Prof Sivji hotuba yaake ya kuaga kuwa mwenyekiti wa kigoda cha mwalimu ilikuwa inaonyeshwa live katika ITV na mimi nilibahatika kumsikliza katika sehemu ya mwisho wa hotuba yake.
Yeye anasema kuwa swala la muhimu sio kujadili idadi ya serikali bali maslahi ya taifa. Mapendekezo yake katika mfumo wa muungano ambayo amesema alishawahi kuyawakilisha kwa serikali ya Zanzibar ni kuwa na dola mbili kamili na kuwa na mabunge matatu, moja la tanganyika,moja la zanziba na moja la muungano. Pia anapendekeza mambo ya muungano ya angaliwe kwa level tatu za umuhimu, kuwe na mambo ya muungano, kuwe na mambo yasiyo ya muungano lakini yanaangaliwa kwa karibu sana na serikali au bunge la muungano na yawepo mambo ya common interest kwa wote.
Kwa mtu yeyote aliye ifuatilia hotuba hiyo naomba aongezee.
ITV, au Kigoda cha Mwalimu wakiiweka ile hotuba you tube watatusaidia sana,kwani ilikuwa ni hotuba ya kufungua macho kuhusu suala la rasimu ya katiba