Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

viongozi, kocha, wachezaji wote ni uharo mtupu...kwa hiyo kama mnataka vidonda vya tumbo na presha za kupanda na kushuka basi shangilia timu hilo.
 
Mbali na Maximo yupo kocha mwingine wa timu ya vijana anaitwa Tinoco....Hovyo kabisa, atimuliwe hata kesho, maana ana miaka miwili tangu kaja hapa, analipwa mshahara na marupu rupu kibao...muulize timu ya taifa ya vijana aliyonayo na imeshiriki mashindano gani so far, hakuna!!!

Thats not entirely true....mwaka jana Tinoco alipeleka timu ya TAifa ya vijana kwenye mashindano Burundi au Rwanda,ilikuwa ni East and Cenl championship i think.Tanzania ilifungwa mechi ya kwanza na timu ambayo ilikuwa na overaged players wengi tu.Ilikuwa ni issue kubwa lakini TFF walilalamikiwa kwa kutoendeleza malalamiko hayo,kwa sababu hko nyuma Tanzania ilishawahi kuwa disqualified kwa kuwa na overaged players.
Tukirudi kwa Maximo,kwa kweli mimi sijui kama yule kocha ni mzuri au mbaya,lakini wachezaji nao kwa sasa hatuna jamani hilo lazima tukikubali.Jumamosi iliyopita nilienda kuangalia ile mechi dhidi ya Mauritius,Tanzania ilitakiwa kushinda kwa zaidi ya goli tano za wazi! Yule Gabriel alikosa goli akiwa yeye na goli,akakosa penalti,na akakosa mengine kama matatu akiwa yeye na kipa! Sasa hapo jamani tutamlaumu kocha kweli? Kila ukiuliza kama hatuna strikers wengine,unaambiwa huyo Gabriel ndiye top striker! Mimi sioni kama kumfukuza huyu kocha kutaleta tofauti yeyote,lakini ninachomsifu ni kwamba yeye ni jasiri.He has belief in his players...anapoitoa hio belief anajua mwenyewe>Labda basi kama ikibidi, timu apewe Jamhuri Kiwelo(Julio) maana yeye anasema kuwa anajua cha kufanya
 
He should be fired if we loose the game with Cameroun or even a draw. It is time to show him a pink slip. Enough is enough. That is my opinion.

While i agree with most that Maximo is overated and overpayed, he is not the problem, put any coach in there and the results will pretty much be the same. World class football and for that matter world class players are not created overnight.

Where it is as if the media creates superstars overnight. In reality a tremendous amount of work and time has been spent grooming these players into the final product.

Tanzanians have been told thousands of times that there is no shortcut. It will take years and it needs to start with youth development. The 12 and 13 year olds of today if trained properly, given the right nutrition and discipline will eventually yield players capable of competeing on the world stage.

Our current crop of players really don't have a chance. People who expect to suddenly turn into great players just because we have a new coach are dillusional.
 
Mimi namlaumu Makamu wa Rais Dr Shein yaani wenzie wote wanafuatilia timu kwenda kambini na kwenye mechi yeye hata kutoa salam hajawahi kutoa!

Hivi baina yake na Boss wake ni nani alie busy zaidi?

Masatu karibu .
Kocha Masimo kesha wajua Watanzania yeye anaponda mahela yetu tu .Hakuna atakalo fanya na he is playing politics.Kama huamini leo narudia mara ya 2 ngojea utaona.
 
Swali dogo, Tanzania tuko tayari kumlipa World Class Coach Dollar 1 Million kwa mwaka? Alafu inabidi tuwe na mipango ya muda mrefu mambo ya kutegemea maajabu katika kipindi kifupi ni ujuha.
 
Wako wapi waliosema beauty pageants ni wrong priority?
 
Maximo naona atabaki sasa!!


Wako wapi waliosema beauty pageants ni wrong priority?

Pundit, naona una zungurusha maneno yangu au ya wengine waliokuwa na msimamo sawa na wangu kwenye ile thread ya u-miss....

