Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

kesha nogewa bana TZ kwa mtu kama Maximo anayepata mapesa kwa kazi ya wiki kwa miezi mitatu na usisahau na u VIP anaopata ah pepo zote hizo aziache na sasa kauanza Ukanumba!mtasema mtachoka ,ataondoka tu pale mkulu akipenda[/QUOTE]

Ahaaa ila mkulu naye inamaana aoni kama kuendelea kumhudumia kocha huyu akutofautian na ufisadi maana anaendelea kula pesa za wananchi bila kutimiza tunachokitarajia
 
Ahaaa ila mkulu naye inamaana aoni kama kuendelea kumhudumia kocha huyu akutofautian na ufisadi maana anaendelea kula pesa za wananchi bila kutimiza tunachokitarajia[/QUOTE]



Mkulu sasa aambiwe sasa ajira ya mtu huyu itegemee matokeo ya mashindano haya asiendelee kutuongezea gharama bila mafanikio tumeshuhudia akiwateme wachezaji kadhaa lakini kilichofanyika ni "kutoa mgonjwa na kuingiza mahututi" ili wapatikane wa kuwalaumu! tusikubali kudanganyikaaaaaaaaa!
 
tatizo kashakua full misheni tauni,hadi movie za kibongo yumo....kiukweli, alipotufikisha panatosha,apewe mwingine..
 
Chuji alimuambia Maximo aache mambo ya Chuji, kaseja na Boba sasa awaeleze Watanzania KWA NINI HADI SASA Nchi haina Kikosi cha kwanza katika Timu ya Taifa. Swali hili ni muhimu sana akalijibu. Enzi za wakina Zamoyoni Mogera, Athmani China, Malota Soma, n.k ukisikia Timu ya Taifa LAZIMA uwe na Kikosi chako tayari mkononi kwamba hawa ndiyo wacheza wa Kikosi cha kwanza. Nenda hata kwao na Maximo (Barazil) Timu yao ya Taifa inao wachezaji 11 wa kwanza, nenda hata kwa Timu za Mchangani mkiwa na mechi mnajijua kabisa kama hakuwepo fulani, fulani na fulani wa fulani Timu haijatimia. Sasa leo Maximo aliowapelekea Brazil sijuwi wamebaki wangapi ktk timu ya Taifa, alikwenda nao Denmark sijuwi kuwaaacha wapi? n.k n.k. Lakini Huo Mshahara na marupurupu anayopewa Maximo na familia yake angetafutwa Kocha kutoka Nchi yoyote ya Kiafrika ambayo soka lao lipo juu angeweza angaliu hadi sasa kuwa na Kikosi cha kwanza, hata kama kinafungwa LAZIMA UWE NA CHA KUONYESHA kwamba hii ndiyo 11 yangu pamoja na kwamba kila siku inafungwa.

Anachofanya Maximo na Biashara, pengine uwezo wa Ukocha hana matokeo yake akiambiwa kweli na Wachezaji wenye vipaji vyao (Kaseja, Chuji, Bobani, n.k) anawaeleza hawana nidhamu, WHAT IS THE DEFINITION OF NIDHAMU? sijuwi kama mnakumbuka kisa cha Zamoyoni Mogela, Hamisi Thobias (Gagarino), Athumani China walipomueleza Mhe. Naibu Waziri wa Michezo Mhe. Bendera wakati huo aliteuliwa kuwa kocha wa Mpira wa Timu ya Taifa. Walimueleza wewe siyo kocha wa Mpira wewe ni Kocha wa riadha, sasa wakati wa mazoezi ya kukimbia walikuwa wanaingia uwanjani kwani ndiyo taaluma ya Mhe. Bendera, lakini wakati wa kufundishwa namna ya kujipanga, kushambulia, kupiga chenga, kutoa pasi n.k wachezaji hao walimuambia hawawezi kufundishwa na yeye. Nadhani Maximo ni Kocha wa KUZUNGUMZA KIINGEREZA CHA KIBRAZIL.

Hebu tufike mahala tukumbuke msemo wa Hayati Mwl. Nyerere alipokuwa anawahutubia Wafanyakazi wa Tanzania wakati wa Kilele cha sikuu ya Wafanyakazi Mkoani Mbeya alisema

"Mtu akikushauri jambo la Kijinga na anajua kwamba analokushauri ni la kijinga na wewe ukailichukua na kulifanyia kazi ujue amekudharau sana."

Huyo Ndiyo Maximo anashindwa kutuonyesha matunda ya kazi yake, matokeo yake anatufanya tuelewe kwamba "NIDHAMU" kila siku "NIDHAMU" Ebu kama watu hawana nidhamu si aondoke.

