[FONT=ArialMT, sans-serif]Kocha wa timu ya taifa, Marcio Maximo, ataendelea kuwa mwalimu wa Taifa Stars mpaka mkataba wake utakapomalizika na serikali imewataka 'wanaopiga kelele' kutaka afukuzwe, wamuache afanye kazi yake kwani gharama za kuuvunja mkataba wake ni kubwa mno.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kauli hiyo ya serikali ya kumtetea Maximo imekuja kufuatia shutuma mpya za mashabiki na wadau wengine wa soka kutaka kocha huyo Mbrazili ampishe mwalimu mwingine kwa madai kwamba uwezo wake 'umegota'. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza na Nipashe jana, Msemaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Jacob Tesha, alisema kuwa hakuna sababu ya wadau kumponda Maximo wakati amejitahidi kwa kiasi kikubwa kufanya mapinduzi kwenye soka la Tanzania.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Tesha alisema kuwa ni jambo la busara kama wadau hao kumpa nafasi Maximo kutekeleza mikakati aliyojiwekea kabla ya kumaliza mkataba wake mwakani.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Jamani hebu tumuunge mkono Maximo, tunataka atufanyie nini? Amelikuta soka letu likiwa sehemu isiyo nzuri na ametufikisha hapa, tumpe nafasi ili akamilishe programu zake kabla ya kumaliza mkataba wake," alisema Tesha.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aliongeza kuwa gharama za kuuvunja mkataba na kocha huyo kwa vigezo vya kutoridhishwa na uwezo wake ni kubwa kuliko inavyofikiriwa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo Tesha alieleza kuwa si vibaya kwa wadau wa soka kutoa maoni yao lakini wanapaswa pia kuyangalia na mazuri aliyoyafanya kocha huyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shutuma mpya dhidi ya Maximo zimekuja kufuatia matokeo mabaya katika mechi tatu za kirafiki za kimataifa zilizofanyika nchini Yemen hivi karibuni ambapo Stars ilifungwa mechi mbili na kutoa sare moja.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika mechi ya kwanza dhidi ya mabingwa wa Afrika Misri, Stars ilizidiwa kila kitu na kulala kwa magoli 5-1, kabla kulazimisha sare 1-1 katika mechi ya pili dhidi ya Yemen. Katika mechi ya marudiano na Yemen Stars ililala 2-1, na kuamsha hasira za Watanzania.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Miongoni mwa shutuma zinazomkabili Maximo ni kuwaita kwenye kikosi cha taifa makipa ambao hukaa benchi kwenye timu zao na pia kuwaacha nyota wengine -- jambo ambalo mwenyewe ameshalitolea ufafanuzi mara kwa mara kwamba ni ukosefu wa nidhamu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati huo, Maximo amepata sapoti kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama cha makocha nchini (TAFCA) Eugean Mwasamaki ambaye amesema kuwa makocha nchini wanatakiwa kujifunza kutoka kwa Maximo juu ya msimamo wake wa kutosikiliza maneno ya nje.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kocha anatakiwa kuwa na misimamo yake hasa kwenye suala la ufundi, makocha hawatakiwi kusikiliza maneno kutoka nje kama wanataka mafanikio, wafanye kazi kwa misingi ya kazi na taratibu waliyojiwekea wao na si kusikiliza kele za mashabiki, alisema Mwasamaki.[/FONT]