Get it right dawg. I did not say beauty pageant is wrong priority, I said the way is currently being conducted in Tanzania is not as straight as it should be... in these competitions something is missing - and that i could call the absence of that thing "twisted priority".
 
Tanzania coach Marcio Maximo has signed a new one year deal to lead the Taifa Stars.
The Brazilian, whose contract was due to end on 30 June, had been offered a two-year extension but has only agreed to another 12 months.
The Tanzania Football Federation (TFF) made their offer after last week's memorable 0-0 draw with Cameroon in a 2010 World Cup qualifier.
"We wanted to continue with him for two more years, but he refused for personal reasons," TFF President Leodegar Tenga said.
"But if the team qualifies for the World Cup finals or the Nations Cup he will sign another contract."
The new deal is a direct result of Tanzania's impressive performance against the Indomitable Lions.

Source: BBC
 
Maximo apata ulaji Brazili

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', Maarcio Maximo amesema hataongeza muda wa kuinoa Stars, baada ya mkataba wake wa sasa kumalizika Julai mwakani.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Bulyanhulu jana, ambapo Taifa Stars imepiga kambi, Maximo alisema amepata ofa mbalimbali nchini Brazili ikiwa ni pamoja na kuinoa timu ya Taifa ya vijana ya nchi hiyo.

Hata hivyo alisema kutokana na kuishi vizuri nchini hakutaka kuvunja mkataba wake wa kuinoa Taifa Stars, badala yake ameamua mkataba wa sasa utakapomalizika hataongeza.

Alisema pia katika masuala ya kitaalam ni vyema akaja kocha mwingine akaendeleza programu aliyoianzisha, badala ya kocha mmoja kufanya programu hiyo peke yake.

Lakini Maximo alisema licha ya kupewa ofa hiyo nchini Brazili, hawezi kuondoka kwa sasa, hadi mkataba wake utakapomalizika na kuwataka Watanzania wasiwe na wasiwasi.

Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela alikiri kufahamu Maximo kutoongeza mkataba baada ya kumalizika wa sasa.

Lakini alikana kwamba kutoongeza mkataba kwa Maximo kunatokana na kauli aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akihutubia Bunge hivi karibuni mkoani Dodoma, alipoitaka TFF kuanza kujitegemea kumlipa kocha wa Taifa Stars kwa kuwa hatua ya sasa ya serikali kumlipa Maximo si ya milele.

Alisema tayari TFF imeanza mpango wa kusaka fedha za kumlipa kocha atakayefika badala ya Maximo na kwamba hata sasa bado fedha za kumlipa Maximo zipo.

Kocha huyo alitua nchini Julai mwaka 2006, ambapo ameiongoza Taifa Stars katika michuano mbalimbali ikiwemo ya kuwania kufuzu fainali za Afrika zilizofanyika Ghana Februari mwaka huu, lakini Stars haikupata tiketi hiyo, pia hivi sasa anaiongoza timu hiyo katika michuano ya kuwania kufuzu kombe la dunia mwaka 2010, ambapo tayari Stars imeshakosa tiketi hiyo.

Source: Majira
 
Aende zake kwanza Tanzania sisi mpira si asili yetu, wabongo wazuri kwa majungu na michezo ya kuigiza hamuoni serikali yetu ya JK na usanii kila kukicha? Maximo nenda zako enough is enough ...

hana jipya akwende
 
Mrithi wa Maximo kuwa bei poa


Pamoja na kiwango cha juu cha ujuzi na uzoefu, kocha atakayekuwa na gharama nafuu za malipo ndiye atarithi nafasi ya mwalimu Marcio Maximo kwenye timu ya taifa, Taifa Stars, shirikisho la soka, TFF, limesema.

Katibu mkuu wa shirikisho la soka Frederick Mwakalebela alisema mbali na kuangalia wasifu wa makocha wote watakaotuma maombi ya kuajiriwa, pia TFF itazingatia wenye gharama nafuu za malipo.

