Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

vyovyote vile
lakini tungekuwa na uhuru wa kumfukuza
kama angeshindwa..
Sasa huyu maximo tunashindwa kumfukuza
kwa sababu ya jk.
Wabongo banaaaaa mmeshaanza kumtupia lawama JK eti ndo kamleta acheni hizo ..wachezaji wenu hawafundishiki hata akija The Special One Maurinho ni bure tuuuu.
Maximo angekuja kipindi wapo wachezaji walioshiba kama akina Mwameja,Athman Juma Chama,Juma Mkambi,Victor Mkanwa,Juma Mgunda etc. hapo bongo ingefika mbali even World Cup.Lakini kwa hawa 5'5 ft wachezaji, msitegemee miujiza Hata Rwanda na Burundi wakija wanatubamiza jamani.Vile vile ikumbukwe unawezakuwa mchezaji wa 5'5ft but ukawa na stamina, unawakumbuka akina Omar Hussein Keegan??au Raphael Paul-RIP, au Abubakar Salum?????walikuwa wafupi lakini stamina ilikuwepo.Wachezaji wa sasa chips/kuku halafu mnataka waende world cup wakapambane na akina Essien,Obi Mikel,Lampard,JT kweli????mwacheni Maximo afanye kazi yake,hao akina Mziray si walikuwepo enzi hizo ??Na tulikuwa kichwa cha mwenda wazimu???.........ndio hio wandugu.
 
Essien,Obi Mikel,Lampard,JT kweli????mwacheni Maximo afanye kazi yake,hao akina Mziray si walikuwepo enzi hizo ??Na tulikuwa kichwa cha mwenda wazimu???.........ndio hio wandugu.

Mkuu wewe ni wa Darajani? Chelsea tupu hao! Lakini mbona akina Mesi, Shaun Wright Phillip, Walcot wote wana maumbile madogo! labda useme wachezaji wetu hawafundishiki sababu hawana akili inaweza kuwa sababu
 
Huyu Maximo aondeke muda aliokaa TZ kama kocha unamtosha
kwanza naona ugomvi wake na wachezaji unakuwa kama vile ana personal enterest
anashindwa kuweka vijana wazuri kisa watovu wa nidhamu huo utovu wa nidhamu walionao ukimwambia elezea anajiumauma tu

aende
 
Hata akija mtu kutoka mbinguni, bila kubadilisha program za mpira Tanzania na kukuza vipaji vya watoto mpira hautaendelea ng'ooo.Mtakua kila siku mmnataka kubadili makocha.
 
Maximo hata leta jipya...nashukuru ametu improve hiyo miaka 3 lakini hana mkakati mpya tena wa kutupeleka mbele...tunahitaji mtu mwingine aichukue timu hapo ilipo nae aisogeze mbele kidogo....ndio maana anakuwa mbogo na maswali kwa vile hatopata tena kazi ya kulipwa kama hii....hivi mziray angelipwa hiyo hela angeshindwa haya ya Maximo 5-1?Maximo bdio kocha wa kwanza Taifa Stars kupata corporate sponsorship.?...
 
Maximo hata leta jipya...nashukuru ametu improve hiyo miaka 3 lakini hana mkakati mpya tena wa kutupeleka mbele...tunahitaji mtu mwingine aichukue timu hapo ilipo nae aisogeze mbele kidogo....ndio maana anakuwa mbogo na maswali kwa vile hatopata tena kazi ya kulipwa kama hii....hivi mziray angelipwa hiyo hela angeshindwa haya ya Maximo 5-1?Maximo bdio kocha wa kwanza Taifa Stars kupata corporate sponsorship.?...

ni kweli tunahitaji mabadiriko
 
Huyu jamaa ikiwezekana hata leo hii afungashe vilago aende zake,bora timu ibaki bila kocha kuliko kuwa na kocha wa dizain hii,wazo lililo nijia ni kwamba huyu hawezi kuondoka kwa matakwa yake,bali naomba ushirikiano wa wazee wote wanaojua sanaa ya kutengeneza majini,wamtupie majini yatakayomsumbua asiitamani tanzania na vitanzania(vilivyomo) vyake,hilo ndio suluhisho!!
 
