Wewe jamaa bana, mimi nakuletea makubaliano ya marais, ya mwaka wa 2017 kuhusu CONFEDERATION ya nchi za EAC. Wakati JPM alikuwa ndiye rais na wewe unaniletea video ya Kikwete akiongea kuhusu federation na sio confedaration. Hivyo ni vitu viwili tofauti. Nimeshakueleza yote kwenye post yangu iliyotangulia hii hapa. M7 pekee yake ndiye aliyekuwa anataka political federation, nadhani alikuwa na matumaini ya kuwa rais wa kwanza wa EAC. Kenya, Tz, Rwanda na Burundi wote walikataa. Alafu mimi pia sijaunga mkono hoja ya muungano wa kisiasa wa aina yeyote ile, iwe federation au confederation. Wakenya tulipofika sasa hivi kikatiba, kisiasa na kidemokrasia hatuna lolote la kufaidi kutoka kwa nchi yeyote nyingine ukanda huu. Nyinyi wote mnaongozwa kidekteta na kiubabaishaji wakati sisi tulishatoka huko zamani, tena kwa jasho na damu na hatuna hamu kabisa ya kurudi nyuma.