Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

Malaria sugu usipate tabu sana na Maximo, ni suala la kumuelewa tu huyu bwana, jana kazungumza vizuri sana katika harakati zake za kucheza na akili za Watanzania na kujaribu kutufanya tuwachukie wachezaji wetu. Anadai kuna baadhi ya wachezaji ambao hajawachukua ni wasaliti, sasa najaribu kujiuliza, msaliti kwa kiswahili cha kawaida ni mtu anayefanya jambo kwa makusudi ili kuzorotesha maendeleo au mafanikio ya taasisi au idara, katika context hii ni timu ya Taifa. Sasa tujiulize msaliti ni nani kati ya Maximo na hao wachezaji walioachwa. Kwangu mimi msaliti ni mtu ambaye kwa makusudi anamchagua mchezaji asiyekuwa na uwezo na kumpanga halafu timu inafungwa. Kwa upande wa pili pia TFF nao ni wasaliti vile vile, kwa kukaa kimya na kuacha hiyo tabia ya kisaliti iendelee kufanywa.
 
Huyu Bwana Mtu wa ajabu kweli.Inadaiwa kuwa hamtaki Kaseja sababu hapo nyuma alimcheka Ivo Mapunda alipofungwa goli la kijinga.Hii ilikuwa katika siku za mwanzo za ukocha wake.

Mimi nilitegemea kuwa kama Kaseja alifanya hivyo na kimpira ni makosa angemrekebisha na sio kumsusia kwa kuwa yeye ameletwa kujenga professionalism pia.Sasa ukimuacha unamsaidia nini.Chuji anadai hana nidhamu sasa mbona Vieira alikuwa analambwa redcards mpaka nne kwa msimu na bado aka-captain France?

Mtoto wako kama hataki kwenda shule na wewe ukasusa sasa unamkomoa nani?Simtetei Kaseja ila generally Maximo ana mapungufu.Mkwasa angepewa hayo mamilioni na nyumba pale Masaki tungekuwa mbali ila hii dhana kuwa Watanzania hapa usiwalipe watafanya kazi tu ndio inatuponza.
 
Eti ndugu zangu, kuna mtu anafahamu Kaseja alifanya kosa gani ambalo halisameheki?

Ukweli ni kwamba hakuna anayejua ila kuna mambo matatu yanayotajwa sana:
1. Juma Kaseja aliwashawishi wachezaji wenzake wa Simba waliokuwa timu ya Taifa kipindi hicho wadai posho kuanzia siku ya kwanza katika ile safari ya Brazil. Kwa wale wanaokumbuka ile safari ya Brazil timu ya Taifa iliondoka nusu nusu, wachezaji wa Simba walibaki kucheza michuano ya Kimataifa na wakaungana na wenzao baada ya wiki moja. Sasa kuna watu wanadai kwamba wachezaji wa Simba wakiongozwa na Juma walidai posho kuanzia day 1 kwasababu mdhamini alitoa posho kwa wachezaji wote kuanzia day 1 ingawa wao walijiunga a week later!
2. Kuna watu wanadai Juma K aligongana na Maximo kwa mwanamke ambaye wote walikuwa wanammega, huyu ni binti mtangazaji wa C10 ingawa saa hivi haonekani kwenye luninga.
3. Wapo wanaodai kwamba Juma alimcheka Ivo wakati tunapigwa four oclock na Wasenagal, na hili Maximo kaligusia jana katika press conference.
 
Huyu Maximo anacheza na akili za watu. Watanzania lazima waamke na kuangalia na kuchambua huyu Maximo amefanya nini tangu aje.
Kwanza nadhani hana mpango unao heleweka wa kuendeleza soka hapa Tanzania na matokeo yake ni kubadillisha timu kila siku.
Visingizio kuwa Tanzania haina Proffessional players siyo ya msingi.
Binafsi ningependa kumuuliza swali Maximo, kwa nini wasaidizi wake (wanaotoka Brazil) hawakai?
 