Acheni ukurumbizi huwo, kwanini msilaumu uwezo mdogo wa wachezaji wenu ambao hawafundishiki, vifuu tundu, hawafahamu. Kwanini mnakuwa watovu wa shukurani, ni wakati wa Maximo angalau Tanzania imeona 'profeshino' wawili wa tatu. Na halafu, si Maximo mwenyewe alipomaliza mkataba wake alitaka kuondoka kwanini muanze kupiga mbiu kama vile yeye anang'ang'ania, kwa lipi? Si TFF wenyewe waliomlazimisha abakie...mbona mnakuwa watovu wa hisani jamani!!!!!!!!!
Hapa hakuna cha hisani bwa mdogo,huyu jamaa kaja kufanya kazi na mshahara mnono anapokea,dogo unatakiwa kujua kuwa hakuna kisichofundishika,kama mbwa anaweza fundishwa akaelewa iweje uniambie wachezaji wetu hawafundishiki?Siku zote huwezi mfundisha mtu kituanachokijua,huyu jamaa mbinu zake za kufundisha tuu ndio mbovu lakini si kweli kama wachezaji hawafundishiki,mbona Phiri anaenda sawa na watoto wa msimbazi,mtu kama huyu ukimwambia kuwa wachezaji hawafundishiki atakuelewa kweli?Na kama kweli hawafundishiki mbona maximo halalamiki kuhusu hili?Jiheshimu dogo!!
 
Maximo shuold try and borrow a leaf from the Zambian National coach . The Zambian national coach done good for the Zambian national team. Maximo maybe should go to Zambia for a study tour together with TFF officals.
 
Marcio Maximo, a Brazilian, is the head coach of the Tanzania National Football Team. He is responsible for the Taifa Stars.

His appointment by the Government of Tanzania follows a promise made by the President of Tanzania, Jakaya Kikwete to ensure improvement of football in the country.

He had previously coached Livingston Football Club in Scotland in 2003/2004. He was also a member of Brazil's youth coaching staff (under-17 and under-20) in 1992 and 1993.

His main task was to qualify the Taifa Stars for the 2008 African Nations Cup finals in Ghana for the first time in more than 25 years. However, he failed to reach that ambition but his recent focuses have been on qualifying for the 2010 World cup. Recently Maximo has meant a lot to Tanzania so as to improve football. Under his leadership, the ranking of the Tanzanian team has risen. Marcio Maximo only made Tanzania to qualify for CAN finals for home players. These took place in Ivory cost from February 22 to March 8th, 2009. Tanzania qualified after beating Sudan 5-2 goal aggregate. Tanzania performed badly in the tournamaent.Marcio Maximo, has extended his contract with the Tanzania Football Federation (TFF) for another year until july 2010.

Former Livingston FC Coaches

* Scotland Jim Leishman (1995–1997)
* Scotland Ray Stewart (1997–2000)
* Scotland Jim Leishman (2000–2003)
* Brazil Marcio Maximo Barcellos (2003)
* Scotland David Hay (2003–2004)
* Scotland Allan Preston (2004)
* Scotland Richard Gough (2004–2005)
* Scotland Paul Lambert (2005–2006)
* Scotland Alec Cleland (Caretaker, 2006)
* Scotland John Robertson (2006–2007)
* Scotland Dave Bowman (Caretaker, 2007)
* England Mark Proctor (2007–2008)
* Italy Roberto Landi (2008)
* Scotland Paul Hegarty (2008–2009)
* Scotland David Hay (Caretaker, 2009)
* United States John Murphy (2009)
* Scotland Gary Bollan (2009–)
 
Hata akija mtu kutoka mbinguni, bila kubadilisha program za mpira Tanzania na kukuza vipaji vya watoto mpira hautaendelea ng'ooo.Mtakua kila siku mmnataka kubadili makocha.

sasaaaa! wakina kibadeni walifanyaje???
 
