Shock: Hospitali ya Kairuki yakataa wagonjwa wa ugonjwa wa mifumo ya hewa kijanja, yaweka bei isiyowezekanika kwa Watanzania wengi

Shock: Hospitali ya Kairuki yakataa wagonjwa wa ugonjwa wa mifumo ya hewa kijanja, yaweka bei isiyowezekanika kwa Watanzania wengi

Hivi hospital ya Saint Thomas gharama zake za kujifungua ni kiasi gani wakuu..?
 
Missile naona umepata vidonge vyako kwenye huu uzi wako
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ni watu wenye hasira na serikali yao sasa wanadhani kuunga mkono bei komoa za taasisi binafsi za afya ni kuikomoa serikali kumbe ni kwa hasara yao.

covid ikigonga majumbani mwao familia ya watu watano ikapata msala ni wao na si serikali. Wanadhani nyungu zitawaokoa, Covid ikishaingia kwenye mapafu, oxygen ikashuka halafu kila mtu ndani ya family anatakiwa alipe laki nane na nusu per day ndo aweze kunusuru maisha yake ndo watakumbuka tunachokipigania hapa kwenye huu uzi.

Kuvurunda kwa serikali kwenye mambo mengi kumekatisha watu tamaa kiasi kwamba hawana tena ari ya kuhoji kuvurunda zaidi.

Ninapoisema Kairuki hospital siyo kwamba naunga mkono hospitali nyingine zenye bei kama zao la hasha, bali hii ndo tumeikamata ready handed na itumike kama awakening call kwa serikali na taasisi binafsi za tiba kuwa gharama zao kwenye matibabu haya ya "mfumo wa hewa" yako juu sana, wayapunguze.

Watu wengi wasichokiona katika uzi huu ni kuwa, hii move ya kupandisha bei ni teknic tu ya kuwazuia wagonjwa wa korona wasiende mahospitalini, ikiwa sababu mojawapo ni kuficha kiwango cha korona nchini, maana wakitibiwa hospitali kuna data zitakuwa accumulated. Wanasiasa hawataki hilo.

Lakini kitu kingine kitakachotokea ni kuwa watakaoumia ni akina kabwela, maana hao hawatakuwa na chance ya kupata medical attention pindi wakipata korona, wataishia kunywa tangawizi na limao, na kama kitu kikipanda kwenye mapafu na kuanza kutafuna mapafu basi hawana msaada wa oxygen.

So, ukisoma comments za watu badala ya kuishinikiza serikali yao ifanye something ikiwemo let say kuzipa incentives fulanifulani hospitali hizo kwenye kodi, umeme au maji au chochote kile kinachowezekanika ili angalau zishushe hizo gharama wananchi waweze kuzimudu, wao wameona kuwa labda kuikomoa serikali ni kuwaunga mkono hao wanaowasomesha namba wananchi ili iwe vindication kwa serikali kuwa "mmeona, mmeona, kama serikali yetu inabehave vile basi ngoja na hawa wabehave hivyihivyo tu" (rejea mfano wa hoja inayojirudia ya kupima korona kwa dola 100). But at the end of the day tunaumia siye kina Kabwela na si serikali!

Na hii itoshe kukuonyesha kuwa katika nchi hii hali imeshabadilika, hii jamii imeshakua "man eat man society" kwamba wewe usiye na hela nobody gives a damn about you. Watu wanamtetea mwenye nacho kwamba hicho alichonacho kinampa haki zaidi ya kupata alichonacho hata kama ni kwa kumkamua asiyenacho mpaka adondoke afe. Sasa unfortunately mwenye nacho anataka kukimbia wajibu kutoa huduma aliyosajiliwa kwayo (naamini kwa sababu za kisiasa) lakini pia at the same time kaona opportunity ya kuwa nacho kingi zaidi kupitia afya za watu na unfortunately humu ndani ya JF watu wanaona sawa kwa sababu "kama huna hela wewe kufa tu". They don't see a big picture, wao wanaona ni business issue kumbe kuna beyond that, kuna political move ya kuficha crime ya mishandling ya Covid nchini!

Inabidi uwe na critical mind kuweza kuliona hili
 
Katika hali inayoonekana ni muendelezo wa maisha magumu kwa wananchi.

Hospitali ya Kairuki nchini imekuja na utaratibu wa kushangaza wa kutoza malaki ya hela kwa siku kwa mtu atakayeenda katika hospitali hiyo kutibiwa ugonjwa wa mifumo ya hewa.

Katika utaratibu huo mgonjwa yeyote atakayekwenda kupata huduma ya ugonjwa wa mfumo wa hewa, Hospitali hiyo itamtoza shilingi Laki sita kwa siku (600000)kama hatahitaji huduma ya Ventilator. Na kama atahitaji huduma ya ventilator basi atalazimika kulipa shilingi Laki nane na nusu (850000).

Nilipokuwa naongea na wananchi kuhusiana na suala hili, wengi wameonyesha kuwa na wasiwasi kuwa hospitali hiyo inataka kuwakimbiza wananchi wenye matatizo hayo wasiende kwenye hospitali hiyo. Na kwa kuwa ni kinyume cha maadili ya kidaktari kukataa kuhudumia mgonjwa basi hospitali hiyo inataka kukwepa kuhudumia wananchi katika maradhi hayo kijanja.

