Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

NA LEO TUKIKANYAGWA NA ZENJ-BAR HUYU MKULIMA WA MATUNDA KWAO BRAZILI ANAONDOKA .... NA TIMU YA TAIFA INABIDI IWE ZANZIBAR...MAANA WATOTO WANAPIGA MPIRA WA UKWELI..NA KOCHA WAO NI MZAWA....SIE TUNANGANGANIA MFANYABIASHARA MAXIMO...enende jamani atuachie timu yetu ya taifa hana jipyaa
 
Lakini mie nina mashaka naona Maximo amefanana na Mheshimiwa!!!
 
........Hivi nani anaikumbuka timu ya USHIRIKA MOSHI.

Je mwaikumbuka TUPWISA LINDANDA WANA WA KAWEKAMO PAMBA YA MWANZA????? walikuwa wakicheza toto futball nchi nzima matokeo yake USHIRIKA MOSHI na PAMBA YA MWANZA viongozi wakaziua na enzi izo FAT ya Ndolanga na Ragge yaniii mpira huko ndipo ulikuwepo na hao viongozi wakauuuuwaaaaaaa kabisaaaaaa

........ Nataka kuwaambia Timu za Simba, Yanga na Mtibwa ni Timu nzuri na zinaonyesha kiwango cha soka kuliko hiyo TIMU YA MAXIMO NA TENGA WAKE.

Nikuulize kaka swali Taifa staaarrrrr si imejaaaa Simba, Yanag na Mtibwa na si ndio timu hiyo ya Maximo.

Tatizo hapo ni wachezaji wetu jamani hilo mkubali msikubali uwazi ndio huo vichwa vya wachezaji wetu ni vigumu kuelewa mapema mpira wa miguu ule wakucheza pamoja.

Hatuna Chuo cha Mpira kufundisha soka la vijana kuanzia umri wa miaka 7 hadi 20 hakuna. twategemea nini kwa soka la bongo.

Kumbukeni Ivory Cost walichemka kwenye mashindano walipo rudi kwao walipigwa rumande wote, haiwezekani nchi iwagharimikie nyie mkavurundee huko na kila kitu walipewa.

Leo hapa kwetu mwadai ni maximo huyo mtu mmoja ndie mwenye kosa??? twisha ambiwa na Mwinyi sisi ni kichwa cha mwenda wazimu hatupendi kubadilika hata kama Scorali au cappelo hata yule coach wa spain aje au Dunga hatutobadirika ng'ooooo mwelewe ivyo.

Tubadirishe mfumo wa kuchagua wachezaji wa Taifa stars
iwepo mikakati madhubuti ya kuitunza Taifa stars iwapo kambini, kiuchumi, ki psychology.
Kuwepo na mifumo mizuri huko kwenye vilabu za wachezaji watokapo, mfn waweze ku replya back au ku preview games walizocheza na makosa yao wayaone, yaani kuan mambo mengi sana ya kufanya ila TFF haitaki ku introduce izo system kwa wachezaji wetu na Lastly Nidhamu kweli hapo ndipo watanzania twashindwa kabisaaaaa
 
.......Inawezekana kabisa kuwa Maximo amefika ukomo, au wachezaji wamefika ukomo wa kufundishika. Kumleta Mzirai sio suluhisho.

Hapo mpwa umenena hiyo ndio ingekuwa Thread Heading,
Kuna timu mfano brazil wanawachezaji wengi kupita maelezo na wote ni wakali pale Coach ni kutumia akili kuwachagua kuingia timu ya Taifa na pili mbinu za kubadilisha na kufundisha zibadilike uwe mjanja sana na games na uutambue mfumo mzima wa mpira.