``Makocha wanatofautiana kwa mishahara mikubwa, hivyo tutaangalia pale tunapoweza,`` alisema Mwakalebela ambaye alibainisha inapoweza TFF ni mshahara ambao ``sio mkubwa sana au mdogo sana.``

Mbali na mshahara usio mkubwa sana au mdogo sana, kocha mpya wa Taifa Stars baada ya kukamilika kwa mkataba wa Maximo Julai mwakani atalipiwa pango la nyumba na gari dogo la kutembelea.

Maximo analipwa na serikali dola 10,000 za Marekani (sawa na shilingi milioni 11.6) kwa mwezi, kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.

Serikali imeshaeleza kusudio la kuacha kulipa mshahara wa kocha wa Stars na kujikita katika kusaidia kunyanyua michezo midogo kama riadha.

Utafutaji wa mwalimu mpya wa timu ya taifa utakuwa chini ya Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, alisema Mwakalebela.

``Inabidi huu mchakato uanze mapema, kwani sio hadi Maximo anamaliza ndio tunaanza kuhaha ndio maana tunasema benchi la ufundi litakapotangaza nafasi hiyo ya kazi itakuwa haraka.``

Tayari kocha mkuu wa timu za vijana za taifa Marcus Tinoco kutoka Brazili pia kama Maximo, ametangaza nia yake ya kumrithi mwalimu huyo.

Hatahivyo upo uwezekano mdogo wa Tinoco kupata nafasi hiyo kutokana na kutokuwa na uzoefu wa kutosha kimataifa na ukweli kuwa Mbrazili aliyemtangulia ameshindwa kufikia malengo ya TFF na serikali katika miaka mitatu atakayofundisha.

SOURCE: Lete Raha
 
Maximo mbioni kuikimbia Tanzania


KOCHA wa Kilimanjaro Stars, Marcio Maximo huenda akajiunga na moja ya klabu za Ligi Kuu ya Afrika Kusini au China.

Mbrazil huyo ambaye mkataba wake unamalizika Julai, hajaonyesha nia ya kutaka kuongeza na ameishauri serikali na Shirikisho la soka la Tanzania limpe tenda msaidizi wake, Marcus Tinocco.

Kocha huyo akizungumza mjini hapa jana alisema kwamba amezungumza na klabu mbili za Ligi Kuu za nje, lakini akaziambia zisubiri kwanza mkataba wake umalizike.

"Nimezungumza na klabu moja ya China na nyingine ya Afrika Kusini wote wananihitaji, lakini nimewaambia wasubiri kwanza nimalize mkataba wangu nikabidhi majukumu niliyopewa,"alisema Maximo.

"Kila mmoja alikuwa akitaka nivunje mkataba huku halafu niende nikakataa kwa vile niliwaambia tatizo sifedha.

"Lazima uangalie na utu na ulipoanzia, umefikia wapi. Nikishamaliza mkataba wangu ndio nimewaambia nitakaa nao tuongee vizuri,"alisema kocha huyo na kugoma katu katu kutaja jina la klabu hizo kwa madai kuwa ni siri.

Kocha huyo alisema kwamba bado hajafikiria kubadilisha mawazo ya kuondoka Tanzania.

Maximo alisema kwamba ameanzisha msingi mzuri ambao anahitaji mtu mwenye mtazamo mwingine kuuendeleza.

Tangu akabidhiwa Stars miaka miwili iliyopita, Maximo amecheza mechi 39 akiwa ameshinda 17, sare 13 na kupoteza
tisa.


Habari hisani kubwa ya Mwananchi
 
Dawa ni kuwapa timu makocha wetu (Mziray, Msola, Mash nk) na mshahara kama anaopata Maximo na marupurupu mengine. Lakini tu wasiingiliwe. Tatizo la makocha wa kibongo ni kuingiliwa na viongozi wa TFF wakati wanachagua timu ya Taifa. Kila mtu analeta jina/majina yake.
 