HUYO NI MGANGA NJAA, MCHIMBA CHUMVI hana analolijua katika medani ya Soka.

Watanzania tufikie mahali tuseme ukweli. Hata ukitazama zile mechi ambazo TZA tumeshinda kiwango cha Mpira ni kibovu Kibovu ni kama mipira ianwagonga wachezaji wa Tanzania na kwenda mbele. Huoni kwamba sasa Timu inataka kufanya mashambulizi. Hivi nani anaikumbuka timu ya USHIRIKA MOSHI. Ulikuwa unasikia raha kuiona inapocheza. na Nataka kuwaambia Timu za Simba, Yanga na Mtibwa ni Timu nzuri na zinaonyesha kiwango cha soka kuliko hiyo TIMU YA MAXIMO NA TENGA WAKE.
 
Ni wazi sasa maximo amekalia kuti kavu, jana alekuwa mbunge wa Kigamboni magoba aliitaka Tff Kumfukuza ktk timu ya taifa maximo kutokana na kuonekana uwezo mdogo ktk timu ya taifa
source: Redio 1


Safi sana Mh. magoba....yani tz tupo slow kwenye kilakitu eti subira subira lazima tujue huu ulimwengu tuliopo sasa hv ni wa .com yani ni fasta decission kwa kwenda mbele.

sasa kila siku tusubiri tusubiri, migodi yani kila kitu matatizo tu.

go back to your country pliiiiiiiz
 
Richmond, meremeta, ufisadi, deep green,... vimetushinda, jamani hata kumtoa Maximo tumeshindwa??????? Watanzania hususani wapenda socker tuamke!!!!
 
huyu maximo safari imewadia sasa, aanze kuosha mabegi mapema....
 
TFF hawawezi kumfukuza huyu bwana kwani wao hawajamwajiri, kaajiriwa na IKULU.
lakini je tatizo letu ni kocha kweli? maana huwa tunapenda kutafuta sababu rahisirahisi kama hizi bila kutafiti vizuri.
kwanza kwa timu kufungwa ni moja ya matokeo, kila kocha atakeyekuja kuna wakati timu itafungwa.
mimi naona tatizo letu huenda si timu ya taifa bali tatizo lipo toka kwenye timu zetu za ligi, mbona hata hizi timu zetu hazina makombe kama CAF nk? huwa tunaringiana hapahapa tu?
je wachezaji huku kwenye ligi wanatunzwa vipi kimchezo, kisaikologia nk?

lazima changes ziazie huku chini tukiwa na vilabu imara tutapata wachezaji wazuri na pia tutakuwa na timu ya taifa iliyo imara.
 
kama wachezaji wana tatizo na kocha naye ana matatizo anaendekeza visasi tu
 
Kama mbunge hajui kocha ameajiriwa na nani, anaweza kweli kujua uwezo wa Kocha?

Kwanini anatoa suggestion ya kumfukuza tu bila kutuonesha kocha anyefaa zaidi ya Maximo?
 
Mazimo to me is not a coach.maana sijawai kuona CV yake na wapi kawahi kufundisha.ni sana tupu...huyo aliyemleta amchukua kwa taifa stars hatufai..Jamani si kuna SHIMIWI na pale ikulu wana timu yao inashiriki?basi aende huko
 
wapo ila wachovu kaseja ndio kinara wao,aitwe kaseja kama kweli ni national team,au la basi tuahache,Mziray yupo sawa kabisa na anachokisema,wakati ule wa team ya Mziray siye wachezaji tunajua tulikuwa hakuna kitu chochote cha ziada kwenye team ya taifa tofauti na sasa hivi,kama hujui mpira ndio utaongea kama Bongolander,kuanzia lini team ya ilikuwa inaenda nje ya nchi kwa ajili ya friend match?au inaweka kambi Brazil?au inakuwa na wazamini kama sasa hivi?Maximo keshafikia mwisho mtake msitake na hatufai tena kwakweli.

Middle sikuelewi unachosema, una maana hali ilikuwa nzuri wakati wa mzirai ambapo timu haikuwa na kitu, na hali ni mbaya wakati wakati wa Maximo wakati walau kuwa Timu ya taifa ni heshima.

Unataka kuniambia kuweka kambi Brazil ni vibaya, au unataka kuniambia kuwa hakuna sababu ya kuweka kambi Brazili.

Unaweza kuwa mchezaji mzuri, lakini huwezi kuniambia kuwa mtaalamu wa elimu ya viungo ni mzuri kuliko mtaalamu wa kufundisha soka. Sina maana kuwa Maximo ni kocha mzuri kabisa kuliko Kocha mwingine, lakini najua kabisa kuwa Maximo ni kocha mzuri kuliko Mzirai.

