Short Notice ya Malawi yaleta hasara kubwa kwa wafanyabiashara Tanzania

Short Notice ya Malawi yaleta hasara kubwa kwa wafanyabiashara Tanzania

Mfanyabiashara ameshatoa mzigo shambani ama yuko mpakani au yuko njiani kisha anakutana na notice ya kutoingia Malawi

Kwanini wasitoe notice hata ya wiki mbili au mwezi mmoja?

Waziri wetu Hussein Bashe ametoa notice ya wiki moja kwa wafanyabiashara wa Malawi na Africa Kusini kuwa hawataruhusiwa kuingiza mazao yao wala kutumia ardhi ya Tanzania kuvusha mazao yao kwenda nchi nyengine

Ifike mahali watu wawe waugwana, Malawi walipata majanga ya njaa huwa tunawasaidia sana mahindi nk.

View attachment 3310922
Hivi mnafanyaje biashara bila kuwa na mawasiliano upande wa pili, kwahiyo mkiingia Malawi hizo bidhaa zenu mnapanga mfungu kandi ya barabara na kuanza kuuza! Mnakuwa na simu kali lakini hamzitumii kibiashara!
 
Bashe eti anatoa Ultimatum kwa South Africa?
SA ndio wapuuzi namba moja walipewa ban na Botswana wamefunguliwa mwaka Jana wao ni wasumbufu sana kwa bidhaa kutoka Tanzania wakati wao wanaleta hadi vitunguu Tanzania na kupeleka Kenya.
 
Africa bwana shida sana.

Huyo ni kijana kajiajiri kakutana na hizi mambo, kesho na keshokutwa vijana wote wanaamua kuwa machawa jaz band.
 
Back
Top Bottom