Maximo ni kocha mkuu wa timu yetu ya taifa, kwa hiyo matokeo yoyote mabaya ni lazima awajibike. Tusilaumu wachezaji, kwani hao wachezaji ni nani anayewateua? Ni yeye mwenyewe!!! Kama kweli angekuwa serious basi angefanya scouting ya kutosha nchi nzima kutafuta wachezaji mahiri wa soka ambao naamini wapo wengi tu, ila hawajapata exposure. Mambo ya kusubiri mpaka mchezaji aibukie Kagera Sugar baada ya kuchezea timu ya kijiji chao kwa miaka kadhaa, kisha aje Yanga au Simba, halafu umchukue Stars na uishie kumlaumu kwamba hafundishiki IS NOT FAIR!!

Mbali na Maximo yupo kocha mwingine wa timu ya vijana anaitwa Tinoco....Hovyo kabisa, atimuliwe hata kesho, maana ana miaka miwili tangu kaja hapa, analipwa mshahara na marupu rupu kibao...muulize timu ya taifa ya vijana aliyonayo na imeshiriki mashindano gani so far, hakuna!!!

Tuangalie upya hawa jamaa, wanatulisha sumu!!!
Maximo is a great coach.Ni yeye aliyemuibua Geofrey Bonny kutoka Prison ambapo amecheza kwa takriban miaka 4 bila yanga kumuona.Ni yeye aliyemuibua Kigi Makasy , Jerry Tegete.Amefanya sehemu yake.
Maximo amefika hapa amekuta mfumo mbovu na bado upo wa uongozi wa vilabu.Ni kupitia vilabu ndipo utapata timu nzuri ya taifa.
Amefanya kazi katika mazingira magumu sana.Tulipofika ndani ya miaka hii miwili ni pakubwa mno.Kama atakubali kurefusha mkataba ni vema na akiamua kuondoka ametuachia kitu cha kujivunia.
Since 1980 Lagos, sasa tunakwenda Abdijan 2009.Siyo kitu kidogo.
 
Maximo anatishia Nyau, kila wakati anaipenda sana hii kauli kuwa anahitajika na timu nyingine. Sio kwamba yawezekana ni uongo. Lakini akifanikiwa kuifikisha Timu yetu ya Taifa angalau nusu fainali, atataka kuongezewa dau, kwa kusema kuna timu zinamuhitaji, akitolewa mapema hatabembelezwa sana, hivyo ataondoka taratibu. TFF sasa wako na bembeleza mwana:-

Mrithi wa Maximo kuanza kusakwa Aprili
na Makuburi Ally

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limemtaka Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mbrazil, Marcio Maximo, kwamba hadi kufikia Aprili mwaka huu, awe ameamua kama ataendelea kuifundisha timu hiyo au la.

Hayo yalisemwa jana na Rais wa TFF, Leodegar Chilla Tenga, wakati akizungumzia masuala mbalimbali ya Shirikisho yatakayofanywa ndani ya miaka minne ijayo.

Alisema, kwa vile mkataba wa mwaka mmoja wa Maximo utafikia tamati Julai mwaka huu, wamemsihi hadi ifikapo Aprili awe ameamua kama ni kuongeza mkataba au vinginevyo.

Tenga alisema, awali kabla ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja, Maximo hakutaka kuongeza tena, lakini kutokana na mafanikio makubwa, wamempa nafasi ya kufikiria upya msimamo wake wa awali.

