Shobo zangu zimenitia aibu, kuna wadada wana maringo sana

Shobo zangu zimenitia aibu, kuna wadada wana maringo sana

Nimefika kwenye kimgahawa kimoja, nikaenda kwenye matunda nikakuta mdada ameshika sahani ya chakula.

Chakula kilikua kiugali kidogo kama vitonge vitatu, na vinyama huku akisusubiri matunda.

Kwa shobo zangu nikamwambia “ugali huo utashiba?” Nikamuuliza kama mara tatu lakini akafanya kama hasikii
Mara ya nne ni kama nikamgusa kidgo mana nikahisi labda ni kiziwi, lakini hakutaka hata kushtuka.

Ilionesha clearly kua ameamua kunilia buyu, kisha akaondoka zake, nimefandhaika na kujiona mjinga sana.

Muuza matunda kwakua ananiheshimu, kafanya kama hajaona kilichotokea.

Anyway leo nimejofunza ku balance shobo hasa kwa watu niliowajua.

Pengine alidhani namtaka kimapenzi au natafuta ukaribu nimtongoze, kumbe sina hata nia hiyo🙌🙌
Mtu humjuwi mwanzo wala mwisho unaenda kumuingilia namna yake ya kula.

Ujinga huo.
 
Umenikumbasha mbali Sana...wakati tunasoma nikiwa kidato Cha nne,nakumbuka Kuna Binti alikuwa msomali..yule manzi alikuwa ni pisi haswa..sasa sikujua ilikuwaje siku Ile ...tulikuwa tumetoka likizo Sasa Ile wanafunzi tumekutana shule zishafunguliwa...bhasi Ile tumeonana tu alikuja spidi kunikumbatia Hadi nilipatwa na mshangao Yani mapigo ya moyo yalienda kasi Sana .[emoji3]nilikosa nguvu ya kumkumbatia kwakweli na ilikuwa suprise ya hatri mbele za washkaji kibao
Sasa wewe mbona hapa ndo umeshobokewa, aibu iko wapi?
 
Kwanzia leo jifunze nidhamu hizi chache za kuongea ili uwe gentlemen

1. Ongea pale tu inapohitajika uongee, epuka kuongea sana ili ukiongea watu wazingatie unaongea nini
2. Salimia kwa sauti inayosikikia na usipojibiwa kaa kimya usilazimishe salam endelea na shughuli zako.
3.Mtu akikufata kukusimia kwa kukupa mkono usimpe mkono ukiwa umekaa chini simama kwanza shakehand ukiwa umesimama.
4. Ukiongea na mtu hakikisha unamuangalia machoni haijalishi yeye ni nani.
5. Ukiulizwa swali usikimbilie kuropoka kujibu hata kama unajua anachouliza tulia sekunde 3 ndo ujibu.
hapo kwenye kuangalia machoni huwa naghairi sometimes maan hili lisura lang lilivo baya mtu anaweza zimia kabisa...nataka nishindanie mashindano ya sura mbaya kama yapo nishtuen
 
Mademu wapumbavu sana. Nilipotea njia siku moja nikakutana na demu, nikawa nakazana kumsimamisha ili anielekeze njia, nikawa namwita kweli lakini kanilia buyu tu. Kumbe kwa akili zake ndogo alijua nataka kumtongoza, majinga kweli haya.
Usiite mtu mpumbavu bila kujua alikua anapitia maswaibu gani hata asikusikilize. Kama utaona mtu haelekei kukusikiliza ni vema umuache hutapungukiwa chochote mana si lazima akusikilize.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta creed Aventura

Ambition.

Hivi vitu ukinukia vizuri halafu ukiongeza na shobo

Zinakuwa shobo dundo. [emoji2]Mbona watakuitikia na goti kabisa.

Tatizo unapulizia deodorant za buku 6 zinanukia kama dawa za mbu
 
Wapi wewe ulikua unamtaka, kwani yeye kula ugali mdogo inakuhusu nini
Kua na shobo haimaanishi mtu unamtaka, she wasn’t even that beautiful, she couldn’t make it in my dating pool at all.
Mlugaluga wewe
 
Tafuta creed Aventura

Ambition.

Hivi vitu ukinukia vizuri halafu ukiongeza na shobo

Zinakuwa shobo dundo. [emoji2]Mbona watakuitikia na goti kabisa.

Tatizo unapulizia deodorant za buku 6 zinanukia kama dawa za mbu
Hiyo ni kwa wanaonuka jasho
 
Sikumbuki vzr ila alikwenda kwenye Kongamano la dunia ambalo Mgeni rasmi alikuwa ni Bill Gate. Wakiwa bado wako nje ya Ukumbi Bill Gate alipita akiwa kavaa Jeans na shati (casual) akamsalimia ila Madam Ritta alimtazama tu kwa dharau na hakupokea salamu ya bilionea huyo.
Nadhani Madam Ritta mwenyewe ali-tweet huku akijutia kutopokea salamu ya Bilionea huyo eti akijitetea ya kuwa hakumtambua sababu alivaa casual. Kwa walio na tweet hiyo wanaweza kutuwekea hapa.
Chai
 
Hiyo ni aina nyingine ya salamu mkuu huyo mwanamke hajitambui na zaidi sana ako na majivuno kupindukia hivyo wala asikupe shida..
 
Katika mambo niliyojifunza mapema sana nikiwa bado kijana mdogo ni kuwa na mipaka na kufanya kama siwaoni hasa hawa wadada wa mjini.
Wengi wana matatizo ya akili na ukijifanya kuwa mtu mwema au social kwake yeye anakuona kama unajipendekeza hivi.
 
Back
Top Bottom