Kwa kweli hili jambo ni la kusikitisha na la kutia aibu kwa wamiliki na waendesha hospitali hiyo.

Kwanza kuna maswali ya kujiuliza, kwa nini hatua hii ya ajabu ije kwenye kipindi hiki cha Korona?.

Je, ni kweli kuwa kwa utaratibu huu hospitali hiyo inafukuza wananchi wanaohitaji huduma hiyo kijanja kwa kisingizio cha pesa?

Na kama hailengi kukwepa wajibu wa kuhudumia wagonjwa, je wamiliki wa hiyo hispitali wameamua kyigeuza Korona kuwa dili, yaani kuvuna mamilioni ya pesa kupitia wananchi wanaohitaji huduma ya hospitali?

Je, kuna baraka za serikali katika hatua hii, ili kulazimisha wananchi wafanye tiba mbadala majumbani ili takwimu halisi za wenye ugonhwa wa Korona zisipatikane?

Tunaitaka serikali kupitia Waziri wa Afya aingilie kati suala hili.
Tunajua serikali inayo mamlaka ya kuingilia kati utendaji wa hospitali zote nchini katika mfumo wao wa utoaji huduma nchini.

Tunamtaka Waziri wa Afya aje public atueleze kama anaunga mkono kitendo kama hiki cha hospitali ya Kairuki ili hiki walichokifanya kisije kikageuka kuwa mfano wa hospitali nyingine.

Ubaya wa kitendo cha hospitali ya Kairuki, hawshaspecify hata uhonjwa husika, wametumia magonjwa ya mfumo wa hewa!. Kwa hiyo watoto wetu wachanga wakipata nimonia ya kawaida kabisa isiyokuwa hata hiyo Korona ndo mnataka kuwatoza Laki nane na nusu kwa siku? - Hii hospitaki inataka tupoteze hata watoto wetu kwa sababu ya watu wenye mawazo. mfu wachache!

Tunataka hii hospitali ibadirishe huu utaratibu maramoja!. Mwanzilishi wa hii hospitali hayati profesa Kairuki atakuwa anajigeuza kaburini sasa kwa baadhi ya cowards wachache kutaka kuwatosa wananchi katika kipindi hiki kigumu cha kiafya duniani!

Hili halikubaliki:
Angalia fomu hii hapa chini kutoka hospitali hiyo.


View attachment 1692378
Wewe huna maana kabisa! Unajua uendeshaji wa Private institutions kuwa ni wa ghali sana? Nani afidie gharama hizo? Hii siyo hospitali ya dini kuwa mtaji wake ulichangiwa na waumini bwashee
 
Siasa unaleta wewe Hamatan
Unazijua taratibu na sheria za kuendesha taasisi ya afya!? Unajua hawa watoa huduma wanafanya kazi katika miongozo gani?

Hi sio biashara ya kuuza nguo bali ni kutoa huduma na kunusuru uhai wa watu
Mishahara wanalipaje?
 
Na vipi kuhusu Agha Khan Hospital inayowatoza wagonjwa wa aina hio 4,000,000 kwa siku?
 
Waganga wa kienyeji na wapiga ramli wamesema hakuna korona sasa ngoja nije niwasikie wanatoa maagizo gharama za matibabu zishuke ilihalinwalitangaza hakuna korona ila walisema kuna korona ya ajabu ajabu
 
Naona wametoka mafichoni wameukana waraka wao wenyewe.

IMG-20210203-WA0048.jpg
 
Kunapotokea pandemic yoyote ya kiafya, jukumu la tiba huwa ni la serikali...

Sasa kama serikali yetu inakana uwepo wa hayo magonjwa, unadhani hospitali binafsi zitakubali kirahisi?

Watu wenye matatizo ya upumuaji wakijazana hapo, itapelekea raia wenye magonjwa mengine ya kawaida kuikimbia hiyo hospitali...
 
Pale unapopandisha bei mara nyingi katika kipindi fulani cha ugonjwa wa mlipuko ni dhahiri kuna question mark. Kwa nini hizi bei hazikushoot kiasi hiki miezi kadhaa nyuma wakati tatizo la korona halikuwa kubwa nchini?
Hivi kuna tangazo lolote la serikali linalo onesha Tanzania corona imerudi?
 
nadhani tatizo ni hiyo form, lkn private hospital karibia nyingi gharama lazima zifike huko. mimi kuna watu nimewatembelea unakuta baadhi ya sindano hazipo hata kwenye bima ya afya inabidi wajilipie wenyewe. sasa kwa anaetumia cash ndio balaa kabisa.

nishauri serikali pamoja na kuwa hitambui hili tatizo waboreshe huduma kwenye hospitali zambazo zinaendeshwa kwa kodi zetu maana watu wanakosa huduma wanakimbilia private.

pia niwakumbushe watanzania kuwa na bima maana hujui nileo au kesho janga hili litakupata.
 
Back
Top Bottom