Tenga alisema, kama Maximo atazidi kushikilia msimamo wake wa awali, TFF italazimika kuanza mchakato wa kusaka kocha mwingine atakayetwaa mikoba baada ya mkataba wa Maximo kukoma.
Source: Mrithi wa Maximo kuanza kusakwa Aprili
 
Ni kipndi kirefu sasa tangu kocha marcio maximo anaifundisha timu ya taifa ya tanzania.
Kwa mawazo yangu maendeleo ya timu ya taifa yaliyopatikana kwa uongozi wa kocha marcio maximo ni ya taratibu mno.
Tumeishi kwa matumaini kwa muda mrefu sasa.
Kufukuzwa kwa kocha scolary wa chelsea kumenikumbusha kuhusu kocha marcio maximo.
Kisha najiuliza, je ni kweli kwamba maendeleo ya timu ya taifa ya tanzania yanaridhisha kiasi cha kuona kwamba ni vema kocha maximo akaendelea kuvumiliwa?
Au kocha maximo anayo kinga ya kumzuia asifukuzwe kama scolary?

Marcio Maximo, a Brazilian, is the head coach of the Tanzania National Football Team. He will be responsible for the Taifa Stars.
His appointment by the Government of Tanzania follows a promise made by the President of Tanzania, Jakaya Kikwete to ensure improvement of football in the country.
He had previously coached Livingston Football Club in Scotland in 2003/2004. He was also a member of Brazil's youth coaching staff (under-17 and under-20) in 1992 and 1993.
His main task was to qualify the Taifa Stars for the 2008 African Nations Cup finals in Ghana for the first time in more than 25 years. However, he failed to reach that ambition but his recent focuses have been on qualifying for the 2010 World cup. Recently Maximo has meant a lot to Tanzania so as to improve football. Under his leadership, the ranking of the Tanzanian team has risen. Marcio Maximo has made Tanzania to qualify for CAN finals for home players. These final shall take place in Ivory cost from February 22 to March 8th, 2009. Tanzania qualified after beating Sudan 5-2 goal aggregate. Marcio Maximo did a lot to improve Tanzanian football. Brazilian coach, Marcio Maximo, has extended his contract with the Tanzania Football Federation (TFF) for another year until july 2010
 
Anyway mimi si mtalaam wa soka (Soccer Science), ila kwa maoni yangu naona kuna kaprogress fulani kamepatikana tangia Maximo achukue mikoba ya ukocha. Mi nafikiri, tatizo letu ni kwamba vijana wetu hawana background nzuri sana ya nidhamu ya michezo na Elimu ya MICHEZO kwa ujumla wake tofauti na vijana tunaowaona wanasukuma kambumbu huko Europe, wale vijana walio wengi wamekulia kwenye ma academy ya michezo and they know exactly what football means to them, so kwao kocha nafikri kazi yake inakuwa ndogo sana ya kuwajenga kisaikolojia na kuwajenga kitimu zaidi!

Sisi vijana wetu wanaweza kuwa na vipaji sana vya soka lakini havijaendelezwa, kila moja anachomoka toka huko uswazi kivyake......, hakuna wakumjenga stamina, hakuna discipline ya michezo, yaani tabu tu...so hawa makocha wanao wafundisha cha moto wanakiona na wanajitahidi sana kwa kweli!
 
Anyway mimi si mtalaam wa soka (Soccer Science), ila kwa maoni yangu naona kuna kaprogress fulani kamepatikana tangia Maximo achukue mikoba ya ukocha. Mi nafikiri, tatizo letu ni kwamba vijana wetu hawana background nzuri sana ya nidhamu ya michezo na Elimu ya MICHEZO kwa ujumla wake tofauti na vijana tunaowaona wanasukuma kambumbu huko Europe, wale vijana walio wengi wamekulia kwenye ma academy ya michezo and they know exactly what football means to them, so kwao kocha nafikri kazi yake inakuwa ndogo sana ya kuwajenga kisaikolojia na kuwajenga kitimu zaidi!

Sisi vijana wetu wanaweza kuwa na vipaji sana vya soka lakini havijaendelezwa, kila moja anachomoka toka huko uswazi kivyake......, hakuna wakumjenga stamina, hakuna discipline ya michezo, yaani tabu tu...so hawa makocha wanao wafundisha cha moto wanakiona na wanajitahidi sana kwa kweli!

Kwanini sisi hatuwezi lakini wao wanaweza?
 
Back
Top Bottom