Sasa hapa kwetu tumekazania wachezaji wa simba oooh mara kaseja sijui chuji jamani why kiala mchezaji mwang'ang'ania anatoka Dar simba au yanga hao ndi wantumalizia mpira wetu kwanini tusililie kuwepo na chipukizi na wakuzwe kama serengeti boys hao wazeee wana miaka mingapi kwanza??? Ghana mfano mzuri wa kuigwa jamani hatuoni U20 world Cup Champions hamjiulizii wamefikaje hapo???? TFF tumeni watu waka jifunze na warudipo mkubali mabadiliko mwambiwayo na yafanyike ipasavyo na siokuwa ati watakuwa wamewadharau.
 
Wana JF kwa mara kadhaa MKULU anamtetea marcio maximo je ni kweli anahitaji muda zaid kuifundisha timu yetu ya Taifa?? kipimo ni kipi cha kumfanya awepo au asiwepo??
Niliwahi kuuliza huko nyuma kwamba mwisho wa kibarua chake kiwe lini duh niliyojibiwa Mhhhhhh!
Mkulu bado tu huoni hata sasa??
 
Naomba kuwa wa kwanza kusema muda wake na kiwango chake kimefikia kikomo! HE HAS TO GO FOR GOOD!
 
Mimi nafikiri bado tunamuhitaji, kinachotakiwa ni kubadili mfumo wa soka ili tuwe na klabu hodari zaidi zenye wachezaji chipukizi ambao watcheza soka la Ulaya. Ila hata aondoke Marcimo aje Ancelloti au Ferguson hakuna mabadiliko yoyote yatakayotokea kwenye national team
 
KiliTime Mkulu hawezi kumtoa Masio Maksimo sasa hivi, hiyo ndiyo kete yake come 2010 atakapoenda kwa vijana kuomba kura!! Atawaambia "mimi nimewaletea kocha toka Brazil ili aje kuinua kiwango cha mpira Tanzania, kama kiwango cha soka cha Taifa stars hakikuinuka, mlitaka mi niingie uwanjani kucheza???"

Vijana watambumbazika na kuona kweli Muungwana alifanya kazi, ila TFF ndiyo ilishindwa na hivyo kumpa kura za kishindo na kumuwezesha kushinda for the second term.

Mliona wapi ulaya au america ya kusini watu wanakosakata kabumbu la maana kocha wa timu ya taifa akawa naripoti kwa prezidaa wa nchi???? TFF haiwezi kumcontrol Maximo.

Maximo we endelea kucheza movie
 
Akitoka Maximo kazi apewe nani, Mziray??

Tatizo si Maximo, hata akija Capello hatafanya miujiza tunayoitaka. Tuanze kujenga misingi ya ushindi kuanzia shuleni na vilabu. Hakuna stability, kila siku ni mabadiliko continuity itapatikani wapi?
 
Akitoka Maximo kazi apewe nani, Mziray??

Tatizo si Maximo, hata akija Capello hatafanya miujiza tunayoitaka. Tuanze kujenga misingi ya ushindi kuanzia shuleni na vilabu. Hakuna stability, kila siku ni mabadiliko continuity itapatikani wapi?
Excellent Mkuu
 
Hizi thread ziko kama tatu hivi zinazofanana maudhui, Mods mngeziunganisha ili kuleta flow nzuri ya mawazo!!
 
kocha gani bana hata kiswahili hajui bana amekaa miaka 4................shiiiiit .......HANA UWEZO ANAYEBISHA AWEKE CV YAKE HAPA......LOL??
 
Anyway mimi si mtalaam wa soka (Soccer Science), ila kwa maoni yangu naona kuna kaprogress fulani kamepatikana tangia Maximo achukue mikoba ya ukocha. Mi nafikiri, tatizo letu ni kwamba vijana wetu hawana background nzuri sana ya nidhamu ya michezo na Elimu ya MICHEZO kwa ujumla wake tofauti na vijana tunaowaona wanasukuma kambumbu huko Europe, wale vijana walio wengi wamekulia kwenye ma academy ya michezo and they know exactly what football means to them, so kwao kocha nafikri kazi yake inakuwa ndogo sana ya kuwajenga kisaikolojia na kuwajenga kitimu zaidi!