Watanzania tusiwe wepesi wa kulaumu. Huyu bwana Maximo amejitahidi kwa kiasi fulani lazima tukubali. Tunataka tumpe ukocha nani? Mziray? Jamhuri Kihwelo?
Kipigo cha 5-1 na mapharaoh wa misri hicho hakipingiki, hatukuwa na maandalizi ya kutosha, siwezi kumlaumu sana barthez peke yake, kwa ujumla timu nzima haikucheza siku hiyo na hata Kaseja angekuwepo lazima tungefungwa tu! Suala la kipa wa benchi kudata hilo kwangu siyo tatizo mbona Ben Foster wa Man Utd kadaka juzi kwenye mechi ya Brazil vs England wakati anawekwa benchi na Ben Foster.

Mimi namtetea Maximo ktk suala zima la kujenga nidhamu, huwezi kuwa na watu wanaogawa timu au bila yeye mambo hayaendi. Tujiulize kabla ya Maximo tumechukua makombe mangapi? Tusiwe watu wa kuchonga sana, tusaidiane ktk kujenga soka na pia natoa ushauri kwa akina Mziray et al sio tu lazima Kaseja au Chuji awepo ndio stars inakuwa imekamilika, kuna wachazeji mikoani wenye vipaji vizuri ndio hao tunatakiwa tuwaibue. Brazil mastaa wote huibuliwa toka timu changa siyo lazima watoke Simba au Yanga
 
Wewe Chibingo unajua Maximo analipwa nini na kuwezeshwa mangapi?Huyo Mziray aliwahi kulipwa na kuwezwshwa kama Maximo?Watanzania(makocha) walitupeleka AFCON 1980,tumeshinda Challenge Cup twice...bila mishahara mikubwa wala corporate sponsors...acha wewe
 
Watanzania tusiwe wepesi wa kulaumu. Huyu bwana Maximo amejitahidi kwa kiasi fulani lazima tukubali. Tunataka tumpe ukocha nani? Mziray? Jamhuri Kihwelo?
Kipigo cha 5-1 na mapharaoh wa misri hicho hakipingiki, hatukuwa na maandalizi ya kutosha, siwezi kumlaumu sana barthez peke yake, kwa ujumla timu nzima haikucheza siku hiyo na hata Kaseja angekuwepo lazima tungefungwa tu! Suala la kipa wa benchi kudata hilo kwangu siyo tatizo mbona Ben Foster wa Man Utd kadaka juzi kwenye mechi ya Brazil vs England wakati anawekwa benchi na Ben Foster.

Mimi namtetea Maximo ktk suala zima la kujenga nidhamu, huwezi kuwa na watu wanaogawa timu au bila yeye mambo hayaendi. Tujiulize kabla ya Maximo tumechukua makombe mangapi? Tusiwe watu wa kuchonga sana, tusaidiane ktk kujenga soka na pia natoa ushauri kwa akina Mziray et al sio tu lazima Kaseja au Chuji awepo ndio stars inakuwa imekamilika, kuna wachazeji mikoani wenye vipaji vizuri ndio hao tunatakiwa tuwaibue. Brazil mastaa wote huibuliwa toka timu changa siyo lazima watoke Simba au Yanga

Uache upumbavu..
Sisi waanzania tunataka mafanikio na si nidhamu.
Kama nidhamu ingekuwa big deal basi timu za kanisa na misikiti zingekuwa zinapokezana ubingwa tu.

Tazama nchi kama brazil wametimua makocha wangapi ktk miaka ya hv karibuni?
Je na wao wanatafuta nidhamu au mafanikio?
Tazama mabingwa wa dunia Azurri wamebalasa makocha wangapi mpk kuja kumpata kamanda Lippi na kuwapa ndoo mwaka 06 kisha akajiuzuru na timu ikabolonga then wamemrudisha...je wataliano nao wanataka nidhamu au?
Watazame waingereza, watazame argentina, wote wanataka mafanikio ndo maana wanawatimua makocha wasioeleweka kama huyu muigiza filamu wenu.

Hiyo miaka 9 aliyyokaa hapa nchini ni wazi kuwa kama angekuwa ni mtoto basi sasa hivi angekuwa darasa la pili.
 
