Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,649
- 4,786
Mzirai toka maximo aingie hoja ni hiyo tu kumpinga basi
Dawa ni kuto kwenda uwanjani...
Na kila atakapoonekana tunamzomea.
tukifanikisha hayo mwenyewe atakung'uta ****** yake na kurudi brazil kwao akaendelee kuchoma chapati.
Tunataka NIDHAMU
Asiyekuwa na Nidhamu hatumtaki Taifa Stars! (period)
hapa hata mimi napingana na wewe...mimi nimeanza kumpinga maximo toka anashuka airport kwa kigezo cha "NINI MAFANIKIO YAKE HUKO ALIKOTOKA???"..Mziray anaonekana kumpinga maximo kwa sababu kuu 2- ni kocha wa kizawa na ana haki ya kuhoji maslahi ya taifa na 2- anayo access ya media..ana makala katika gazeti la michezo nchini..ni mdau wa soka
KWANINI MAXIMO ANAPINGWA.....mafanikio ya kocha yanapimwa kwa vitu vikuu viwili..1-makombe na ubingwa timu yake ilochikua, au fainali ambazo timu anayofundisha imefikia....sijawahi kuona kocha duniani anasifiwa kwa 1- Timu ina nidhamu, 2- timu inacheza mpira mzuri lakini inafungwa kila mechi....
UTETEZI WA MAXIMO...anasema anahitaji muda wa kuandaa timu toka kwa vijana then ndio apate timu kali...aseme ni miaka mingapi anahitaji? maana sahivi tayari ameshakula miaka mi4...na pia anajua sehemu gani duniani timu ilianzishwa ikiwa na makinda tupu ... wachezaji wazuri hawaitwi kisa nidhamu...je Paul Gascoine Gaza wa uingereza alikuwa na nidhamu???...mbona alikuwa ndio tegemeo la timu ya taifa....romario wa brazil alikuwa na nidhamu?..ronaldinho gaucho anayo nidhamu???...maximo na watetezi wake hapa hawana hoja ya msingi....TIMU YAKO IKIFUNGWA NDO ULIE??? kipa lazima uwe mrefu???...ni kweli kaseja ndio kipa mfupi kuliko wote duniani...mbona kuna makipa warefu sana duniani kina dida wa brazili lakini vimeo hata kaseja mzuri...
HITIMISHO...maximo upeo wake wa kufundisha soka ni mdogo na umefikia ukomo..tunahitaji kocha mpya na sio lazma awe mziray...mziray aendelee kuwakosoa kila wanapokosea na asinyamazishwe kirahisi hivyo.
Kabla Maximo timu ilikuwa wapi???na yangapi kidunia??Si Maximo ndo at least kaipandiasha timu, kwani Mziray alikuwa wapi????Au sio Tanzania, timu ilikuwa KICHWA CHA MWENDAWAZIMU???Kweli masikini akipata ****** hulia mbwataaa na kusahau alikotoka......Tambarareeeeeeeeeee.Umenenaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. Huyu makisimo siju mashimo anatufanya wapumbavu, mara aseme eti Kaseja mfupi lakini baada ya Kaseja kuprove kuwa ufipi si hoja akaja na kuwa eti hana nidhamu. Sasa Mapunda akifungwa magoli ya kizembe Kaseja hatakiwi kutoa maoni> Wadu tuisusie timu ya taifa waende tu uwanjani wanao mteteta
Kabla Maximo timu ilikuwa wapi???na yangapi kidunia??Si Maximo ndo at least kaipandiasha timu, kwani Mziray alikuwa wapi????Au sio Tanzania, timu ilikuwa KICHWA CHA MWENDAWAZIMU???Kweli masikini akipata ****** hulia mbwataaa na kusahau alikotoka......Tambarareeeeeeeeeee.
acheni ukurumbizi huwo, kwanini msilaumu uwezo mdogo wa wachezaji wenu ambao hawafundishiki, vifuu tundu, hawafahamu. Kwanini mnakuwa watovu wa shukurani, ni wakati wa maximo angalau tanzania imeona 'profeshino' wawili wa tatu. Na halafu, si maximo mwenyewe alipomaliza mkataba wake alitaka kuondoka kwanini muanze kupiga mbiu kama vile yeye anang'ang'ania, kwa lipi? Si tff wenyewe waliomlazimisha abakie...mbona mnakuwa watovu wa hisani jamani!!!!!!!!!
kaka umesahau kusema kitu kimoja, mpira sio kocha tu, mpira ni program nzima ya nchi. Mambo tunayobidi tujiulize je ligi zetu zinakidhi mpira wa kisasa?, kuanzia ligi kuu mpaka ligi za chini tukichukulia mfano wa nchi zilizo endelea kisoka.Acheni ukurumbizi huwo, kwanini msilaumu uwezo mdogo wa wachezaji wenu ambao hawafundishiki, vifuu tundu, hawafahamu. Kwanini mnakuwa watovu wa shukurani, ni wakati wa Maximo angalau Tanzania imeona 'profeshino' wawili wa tatu. Na halafu, si Maximo mwenyewe alipomaliza mkataba wake alitaka kuondoka kwanini muanze kupiga mbiu kama vile yeye anang'ang'ania, kwa lipi? Si TFF wenyewe waliomlazimisha abakie...mbona mnakuwa watovu wa hisani jamani!!!!!!!!!
Acheni ukurumbizi huwo, kwanini msilaumu uwezo mdogo wa wachezaji wenu ambao hawafundishiki, vifuu tundu, hawafahamu. Kwanini mnakuwa watovu wa shukurani, ni wakati wa Maximo angalau Tanzania imeona 'profeshino' wawili wa tatu.