Sisi vijana wetu wanaweza kuwa na vipaji sana vya soka lakini havijaendelezwa, kila moja anachomoka toka huko uswazi kivyake......, hakuna wakumjenga stamina, hakuna discipline ya michezo, yaani tabu tu...so hawa makocha wanao wafundisha cha moto wanakiona na wanajitahidi sana kwa kweli!

Hebu next level fikiria hivi. Una mtoto wako shule ya msingi lakini kila akifanya mtihani anafeli. Unamwuuliza tatizo nini hakupi jibu linaloeleweka unaenda kwa mwalimu unamwuliza tatizo ni nini? Mwalimu anakujibu kuwa mwanafunzi hafundishiki kwa sababu hajatokea kwenye mazingira ya wasomi-wasomi. Utamwelewa huyo mwalimu?
 
frankly speaking.marcio hajafanya kitu cha maana ila tu wachezaji wetu wako commited na uwezeshaji unaofanya na wadhamini.kama huamini ni mara ngapi timu ya taifa ilikuwa inakosa hata fedha za kuwapeleka hapo kenya ila mara zilipopatikana waliweza kufanya vizuri.bora aondoke uone jinsi maendeleo yatakavyoendelea katika soka letu. amemwacha kaseja kisa chuki binafsi kama enzi za mwameja kutoingia kwenye kikosi kisa chuki binafsi.
 
frankly speaking.marcio hajafanya kitu cha maana ila tu wachezaji wetu wako commited na uwezeshaji unaofanya na wadhamini.kama huamini ni mara ngapi timu ya taifa ilikuwa inakosa hata fedha za kuwapeleka hapo kenya ila mara zilipopatikana waliweza kufanya vizuri.
Hii ni point ya msingi pia. Nakubaliana na wew kwenye bold hapo
 
Anyway mimi si mtalaam wa soka (Soccer Science), ila kwa maoni yangu naona kuna kaprogress fulani kamepatikana tangia Maximo achukue mikoba ya ukocha. Mi nafikiri, tatizo letu ni kwamba vijana wetu hawana background nzuri sana ya nidhamu ya michezo na Elimu ya MICHEZO kwa ujumla wake tofauti na vijana tunaowaona wanasukuma kambumbu huko Europe, wale vijana walio wengi wamekulia kwenye ma academy ya michezo and they know exactly what football means to them, so kwao kocha nafikri kazi yake inakuwa ndogo sana ya kuwajenga kisaikolojia na kuwajenga kitimu zaidi!

Sisi vijana wetu wanaweza kuwa na vipaji sana vya soka lakini havijaendelezwa, kila moja anachomoka toka huko uswazi kivyake......, hakuna wakumjenga stamina, hakuna discipline ya michezo, yaani tabu tu...so hawa makocha wanao wafundisha cha moto wanakiona na wanajitahidi sana kwa kweli!

Hakuna maendeleo yoyote yaliyopatikana under Maximo tangu amekuja kabalisha balisha kikosi utafikri anajaribu kwachezaji ili kupata first 11. muulize ana wachezaji wangapi ambao bado wao katika kikosi chake cha kwanza alioanza nao? sidhani wanafika hata 2, sasa consistance utaipata wapi?, na work done yote ya nyuma ipo wapi?

Miaka hii michache tu alikuwa na timu ya taifa kafanya mess kibao kuichezea chezea timu yetu, anazidiwa hata na machocha wa club za ndani kwa tactics. defence bomu sijui kawafundisha wawashike ma striker wakati wanaenda kufunga?

Atuachie timu yetu aende kwao tushachoka. Ungeangalia mpira wa jana ungekubaliana na mimi kwamba tupo mbali sana kisoka. hata kama tungeshinda game ya jana ila Rwanda walicheza vizuri na wana tactics safi za kufundishwa, je hao nao wametoka soka academy?

Kocha mzuri anaonekana tu, mpe game 10 za mwanzo utajua, nani kama Phil?
 
Back
Top Bottom