Huyu Maximo anacheza na akili za watu. Watanzania lazima waamke na kuangalia na kuchambua huyu Maximo amefanya nini tangu aje.
Kwanza nadhani hana mpango unao heleweka wa kuendeleza soka hapa Tanzania na matokeo yake ni kubadillisha timu kila siku.
Visingizio kuwa Tanzania haina Proffessional players siyo ya msingi.
Binafsi ningependa kumuuliza swali Maximo, kwa nini wasaidizi wake (wanaotoka Brazil) hawakai?
Nitakwenda "ndani" zaidi, Kikwete wenu ana mpango wa kuendeleza soka (michezo)?
Fikra zake zina muelekeo wa maana kutuletea mgeni?
Mpaka sasa, kuna matayarisho gani timu ya taifa ifundishwe na Mtanzania?
 
ndiokweli CV ya Maximo haifahamiki kwani uongo?muulize hata yeye mwenyewe aseme ni wapi kafundisha soka kama atakupa jibu,,
 
Mziray ni mzee wa nongwa kila mara anamwandama Maximo,aseme wazi kama anataka nafasi yake si kuja hapa na visingizio kibao.
 
Maximo sio kocha!! simple....i dont see him adding an value to Tz football
 
Mziray ni mnafiki mkubwa! hatumuhitaji kwenye timu yetu ya taifa hata kama Maximo ataondoka leo. Hana la maana zaidi ya kuchonga saaaaana.
 
Tanzania inapoteza hela bure kutafuta makocha wa kigeni..fedha hizo zingetumika katika program nyingine za kukuza vipaji,kujenga vyuo vya soka,kuwafundisha wataalamu wetu wa kizalendo,ambao ndo wanajuwa mahitaji ya soka yetu na wanawajuwa vijana wetu,na wanaeleweka vizuri..tukakuza vijana tokea Juvenile...junior...central mpaka seniors...tukiwa na makocha hao hao akina Mashi na Mkwasa. Si tumeona Kombe la dunia la vijana U-17,Nigeria, watoto wa Kiswiss wanakanyaga gozi la ng'ombe kama watu wazima,wanasema watoto wale wamehamishwa makwao na wengi wapo katika vyuo vya soka wakikuzwa vipaji vyao...na U-swiss wanatarajia kuwa na timu tishio ya taifa kutoka na vijana wale muda si mrefu(wale wtoto si masikhara wanaujuwa hasa)..kwanini tusiwekeze kwenye program kama hizo...kama tumeweza kujenga uwanja kwanini tusijenge chuo cha michezo kukuza vipaji...wachezaji tulionao Stars wanacheza kama wamejifunza mpira ukubwani vile...hawana skills...hawafundishiki..ni aibu kusema timu ya taifa inafundishwa na kocha wa kigeni.
 
maximo katumia cv ya nchi yake kupata kazi tanzania na sisi tulivyo wavivu wakumchambua mtu kabla hatujamuajili ndio maana tumeangukia kwake.
 
Wa kulaumiwa ni sisi sababu ndio tulimtafuta tukampa mkataba
 
huyo Maximo anatugeuza sisi kuwa kichwa ya mwendazimu..hana jipya wala nini...kashatuchukua sehumu ambayo uwezo wake inamruhusu...hana first 11 mpaka leo anakula mshahara ya bure tuu..TFF nayo wajinga wanamuogopa....maximo atuachie timu yetu...Mpeni Timu Patrick Phiri tutaona mwanga and timu itakuwa tishio...angalia simba alivyogeuza mwaka jana and mwaka huu ni moto ya kuotea...go away maximo and leave our team to the ones who love it with their hearts....
 
Phiri nae akichemsha sijui tutamuita nani... ushabiki wa soka unataka moyo mgumu.. duh!!!!!!!
 
Mziray ni mnafiki mkubwa! hatumuhitaji kwenye timu yetu ya taifa hata kama Maximo ataondoka leo. Hana la maana zaidi ya kuchonga saaaaana.

Nakuunga mkono mkuuuulu

Mpira some times ni vichwa vya wachezaji tu kama kaujuzi ni mafundisho madogo sana kwa wachezaji wetu vinginevyo tuko poa tu na hiyo TFF nayo ifanyiwe reshuffle jamani wachezaji inao wachukuwa 100% ni simba na yanga au kwa kiswahili kingine ni wachezaji wa kutoka Dar tu,

Sijui tufanyenini hapo sasa. na tatizo sio kocha

Back
Top Bottom