Mpaka sasa sijasikia kama maximo amemchukulia mchezjai mke wake. Soka sio kambumbu tu, ni nidhamu pia. Kama kocha anaweza kuleta harmony na respect kwa timu na wachezaji ni sehemu ya kazi yake. Huwezi kuacha timu ya Taifa iendeshwe kuhuni.

Kocha yoyote mwenye akili timamu au hata Kiongozi yoyote mwenye akili timamu angemfukuza golikipa ambaye anafurahia kuona nchi na timu yake inafungwa, eti kwa sababu anataka yeye apangwe.

Siwezi kukubaliana na maoni kuwa afukuzwe Maximo aletewe Mzirai. Inawezekana kabisa kuwa Maximo amefika ukomo, au wachezaji wamefika ukomo wa kufundishika. Kumleta Mzirai sio suluhisho.
 
Mazimo to me is not a coach.maana sijawai kuona CV yake na wapi kawahi kufundisha.ni sana tupu...huyo aliyemleta amchukua kwa taifa stars hatufai..Jamani si kuna SHIMIWI na pale ikulu wana timu yao inashiriki?basi aende huko

Mkuu kutoona CV yake siamni kama ni kigezo cha kuona yeye hafai. Kuna watu ni mawaziri na CV zao hatuzijui.
Sasa una suggest nani awe Kocha?
 
CV sio jambo la msingi kwetu kwani ukihitaji cv yake inapatikana na ni nzuri kwani alishawahi kuwa mwalimu wa timu ya Brazil under 17.Sisi tunachotaka alete matokeo mazuri.
 
Huyu muheshimiwa wetu katika level yake ya ubunge ana historia ya kushughulikia maendeleo ya michezo au kwa kuwa tumefungwa ndio kelele zinaanzia hapo. Siwezi kumsifia Maximo kwa chochote alicho ifanyia Taifa Stars lakini kweli tatizo letu la msingi ni kocha pekee.

Kwangu mimi hata Maximo akiondoka leo matatizo yatabaki palepale, chamsingi kama anaondoka leo tumejipanga vipi? Nafasi yake itachukuliwa na nani? TFF walishaambiwa waajiri kocha na aliyemleta Maximo, wanasubiri nini? Kwani mpaka Maximo aondoke ndipo walete kocha mwingine? Kwa leo tukubali hata TFF kuna pesa mno pale na ndio mwanzo wa matatizo. Kama sivyo kwanini wasilete kocha mwingine afanye kazi na Max ili tujue mbivu na mbichi?
 
Kosa la Maximo ni moja tu-Kutomuingiza Juma Kaseja kwenye timu ya Taifa. Hata washabiki wa ile klabu kubwa mtaa wa Jangwani wanalijua hili. Ubishi ndiyo unamponza!
 
WATANZANIA WA SASA hawana nidhamu ya soka, kwa uchezaji na tabia za wachezaji wa sasa hata akija kocha gani itakuwa hivyohivyo tu
ngoja timu apewe Mziray tuone
 
Mwalimu mzuri ni yule anayefaulisha wanafunzi...kwa mwalimu huyu wanafunzi kila siku wanafeli... eti bado tumpe muda, wa nini huo Muda? Hadi lini? lazima aondoke, atafutwe mwalimu mwingine. Kigezo kuwa hata kwenye Klabu hakuna mafanikio si cha msingi, ndo mana hata huko nako makocha huwa wanapendwa kwa mafanikio yao na si kwa sura zao.

kuna walimu wengi walianza na timu zetu kwenye ligi ya Vodacom, lakini wengi wao wameshatimuliwa, Kondik wa Yanga ni mmoja wao. sijui huyu Maximo wanamwogopea nini? Na tatizo haliko ikulu wanakomlipa ujira, tatizo lipo TFF, pale kuna wataalam (Kitengo cha ufundi) wale wangemwambia huyo mlipa ujira kuwa huyu mwalimu Maximo hafai, uwezo wake umegota, sidhani kama hao ikulu wangeendelea kumkumbatia. Kwanza siku hizi kuna joto, mambo ya kukumbatiana hayalipi kwikwikwi. Maximo aondoke!! Na Zanzibar watatufunga tu tukikutana nao.
 
Richmond, meremeta, ufisadi, deep green,... vimetushinda, jamani hata kumtoa Maximo tumeshindwa??????? Watanzania hususani wapenda socker tuamke!!!!

Maximo alishajiunga na ccm? maana watu watasemaaaaa na kuandikaaaa, lakini akirudi kutoka challenge ataongezewa mkataba ili ajenge timu mpya tena.
 
Back
Top Bottom