Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

mkuu malaria sugu tafadhali weka makala yote ya mziray ili tuweze kuijadili vizuri.kwa kuanzia tu tayari naona mziray anachemka kwa kudhani taifa star imefanya vibaya kwasababu kaseja akuchaguliwa.

juma kaseja ni kipa mzuri lakini ufupi wake unachagia kwa kiasi kikubwa kuachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa.najua wako mashabiki wengi wa juma kaseja wanatumia vyombo vya habari kushinikiza aingizwe timu ya taifa,naomba kuwauliza ni timu gani kubwa dunia yenye kipa andunje kama juma kaseja ?.nitajieni walau makipa watatu tu !!!!.
omar mahadhi bin jabir alikuwa mfupi na akachaguliwa kuwa kipa bora wa africa.
 
Huyo Maximo hakutufaa tangu siku ya kwanza, tatizo tulivyosikia tuu kuwa anatokea Brazil basi tukajua ni kocha wa maana.
 
Arghhhhhhhhh....nime naanza kampeni za kumngoa huyu kimeo maximo...
1- asipewe audience yoyote na media za tanzania..tusiandike wala kutangaza chochote kuhusu timu ya taifa..kifupi kumpotezea tuuu
2- timu ikicheza tusiende uwanjani
3- timu ikifungwa hata pale q-bar na jackies tumpige mawe na makopo ya soda na maji ...mpaka aone hii nchi hatumtaki awe kocha wala kujihusisha na soka

anajifanya anataka nidhamu wakati yeye yeye hata tone la nidhamu hana....tushachoka sieeeee...uwanja mzuri timu mbovu kisa kocha kimeo...shiiiiiiiiit
 
Huyo Maximo hakutufaa tangu siku ya kwanza, tatizo tulivyosikia tuu kuwa anatokea Brazil basi tukajua ni kocha wa maana.

Hapa ndugu yangu umenena vyema...
huu jamaa mi nahisi kule Brazil alikuwa ni mchoma chapati.
Ila kwa kuwa watanzania wengi wenu ni wababaishaji mkaamini kuwa yule ni kocha wa ukweli, kumbe ni uharo mtupu...
Hakika huyu jamaa alitakiwa atimuliwe kipindi kirefu sana.
 
Ni kipndi kirefu sasa tangu kocha marcio maximo anaifundisha timu ya taifa ya tanzania.
Kwa mawazo yangu maendeleo ya timu ya taifa yaliyopatikana kwa uongozi wa kocha marcio maximo ni ya taratibu mno.
Tumeishi kwa matumaini kwa muda mrefu sasa.
Kufukuzwa kwa kocha scolary wa chelsea kumenikumbusha kuhusu kocha marcio maximo.
Kisha najiuliza, je ni kweli kwamba maendeleo ya timu ya taifa ya tanzania yanaridhisha kiasi cha kuona kwamba ni vema kocha maximo akaendelea kuvumiliwa?
Au kocha maximo anayo kinga ya kumzuia asifukuzwe kama scolary?

Marcio Maximo, a Brazilian, is the head coach of the Tanzania National Football Team. He will be responsible for the Taifa Stars.
His appointment by the Government of Tanzania follows a promise made by the President of Tanzania, Jakaya Kikwete to ensure improvement of football in the country.
He had previously coached Livingston Football Club in Scotland in 2003/2004. He was also a member of Brazil's youth coaching staff (under-17 and under-20) in 1992 and 1993.
His main task was to qualify the Taifa Stars for the 2008 African Nations Cup finals in Ghana for the first time in more than 25 years. However, he failed to reach that ambition but his recent focuses have been on qualifying for the 2010 World cup. Recently Maximo has meant a lot to Tanzania so as to improve football. Under his leadership, the ranking of the Tanzanian team has risen. Marcio Maximo has made Tanzania to qualify for CAN finals for home players. These final shall take place in Ivory cost from February 22 to March 8th, 2009. Tanzania qualified after beating Sudan 5-2 goal aggregate. Marcio Maximo did a lot to improve Tanzanian football. Brazilian coach, Marcio Maximo, has extended his contract with the Tanzania Football Federation (TFF) for another year until july 2010
Huyu sio Marcio Maximo, bali ni Masikio Makisio! We mtu gani asiyeshaurika huyu?! Na watu wa TFF nao kimyaaa, sijui kv aliletwa na mkulu?!
 
Pamoja na hasira tulizonazo za kuishuhudia timu yetu ikifungwa hatuna budi pia kutoa sifa kwa kocha timu inaposhinda. MAXIMO huyu aliipeleka Tanzania kwenye CHAN, pia aliiwezesha timu kuwa walau inapata matoeo ya kuridhisha against timu za west Africa e.g Ushindi dhidi ya Burkina Fasso, Draw against Cameroon, Ghana, Senegal.
Nafikiri tatizo letu sio MAximo, bali ni mfumo wa soka letu kwa ujumla. Tujiulize maximo anapata wapi wachezaji? Mostly ni Simba na Yanga; zitazame hizi timu kwa miaka mitatu nyuma niambie zimeshinda mashindano gani ya kimataifa au kuifunga timu gani bora hapa Afrika Mashariki na Kati?Kwa miaka miwili mfululizo ligi kuu Bara, mfungaji bora amekuwa ni mchezaji kutoka nje ya Tanzania (hatuna wachezaji wenye uwezo wa kufunga magoli??). Na sio kweli kuwa timu ya maximo inabadilika wachezaji wa timu ya Taifa stars ni wale wale , First eleven imepungukiwa na hawa wafuatao tu Kaseja(alionyesha upuuzi mwenyewe, hastahili mshamaha; huwezi kushangilia timu yako mwenyewe ikifungwa), Ivo Mapunda (kiwango kimepungua), Meck Maxime(kastaafu, kabadilishwa na Juma Jabu), Mwaikimba na Said Maulid (uwezo duni/Umri), Victor Costa(majeraha) na Deo Njohole (kiwango duni) Chuji, nidhamu mbovu(bangi). Hawa ndio walioondolewa ktk first eleven ya maximo na kuanza kuongeza chipukizi wafuatao, Juma Dihile, Jerry tegete, Mrisho Ngassa, Kiggi Makasi, Juma Jabu, nk Chipukizi hawa hatuwezi kubisha kuwa ni kati ya wachezaji bora kabisa waliopo katika ligi kuu ya Bara kwa sasa.

Bottomline is; tatizo liko kwetu tuliondoe, watakuja makocha wote bora tunaowajua hatutafika. Mliotazama michezo ya challenge; be honest na tuache ushabiki; magoli alitokosa MGOSI alaumiwe maximo?red cards za Kijinga hata kwenye mechi ya nusu fainali alaumiwe maximo?

I am just thinking aloud!
Haruna Moshi (Boban), Amir Mafuta je?..kwenye hiyo michuano inayoendelea kama angeongeza nguvu za Boban,Chuji na Kasenja si ajabu kesho tungecheza fainali
 
Tutaongea mengi sana lakini umefika wakati tufanye mamuzi.

Tumeshaona macoach mazuri sana wakitimuliwa bila haya huko ulaya
Hivi hatujifunzi kwa walioendelea? ingekuwa muda hajapewa kweli damn
4 years haitoshi kumjudge huyu mbrazil fake

Aondoke zake bwana..
 
Wabongo kwa longolongo bana Maximo mkataba wake haufi ng'oooooo hata mtoe chozi la damu. Mkataba wake utakufa wakati mmevunja mkataba wa Jakaya Kikwete. Amemuweka Hotelini tangu alipoingia Dar mtoni na ataendelea kukaa tu hapo hotelini. Nyie mlie tu.

Nendeni kufanya kazi nyingine mmeshupalia tu mambo ya Max!

Zitakapoanza kesi za ufujaji wa mali za umma hili lisisahaulike maana na huu pia ni ufisadi tena mkubwa
kwa muda wote huu bado yuko Hotelini?????
Mhhhhhhhhhh Mkulu nae hazionei huruma pesa za walala hoi tena katika zama hizi????????
 
Hapa ndugu yangu umenena vyema...
huu jamaa mi nahisi kule Brazil alikuwa ni mchoma chapati.
Ila kwa kuwa watanzania wengi wenu ni wababaishaji mkaamini kuwa yule ni kocha wa ukweli, kumbe ni uharo mtupu...
Hakika huyu jamaa alitakiwa atimuliwe kipindi kirefu sana.

Maximo alikimbia timu ya daraja la tatu uko Scotland, ila watanzania kwa pupa zetu tukamchukua haraka haraka, kashindwa kutupeleka fainali za chalenji ndio ataweza kutupeleka kwenye AFCON au World Cup?

Tuanzishe petition ya kuondolewa kwake.
 
Si tunasubiri atupeleke brazil tena,kocha gani mbishi??? Hataki ushauri lakini sasa mwisho wake umefika wala hakai,hata kwa babu tutaenda.
 
Haya AMANI na UTULIVU. Kidumu chama cha Mapinduzi. Zidumu fikira (SAHIHI) za mwenyekiti
 
Haya AMANI na UTULIVU. Kidumu chama cha Mapinduzi. Zidumu fikira (SAHIHI) za mwenyekiti


Duh! umenikumbusha Longi! mh wakati hata neno kauli mbiu halisikiki Mhhhhhhhh kweli ya zamani hiyo "zamadam" yaani haipo hiyo leo ni "Kilimo kwanza" tulikua na Mtaji wa masikini, halimpya na.......mpya tz bila.........inawezekana, nanyingine nyiiiiiiingi
 
Natumai hapo alipo anaomba afukuzwe ,anajuuuta kuwa kocha Tanganyika.
 
Conversation between a child and the Judge in court:

Judge: Do you want to live with your mother?

Child: No

Judge: Why?

Child: She beats me.

Judge: Okay, so you want to live with dad?

Child: No

Judge: Why not?

Child: He beats me too.

Judge: So who do you want to live with?

Child: Taifa Stars!!!

Judge: WHY??

Child: They never beat anyone!
 
Back
Top Bottom