Shock: Hospitali ya Kairuki yakataa wagonjwa wa ugonjwa wa mifumo ya hewa kijanja, yaweka bei isiyowezekanika kwa Watanzania wengi

Shock: Hospitali ya Kairuki yakataa wagonjwa wa ugonjwa wa mifumo ya hewa kijanja, yaweka bei isiyowezekanika kwa Watanzania wengi

Siasa unaleta wewe Hamatan
Unazijua taratibu na sheria za kuendesha taasisi ya afya!? Unajua hawa watoa huduma wanafanya kazi katika miongozo gani?

Hi sio biashara ya kuuza nguo bali ni kutoa huduma na kunusuru uhai wa watu
Mama d banah huwa kuna wakati unaongeaga point na kuna wakati unaongea pasipo fikiria,

Kwa hili unapotoka usifananishe huduma za AFYA na BIASHARA yani nimekushangaa sana, hizi taasisi za afya kuziendesha ni kazi sana ukijifanya unaziendesha kwa kutoa msaada mbona utafunga kituo, bila ruzuku ni tabu kazi kuziendesha mfsno tu kcmc wanapewa ruzuku na kwa kuwa ni kituo cha afya chini ya kipo chini ya dini sass nenda kaulize gharama za pale utasikia, vituo vya afya kuviendesha ni shuguli kubwa kuanzia madawa, vitendea kazi tiba, na wafanyakazi ni gharama sana, ukiachilia hilo pia kuna baadhi ya magonjwa kupatiwa huduma ni ghali na pia vipimo baadhi ni balaa,
 
Mbona JPM anasema kajenga hospitali "kwa maelfu", si waende huko wakatibiwe bei karibu na bure?
Hata kama zingekuwa zimejengwa mamilioni ya hospitali, mfumo wa afya Tanzania upo regulated na serikali. Huduma ya afya si biashara huria kwamba wajipangie bei wanazotaka wao.
 
Matibabu ya bei nafuu kadai huko unakolipa kodi aka serikalini, sio watu ambako wametoa jasho na mitaji yao kuwekeza.

Pambana na serikali, ndio chombo pekee una haki ya kukidai, sio hospitali ya mtu. Wewe mwenyewe unaweza kufanya kazi kwa kulazimishwa mshahara au kuuza vitu kwa kulazimishwa bei?
Watu wanachukulia poa sana kukiendesha kituo cha afya... Madawa na vitendea kazi ni gharama sana, bado hujamlipa dactor ndiyo maana kuna baadhi ya hospitali wanachukua madaktari bingwa kama part time mgonjwa akitokea akaitaka daktari bingwa basi daktari atapigiwa simu, halafu kuna mtu unafananisha mambo ya afya na biashara, mimi naamini hata faida watakua wanaipata kidogo sana.
 
Hakuna kitu kisichoratibiwa na serikali hasa huduma za afya.
Kama ulidhani kwa kuwa ni hospitali binafsi basi inaweza kupanga bei kiholelaholela utafikiri wana nchi yao binafsi wasiyobanwa na regulatory authority yoyote basi pole sana!
Wewe unachekesha kweli yaani serikali ambayo inakusanya kodi za hao mnaowaita wanyonge haina huruma nao , taasisi binafsi ndio ije kuwaonea huruma?

Kuna kitu cha kumkomoa mlalahoi kama kitendo ilichokifanya serikali ya wanyonge kama kufanya kipimo cha COVID19, kuwa ni dola 100?!

Jana waziri anasema eti wanafanya hivyo kutokana na watengenezaji wa vifaa hivyo kuviuza bei ghari?!!mbona nchi nyingi tena za kiafrika zinafanya kipimo hiki bure?!

Wao wanakitengeneza?ndio tatizo la serikali ambayo wao kila kitu wanawaza pesa tu badala ya huduma!!halafu cha ajabu walivyowapenda sifa utasikia waziri anakuja kulitolea maelekezo kuwa hizo bei ni ghali sana!!serikali haikubali, je wao kwenye kipimo nani atawaambia??na hata hiyo chanjo wanajifanya tu kwakuwa wanaona ni mzigo mzito kuzinunua sasa wanakwepa kijanja tu.

Mimi nasema hivi, wafanye tu milioni 2!!kabisa, KENGE HADI AONE DAMU KWENYE MASIKIO!!hilo ndio limekuuma sana kuliko hili la kipimo cha 230, 000 tena cha serikali???
 
Mama d banah huwa kuna wakati unaongeaga point na kuna wakati unaongea pasipo fikiria,

Kwa hili unapotoka usifananishe huduma za AFYA na BIASHARA yani nimekushangaa sana, hizi taasisi za afya kuziendesha ni kazi sana ukijifanya unaziendesha kwa kutoa msaada mbona utafunga kituo, bila ruzuku ni tabu kazi kuziendesha mfsno tu kcmc wanapewa ruzuku na kwa kuwa ni kituo cha afya chini ya kipo chini ya dini sass nenda kaulize gharama za pale utasikia, vituo vya afya kuviendesha ni shuguli kubwa kuanzia madawa, vitendea kazi tiba, na wafanyakazi ni gharama sana, ukiachilia hilo pia kuna baadhi ya magonjwa kupatiwa huduma ni ghali na pia vipimo baadhi ni balaa,
Mkuu hakuna popote penye kutoa huduma huduma za afya kuna miongozo yake inayozingatia uhai wa wateja wake. Ndio maana sheria za biashara ya kuuza nguo haiwezi kuwa sawa na kwenye huduma ya afya
 
Watu wanachukulia poa sana kukiendesha kituo cha afya... Madawa na vitendea kazi ni gharama sana, bado hujamlipa dactor ndiyo maana kuna baadhi ya hospitali wanachukua madaktari bingwa kama part time mgonjwa akitokea akaitaka daktari bingwa basi daktari atapigiwa simu, halafu kuna mtu unafananisha mambo ya afya na biashara, mimi naamini hata faida watakua wanaipata kidogo sana.
Wengi wanaobwabwaja hawajawahi hata kufungua genge wakaweka mfanyakazi ambae kila mwezi anataka mshahara.
 
Ila kwa serikali sikivu, kumtonza mtu dola 100, kwa kipimo cha COVID19, ndio biashara huria??
Hiyo $100 ni tozo ya matibabu? Usichanganye vitu hapa. $100 ni tozo ya vipimo kwa mtu anayehitaji kusafiri kwenda sehemu ambayo wanahitaji certificate ya COVID 19, ni kama ilivyo kwa homa ya manjano. Suala la Kairuki ni tozo ya matibabu, tozo kwa mtu anayeumwa anayehitaji huduma ili apone.
 
Imenifanya nikumbuke wimbo wa christian bella, mimi masikini niende wap eeh
 
Katika hali inayoonekana ni muendelezo wa maisha magumu kwa wananchi.

Hospitali ya Kairuki nchini imekuja na utaratibu wa kushangaza wa kutoza malaki ya hela kwa siku kwa mtu atakayeenda katika hospitali hiyo kutibiwa ugonjwa wa mifumo ya hewa.

Katika utaratibu huo mgonjwa yeyote atakayekwenda kupata huduma ya ugonjwa wa mfumo wa hewa, Hospitali hiyo itamtoza shilingi Laki sita kwa siku (600000)kama hatahitaji huduma ya Ventilator. Na kama atahitaji huduma ya ventilator basi atalazimika kulipa shilingi Laki nane na nusu (850000).

Nilipokuwa naongea na wananchi kuhusiana na suala hili, wengi wameonyesha kuwa na wasiwasi kuwa hospitali hiyo inataka kuwakimbiza wananchi wenye matatizo hayo wasiende kwenye hospitali hiyo. Na kwa kuwa ni kinyume cha maadili ya kidaktari kukataa kuhudumia mgonjwa basi hospitali hiyo inataka kukwepa kuhudumia wananchi katika maradhi hayo kijanja.

Kwa kweli hili jambo ni la kusikitisha na la kutia aibu kwa wamiliki na waendesha hospitali hiyo.

Kwanza kuna maswali ya kujiuliza, kwa nini hatua hii ya ajabu ije kwenye kipindi hiki cha Korona?.

Je ni kweli kuwa kwa utaratibu huu hospitali hiyo inafukuza wananchi wanaohitaji huduma hiyo kijanja kwa kisingizio cha pesa?

Na kama hailengi kukwepa wajibu wa kuhudumia wagonjwa, je wamiliki wa hiyo hispitali wameamua kyigeuza Korona kuwa dili, yaani kuvuna mamilioni ya pesa kupitia wananchi wanaohitaji huduma ya hospitali?

Je kuna baraka za serikali katika hatua hii, ili kulazimisha wananchi wafanye tiba mbadala majumbani ili takwimu halisi za wenye ugonhwa wa Korona zisipatikane?

