Shirikisho la Soka Afrika CAF yataja Klabu ya Simba SC nafasi ya 5 kwa utajiri Barani Afrika

Shirikisho la Soka Afrika CAF yataja Klabu ya Simba SC nafasi ya 5 kwa utajiri Barani Afrika

Status
Not open for further replies.
€10,32 hivi hiyo ndio milioni ????

Kwenye maelezo umesema utajiri wa simba ni Paundi(£) ila Kwenye namba naona kuna alama ya Euro (€) , hivi unaelewa umechoandika kweli ?
 
Awa caf wehu sana.team haina hata uwanja eti inaipiku utajiri zamaleki

Au wamehesabu utajiri wa Mo wakaufanya ndio wa mikia.

Unajua maana ya Brand?

Unajua formula ya ku calculate brand ya kitu kujua value yake?
Unajua determinants za brand?

Tuanzie hapo kwanza wakati unatafuta penseli na Daktari la mistari mirefu na mifupi upate darsa
 
Hawa ndio waongo kabisa labda bongo hawaijui vizuri. Hakuna timu yoyote bongo ambayo ina akiba benki angalau milioni 10 tofauti na AZAM ambayo ni kampuni ya mfanyabiashara
 
Weka link ya hiyo habari tujisomee wenyewe
 
€10,32 hivi hiyo ndio milioni ????

Kwenye maelezo umesema utajiri wa simba ni Paundi(£) ila Kwenye namba naona kuna alama ya Euro (€) , hivi unaelewa umechoandika kweli ?
Ni sahihi kuwa £10. 35 nimeweka hiyo kutokana na screen shot kutoka kwenye Chanzo kutoka Johannesburg.. Ndo maana nimeandika kwa ufasaha hapo kwenye thread mkuu.
 
TP Mazembe kama haipo top 3 hyo list itakuwa imepikwa

mleta mada hujui kama kupika data fake ni kosa la jinai?
 
Kwamba hata Tp mazembe tumewapita[emoji16] [emoji16] .

Labda kwa tafsiri ileee ya cherehani mbili TUU KIWANDA
 
Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es salaam imetajwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kuwa klabu namba 5 kwa utajiri Barani Afrika.

Simba SC imetajwa kuwa na utajiri wa karibu Paund milioni 10.35 ambayo ni sawa na Bilioni 32.3 kwa shilingi ya Tanzania.

Katika orodha hiyo Al Ahly kutoka Misri inaongoza ikiwa na utajiri wa Paund milioni 19.25 ikifuatiwa na Esperance Sportive de Tunis 12.75M na Club Africain 11. 8M zote kutoka Tunisia.

Ya nne Kaizer Chiefs ya kutoka nchini Afrika Kusini ambayo yenyewe inatajiri karibu Paund milioni 10.48.

Klabu tajiri zaidi Barani Afrika View attachment 712984

Wale wachovu wa kimataifa mbona hatuwaoni? Basi hapo utawasikia oh hatujapigwa vidole na Mze Akilimali ndiyo maana hatupo hapo.
 
Hawa ndio waongo kabisa labda bongo hawaijui vizuri. Hakuna timu yoyote bongo ambayo ina akiba benki angalau milioni 10 tofauti na AZAM ambayo ni kampuni ya mfanyabiashara
Mkuu japo mimi shabiki wa Yanga lakini utajiri sio lazima cash tu.
Unakokotoa na assets, brand, n.k.
 
Mkuu japo mimi shabiki wa Yanga lakini utajiri sio lazima cash tu.
Unakokotoa na assets, brand, n.k.
Wewe jamaa unajielewa balaa..yamkini atakuwa amekuelewa vilivyo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom