Show ya Alikiba South Africa, iwe funzo kwa wasanii wa Bongo fleva

Show ya Alikiba South Africa, iwe funzo kwa wasanii wa Bongo fleva

Picha zilizowekwa ziko kishabiki sana, watu wamekatwa.

Inawezekana ikawa kweli pia ila ndio maisha yetu wa Tz nakumbuka Diamond wakati anakomaa kwenda nje ilikua kama ivi daily tunamnanga kua anaimba kwenye corridor ila dogo akaziba masikio ilimradi mkono unaenda kinywani leo kasogea hatua kadhaa,kuna thread umu inamnanga Diamond kua kazamia harusi ya dogo wa Psquare ila leo hadithi imebadilika kafanya nao joint na anakaa nao meza moja ukitaka ufanikiwe usiwasikilize maskini maana tunaopiga kelele hata boarder moja hatujawahi kuvusha miguu yetu hapa tunawaza 500 ya bundle duh njaa ya akili mbaya sana.
 
Ashawahi fanya show yake mwenyewe wapi nje ya EA ambayo aliweka rekodi ya kujaza uwanja ivi kama ambavyo wale Psquare wanatuburuzaga wakija Bongo,kwa hapa home Diamond hiyo rekodi anayo sanaaaa nakubali.
Mkuu umesahau ya zimbabwe na zambia,acha utani bana.
 
Mkuu umesahau ya zimbabwe na zambia,acha utani bana.

Alifanya One man show?unasahau kua ni kama Davido aje Bongo apokelewe na mwenyeji Diamond wafanye show najua unajua kitatokea nini,Zimbabwe show ilikua ya yule Dj ambae amefanya nae ngoma nipe miujiza mingine chief...alafu angalia umetaja show mbili tu na zote zipo around na sisi ingawa sio ndani ya EA nenda kaangalie wenzetu kama Wizkid na Davido wakiwa nje uko,tatizo ni mashabiki sisi hatujawahi kuwaunga mkono wasanii wetu ili wasanii zaidi ya kelele za kibwege tu wakati wenzetu wanawabeba wasanii wao.
 
Ali kiba ni msanii mzuri isipokua yeye ajiona bora sana na tabia zake za kibongo kutotaka au kukubali bado kiwango chake kidogo na hataki kujifunza.tofauti na diamond. Hili ni funzo kwake na akina baraka na wa aina hiyo after all hata kwa tungo zao bado ni chache sana
Kajiona anavyopokelewa kenya kifalme akajua basi ni ulimwengu wote! Kalamba dume, a tafute manager aggressive atamnyanyua. Na pia ache kujiona kafika
 
Hapa mtaongea mpaka asubuhi.... 1.uongozi mbovu 2.Kiba hataki kukubali uhalisia kwenye muziki ukishashuka ni ngumu sana kupanda tena 3.Kiba hajui umuhimu wa social media.4.Kumbeba kiba ni kupoteza muda wako bila yeye mwenyewe kuamua kubadilika huwezi kujifananisha na chui wakati kiuhalisia wewe ni swala...ushabiki pembeni show ya jana ilikuwa na watu wachache sana lakini si kitu cha ajabu wala chakushangaza ndio level yake ilipo kwa sasa cha msingi ajitume zaidi.
 
ali kiba anachochemsha tuu ni kujiona yuko juu wen hayuko hvo na also kutaka kumzidi diamond na kupambana nae kwa hali yyte ata kam mwenzake yuko mbali sna nae akijirekebisha hivo atafika mbali
 
Mnaolumbana hapa wengine ni kula kulala, wengine ni wafanyabiashara, wengine ni wafanyakazi wa mwisho wa mwezi mnaivuta weekend iishe mkatumike kwa waajiri wenu. Suala la msingi waswahili wanasema bora kupata kuliko kukosa kabisa. Je! Unamzidi kipato Alikiba? Una nyumba kama yeye? Una vitega uchumi kama yeye?
Nafikiri ni vema kushauri njia bora ya mtu kufanikiwa kuliko kumkatisha tamaa.
Ishu sio Mond au msanii mwingine yoyote lakini hebu fikiri uwezo wake Alikiba japo kidogo msanii kukaa likizo miaka 3 bila kutoa wimbo wowote na baada ya kuanza kuimba tena akafanikiwa kupenya kwenye soko la muziki na kutishia uwezo wa waliokuwepo!
Kwahiyo uwezo anao labda shida ni 'strategies' za kufika kimataifa ambazo anaweza pia kwasababu ni zakujifunza tu.
Likizo au game lilimkaba akaenda bench kidogo kupasha kutafuta strategies zingne za kuja nazo na kinachombeba kba kinajulikana basi tu watu tunajifanya vpofu
 
Angalia hapa show
Unapiga show huku watu wanaangalia Mpira
 
Alikiba ni msaniii wa kawaidaaaa sanaah ila wabongo ni wanafiki mashabiki wake wanampa bichwaaa bureeee tu kumbe hkuna chochotez cha msing akae chin ajitafakar af afanye nyimbo zenye hadh ya kimataifa
 
Daaa aisee! angeweka video ya show ingekuwa njema sana
 
Kuna kitu kinaitwa "Win Win Situation" ambacho Ali Kiba, Diamond na wabongo wote tunakihitaji sana, lakini anayehitaji zaidi (Kama anataka kupanda juu) ni Ali Kiba timu yake. Win Win Situation inawanufaisha wote mlio katika mvutano. Ali Kiba anamuhitaji zaidi Diamond kuliko Diamond anavyomuhitaji Ali Kiba, tatizo ni upeo wa kuona mambo kwa mapana na marefu na kukosa washauri sahihi.

Sisi kama wabongo kwa mmoja wetu hasa wale wenye ushawishi na walio na hawa wawili, tunapaswa tuombe ili huu uhasama utokomee, na siku moja tuwaone wasanii hawa wakishirikiana pamoja wakifanya kazi za kolabo ndani na nje ya Bongo, na hatimaye kuleta heshima kwa nchi, wao wenyewe na wafuasi wao
 
Back
Top Bottom