KWANIII...huyu jamaa anatutaka nini sie watanzania wenye machungu na nchi na timu yetu ya taifa????....marcio maximo if i may ask u kistaarabu kabisaaaaaaa....what do u really want from us verrrry poor tanzanians with our nation team..our only remaining hope for a little happines under the sun???...

madini yetu wamechukua...mbuga nazo wamechukuwa...ardhi nayo wanakuja kuichukuwa...hata haka ka-timu ka mpira wa miguu na wewe unakangangania???...TUACHIE BABA MAXIMO TIMU YETU...HATUNA RAHA TENAA...TUMEHAMIA LIGI YA UINGEREZA NA SPAIN SASA TUNATAWANYIKIA TIMU ZA WENZETU ZA AFRICA ...SIE HATUNA HATA CHA KUJIVUNIA NA KUJIONA NI WATANZANIA TULIOJAALIWA JAPO KITU KIMOJA TUUU NA MWENYEZI MUNGU....

Mr. Marcio Maximo pleasee we are on our bended knees..pleaseee leave us alone with our nation team tujipange upya na wachezaji wetu wasiokuwa na nidhamu hata chembe....(ila ndio hao wanaitwa na timu za ulaya)

au wewe mzee maximo ndio hauna nidhamu???....toa kwanza boriti kwenye jicho lako ili uone kibanzi machoni kwa mwenzako......GO PLEASE MAXIMO WE DONT WANT U ANYMOREEEE...TIRED OF U AND UR COACHING SKILLZ SOUNDS LUNATTIC...
 
Huyo jamaa hana mpya muda wake umeshafika wa kufungasha virago...apewe notice ya mwezi moja kuondoka akikata tutamuondoa kistarabu kama tulivyomuondoa Benziski pale Simba..benziski alikata kata kata kuondoka na alikubali kufundisha bure lakini tulimpandisha KLM usiku bila yeye hata kuelewa kinachoendelea.

Maximo time is up your holiday has come to an end and you have repead more than you have planted so please do the needful and Go Away!!!! acha propoganda za kijinga
 
Huyu alipaswa kufungasha virago siku nyingi sana. Bila shaka baada ya Challenge Cup ataondokwa mwenyewe kwa aibu kwani sidhani kama Watanzania wataendelea kumvumilia. Natabiri kuwa atachapwa bakora na Watanzania wenye hasira siku timu itakaporejea bila ushindi kutoka kwenye michuano ya Challenge.
 
sasaaaa! wakina kibadeni walifanyaje???
hahahaha thats a big joke my friend...haya akina kibadeni walifanyaje vile tena mkuu?tulifika mashindano ya Africxa cup tu, si ndio mazee?.Yes, mda wa akina kibadeni umepitwa na wakati kaka, sasa ni kuboresha ligi zetu kuanzia ligi kuu mpaka ligi daraja la tatu. Pili program za mpira ni mbov Tanzania, tim hazina vijana, kwa mtaji huo bila kufanya hayo mambo tutalia wachuya kaka.huu sio mda wa akina kibadeni, hata yeye na mzirai wanaweza wakawa makocha wazuri lakini bado program ya mpira Tanzania kwa sasa itawaangusha. Angalia mpira wa wakati ule na mpira wa sasa.Ndo maana kuna tim hata ulaya mfano Hungary zamani ilikua tishio, lakini hawakwenda na mabadiliko ya mpira sasa hamna kitu tena pale hungary. Mpira umeisha kabisa.TUBADILI MIFUMO JAMAN WATANZANIA TUSIWE WAJINGA NA KUTETEA UJINGA TUU.
 
Mkuu wewe ni wa Darajani? Chelsea tupu hao! Lakini mbona akina Mesi, Shaun Wright Phillip, Walcot wote wana maumbile madogo! labda useme wachezaji wetu hawafundishiki sababu hawana akili inaweza kuwa sababu
Mkuu mie ni mzee wa Imarati But hao nimeona ndo wachezaji wenye nguvu zao.....na wote watakuwepo kule Jo'burg ndo maana nimewaweka hapo ingawaje 29th November watachukua kipigo toka kwa vijana wa Imarati.
 
Ni sawa na kumpigia zeze mbuzi .Nawaambia Maximo hawezi kuachia ngazi kwanza kesha nogewa bana TZ kwa mtu kama Maximo anayepata mapesa kwa kazi ya wiki kwa miezi mitatu na usisahau na u VIP anaopata ah pepo zote hizo aziache ukiongeza na sasa kauanza Ukanumba!mtasema mtachoka ,ataondoka tu pale mkulu akipenda
 
Back
Top Bottom