Tunaitaka serikali kupitia Waziri wa Afya aingilie kati suala hili.
Tunajua serikali inayo mamlaka ya kuingilia kati utendaji wa hospitali zote nchini katika mfumo wao wa utoaji huduma nchini.

Tunamtaka Waziri wa Afya aje public atueleze kama anaunga mkono kitendo kama hiki cha hospitali ya Kairuki ili hiki walichokifanya kisije kikageuka kuwa mfano wa hospitali nyingine.

Ubaya wa kitendo cha hospitali ya Kairuki, hawshaspecify hata uhonjwa husika, wametumia magonjwa ya mfumo wa hewa!. Kwa hiyo watoto wetu wachanga wakipata nimonia ya kawaida kabisa isiyokuwa hata hiyo Korona ndo mnataka kuwatoza Laki nane na nusu kwa siku? - Hii hospitaki inataka tupoteze hata watoto wetu kwa sababu ya watu wenye mawazo. mfu wachache!

Tunataka hii hospitali ibadirishe huu utaratibu maramoja!. Mwanzilishi wa hii hospitali hayati profesa Kairuki atakuwa anajigeuza kaburini sasa kwa baadhi ya cowards wachache kutaka kuwatosa wananchi katika kipindi hiki kigumu cha kiafya duniani!

Hili halikubaliki:
Angalia fomu hii hapa chini kutoka hospitali hiyo.


View attachment 1692378

Kwakuwa tulishaushinda huu ugonjwa kama tunavyoambiwa na viongozi wetu, hawa jamaa wanaona ni usumbufu ndio maana wanaweka hizi bei ili wasipate usumbufu. Tuendelee kupiga nyungu kama tunavyoelekezwa na Mawaziri wetu na Wizara.
 
Hivi kwanini Mama yangu Gwajima asizichukulie hatua kali hizi hospitally ikiwemo kuzipiga fine kwa kukiuka Taratibu za kiafya za kubagua wagonjwa kama ni kweli wamewabagua lkn ?
 
Pale unapopandisha bei mara nyingi katika kipindi fulani cha ugonjwa wa mlipuko ni dhahiri kuna question mark. Kwa nini hizi bei hazikushoot kiasi hiki miezi kadhaa nyuma wakati tatizo la korona halikuwa kubwa nchini?
Nenda Mwananyamala au Amana jombaa...
 
Hiyo $100 ni tozo ya matibabu? Usichanganye vitu hapa. $100 ni tozo ya vipimo kwa mtu anayehitaji kusafiri kwe

nda sehemu ambayo wanahitaji certificate ya COVID 19, ni kama ilivyo kwa homa ya manjano. Suala la Kairuki ni tozo ya matibabu, tozo kwa mtu anayeumwa anayehitaji huduma i

Hiyo $100 ni tozo ya matibabu? Usichanganye vitu hapa. $100 ni tozo ya vipimo kwa mtu anayehitaji kusafiri kwenda sehemu ambayo wanahitaji certificate ya COVID 19, ni kama ilivyo kwa homa ya manjano. Suala la Kairuki ni tozo ya matibabu, tozo kwa mtu anayeumwa anayehitaji huduma ili apone.
Sio matibabu ni kipimo, utakuwa hujui unachosema, ndio maana kuna baadhi ya hospital binafsi kama aghakani wamepewa kazi hiyo, uwe unataka kusafiri , au unajisikia vibaya kupata kipimo hicho ni 275, 000!!na jana waandishi wa habari walimuuliza waziri, akasema kuwa inatokana nagharama ya kununua hivyo vipimo kuwa kubwa ndio maana wanasisitiza kujenga viwanda vya kwetu?!!!hahaaa!!weee kuwa hoi nenda hospital , pimwa corona , bill itakuja na ya kipimo hicho!!nchi nyingine wanatoa bure!!
 
Hatuwatetei Agha Khan au hospitali yoyote itakayokuja na gharama za kitalii kwa magonjwa ambayo wananchi wengi wanahitaji huduma!

Tunaiamsha serikali na mamlaka zinazohusika na tiba za wananchi zitupie jicho bei hizi utadhani tuko ulaya!

Kairuki wanatushangaza zaidi maana bei zao zimeshoot zaidi kipindi hiki cha korona kuliko ilivyokuwa awali, Je wanakusudia nini kuzipandisha hizo bei kipindi hiki?
Serikali ipi unaiamsha wakati wamesema hakuna Corona? Wao wamesisitiza tupige kikombe [emoji116]
Screenshot_20210202-123056.jpg
 
Back
Top Bottom