Chuji alimuambia Maximo aache mambo ya Chuji, kaseja na Boba sasa awaeleze Watanzania KWA NINI HADI SASA Nchi haina Kikosi cha kwanza katika Timu ya Taifa. Swali hili ni muhimu sana akalijibu. Enzi za wakina Zamoyoni Mogera, Athmani China, Malota Soma, n.k ukisikia Timu ya Taifa LAZIMA uwe na Kikosi chako tayari mkononi kwamba hawa ndiyo wacheza wa Kikosi cha kwanza. Nenda hata kwao na Maximo (Barazil) Timu yao ya Taifa inao wachezaji 11 wa kwanza, nenda hata kwa Timu za Mchangani mkiwa na mechi mnajijua kabisa kama hakuwepo fulani, fulani na fulani wa fulani Timu haijatimia. Sasa leo Maximo aliowapelekea Brazil sijuwi wamebaki wangapi ktk timu ya Taifa, alikwenda nao Denmark sijuwi kuwaaacha wapi? n.k n.k. Lakini Huo Mshahara na marupurupu anayopewa Maximo na familia yake angetafutwa Kocha kutoka Nchi yoyote ya Kiafrika ambayo soka lao lipo juu angeweza angaliu hadi sasa kuwa na Kikosi cha kwanza, hata kama kinafungwa LAZIMA UWE NA CHA KUONYESHA kwamba hii ndiyo 11 yangu pamoja na kwamba kila siku inafungwa.
Anachofanya Maximo na Biashara, pengine uwezo wa Ukocha hana matokeo yake akiambiwa kweli na Wachezaji wenye vipaji vyao (Kaseja, Chuji, Bobani, n.k) anawaeleza hawana nidhamu, WHAT IS THE DEFINITION OF NIDHAMU? sijuwi kama mnakumbuka kisa cha Zamoyoni Mogela, Hamisi Thobias (Gagarino), Athumani China walipomueleza Mhe. Naibu Waziri wa Michezo Mhe. Bendera wakati huo aliteuliwa kuwa kocha wa Mpira wa Timu ya Taifa. Walimueleza wewe siyo kocha wa Mpira wewe ni Kocha wa riadha, sasa wakati wa mazoezi ya kukimbia walikuwa wanaingia uwanjani kwani ndiyo taaluma ya Mhe. Bendera, lakini wakati wa kufundishwa namna ya kujipanga, kushambulia, kupiga chenga, kutoa pasi n.k wachezaji hao walimuambia hawawezi kufundishwa na yeye. Nadhani Maximo ni Kocha wa KUZUNGUMZA KIINGEREZA CHA KIBRAZIL.
Hebu tufike mahala tukumbuke msemo wa Hayati Mwl. Nyerere alipokuwa anawahutubia Wafanyakazi wa Tanzania wakati wa Kilele cha sikuu ya Wafanyakazi Mkoani Mbeya alisema
"Mtu akikushauri jambo la Kijinga na anajua kwamba analokushauri ni la kijinga na wewe ukailichukua na kulifanyia kazi ujue amekudharau sana."
Huyo Ndiyo Maximo anashindwa kutuonyesha matunda ya kazi yake, matokeo yake anatufanya tuelewe kwamba "NIDHAMU" kila siku "NIDHAMU" Ebu kama watu hawana nidhamu si aondoke.
HUYO NI MGANGA NJAA, MCHIMBA CHUMVI hana analolijua katika medani ya Soka.
Watanzania tufikie mahali tuseme ukweli. Hata ukitazama zile mechi ambazo TZA tumeshinda kiwango cha Mpira ni kibovu Kibovu ni kama mipira ianwagonga wachezaji wa Tanzania na kwenda mbele. Huoni kwamba sasa Timu inataka kufanya mashambulizi. Hivi nani anaikumbuka timu ya USHIRIKA MOSHI. Ulikuwa unasikia raha kuiona inapocheza. na Nataka kuwaambia Timu za Simba, Yanga na Mtibwa ni Timu nzuri na zinaonyesha kiwango cha soka kuliko hiyo TIMU YA MAXIMO NA TENGA WAKE.