leo kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA ni aibu kwa TBC, ni aibu kwa Taifa kutoka kwwa waale waliokuwa wakiangalia toka mataifa mengine..ni aibu kubwa kwsa tasnia ya habari...ni mfululizo wa aibu aibu.

Jambo walilolifanya leo TBC si mara ya kwsanza. Mwaka 2015 pale Jangwani wsalifanya hivyo na Mar. Marin Hassan aliponea chupu chupu kipigo kikuu, nakumbuka aliokolewa na red brigade..hata gari la TBC ilibidi lizingirwe na Polisi. Ndipo, viongozi wa UKAWA waalilazimika kuwaatuliza wsananchi. Leo tena, vijana wako wamepanga na kutimiza walichopanga. Kilichofanywa na TBC leo ndicho kilichofanywa na Global TV online. Inathibitisha ni mpamgo wa makusudi.

Najua unajua kuwa kuna kuwajibika kwsa makosa ya wale waliochini yako.

Nasubiri busara zako..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…