Tundu Lissu
Member
- Nov 29, 2010
- 10
- 405
Naomba Kama yupo mwenye nakala ya presentation ya Profesa atuwekee humu tafadhali. Ni vigumu kujadili hoja zake on the basis of newspaper reports.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba Kama yupo mwenye nakala ya presentation ya Profesa atuwekee humu tafadhali. Ni vigumu kujadili hoja zake on the basis of newspaper reports.
Kukaa chini na kuanza kuelezea aina ya muungano ni kutaka kutouchimba mzizi wa tatizo halisia.
Kama anavyobainisha Prof. Shivji na kusema kuwa na serikali tatu ni chanzo cha kuvunjika kwa muungano. Kama matokeo yake ndiyo hayo, kuna kuwa na umuhimu gani wa kuingia gharama ya kuwa na serikali tatu wakati tunafahamu matokeo yake ni kaput.
Mzizi wa tatizo ni sauti ya wananchi kupitia kura ya MAONI (referendum) kujua kwanza kama watataka waendelee na muungano au waachane nao.
Kama wengi wataafiki kuwepo na muungano basi waseme wao wenyewe ni muungano gani wanataka uwepo ili kupata political Legitimacy and political justification kwa wanasiasa wetu kwa kile watakachokifanya baada ya kura ya maoni.
Ninachokiona hapa ni kuchelewesha muda wakati kinachokuja baadaye kinafahamika siyo kwa magwiji wa political science tu bali hata kwa watu wa kwenye vijiwe vya kahawa.
We just need REFERENDUM. Finito.
huyu jamaa ni walewale wa UDSM "matarumbeta ya kukodi"...watakuja kwa fujo na maelezo mengi yakipigiwa upatu ili waje iokoa CCM, na maslahi ya wazenj.
huyu jamaa ni walewale wa UDSM "matarumbeta ya kukodi"...watakuja kwa fujo na maelezo mengi yakipigiwa upatu ili waje iokoa CCM, na maslahi ya wazenj.
we need, wewe na nani? Jiongelee mwenyewe usitake kuwawekea Watz wote maneno Midomoni!
Huyu Nae ni mnafiki na hajulikani msimamo wake Yupo kupotosha watu mara hivi mara vile Yuko kutumikia Mabwana wawili
Mkuu, ninaona hoja yako unatengeneza kwa fikra tu ambazo hazibebwi na ukweli halisia.
Hii research ya Watanzania kuwa chini ya 30% wanaofahamu kusoma na kuandika sijui umeitoa wapi wakati research za kimataifa kama UNICEF na UNESCO zinagonga kwenye 70% na huwezi kuniambia kuwa nusu ya hawa hawajui kama kuna muungano wa nchi za Tanganyika na Zanzibar.
Mimi nafikiri watanzania tumefikia katika level ya kujiamulia mambo yetu na mstakabali wa taifa kisiasa kama wananchi wote na ndiyo maana hata CCM wameliona hili na wakaamua kutoa maoni katika tume ya katiba kama wanaona ni lazima kuwepo na mgombea binafsi.
Japo huwa sikubaliani nae katika hili...lakini nachelea kukuambia humjui Shivji....huu ni msimamo wake na maoni yake tangu awali akihimiza uundwaji wa katiba mpya.
Ahsante mkuu, nakumbuka kabla ya ume ya Wariona Shivji (ambaye namuheshimu sana) alipita sehemu zote za znz katika elimu ya umma. Huko (video zipo) alisema kuwa muungano haukuwa na ridhaa ya wananchi.Zanzibar walipoweka mipaka na kujiomgezea mamaka kupitia katiba yao mpya hakulalamika zaidi kuwatetea kuwa wana haki kama taifa. Sasa hv anaposikia ujio wa serikali ya tatu anaanza kupatwa na hofu ya serikali hizo kuwekeana mipaka, kuna hatarisha muungano.
Wengi hawauhitaji huo muungano, na serikali tatu ni mbinu tu ya kuuvunja huo muungano na hapo ndipo ilipo hofu ya shivji....hana hoja hoja tena bali ni mapenzi yake kwa muungano, asije kushangaa suala hili kumpunguzia credibilities zake.
Mkuu sijakuelewa kabisa unaposema wananchi hawana uelewa kuhusu civics wakati huo huo ni wananchi hao hao wanaopiga kura kuwachagua viongozi kuanzia ngazi ya mtaa mpaka taifa. Sikatai kama kuna baadhi ya wananchi hawafahamu mfumo wa uongozi uliopo Tanzania lakini hiyo haizuii wale waliowengi na wanafahamu mifumo ya uongozi kupewa SAY kuhusu mwelekeo wa nchi yao.Achana na mambo ya takwimu sijui za UN..... nenda kijiji chochote TZ, ongea na watu halafu waulize kuhusu TZ, kuna waTZ tena wengi tu hawajui Tanzania inatokana na nini, kuna watu hata hawajui kama wanaishi ya Tanzania ingawaje wapo TZ, nenda Umasaini huko kamuulize Mmasai kuhusu Tanzania, au Kondoa Irangi huko au Shinyanga vijijini, Karatu, Dodoma huko, n.k!
Haya ni mambo ambayo nimejionea mwenyewe baada ya kusafiri sana ndani ya TZ (vijijini) kutoḱana na kazi yangu na kuongea na watu wengi, sehemu ambayo watu wana uelewa ni Mkoa wa KLM hapo sawa kuna watu wengi hata vijijini wanaelewa kidogo kuhusu TZ kwa sababu ya Elimu na Dar, sehemu zilizobaki huko vijijini wanajua kuhusu Mwenyekiti wao wao wa kijiji, CCM na Nyerere basi, kuna watu wengi tu wanaishi kijijini na hajawahi kufika Wilayani kwake, Sengerema huko, leo ukamwambie sijui kuhusu kura ya maoni kuhusu Muungano wa Bara na Visiwani, hawezi kukuelewa!
Usinielewe vibaya sisemi kwamba haliwezekani lkn inabidi ufanye kazi sana kuwaelimisha watu kabla ya hiyo kura ya maoni, maana hasa ya Tanzania na Muungano, baada ya hapo labda ndio wapige hiyo kura, lkn sasa hiyo gharama, si no bora uwajengee Shule wajifunze kusoma kuandika na kuhesabu au uwapelekee huduma ya Afya?
Tusiige kila kitu bila kuangalia mazingira yetu, jaribu tu kutoka na kwenda vijijini TZ ongea na watu waulize maswali wadadisi ndio utaelewa ninachokiongelea!