Ninavyojua mimi kwenye misiba huwa kuna utani kati ya watani ambayo inasaidia kupunguza uchungu na kubadili hali ya hewa kwa muda kwa kuwaondoa wafiwa kwenye tension ya msiba walau kwa dakika chache, bila kumvunjia marehemu heshma au kuleta taharuki
Lakini leo nimekutana na hii clip nikabaki na mshangao. Nimejiuliza kweli hii ndio style ya ku celebrate maisha ya aliyetangulia?
Huyu marehemu yawezekana akawa mzazi wa mtu, mtoto wa mtu, mume au mke wa mtu. Hivi watu wake wa karibu wanalichukuliaje?
Wengi wetu tuna imani zetu zinazotufundisha heshma na tararibu za kumhifadhi marehemu, maiti, taratibu za maziko, utunzwaji wa makaburi na mambo mengine yahusuyo.
Kwa hili lililotokea hapa sijui viongozi wa kiimani wanasemaje ila kwakweli ipo haja ya kujifunza na kuwafundisha vijana wetu mambo mengi ya kiimani na kijamii
Your browser is not able to display this video.
Mimi ninachojua ni kwamba watu huyazuru makaburi kufanya kumbukumbu ya wapendwa wao wakiwa na imani kwamba wanawapenda na wanawatendea wema kwa kuheshimisha hata pale walipohifadhiwa
Uislam
Niliwahi kuambiwa na babu yangu kwamba Kwenye uislam tunayazuru makaburi ili yatukumbushe akhera kwamba ipo siku tutalala
Ukristo
Hesabu 19 16
Mtu yeyote akigusa mwili wa mtu aliyeuawa au aliyekufa kifo cha kawaida nje ya nyumba, au akigusa mfupa wa mtu au kaburi, atakuwa najisi kwa siku saba.
Sijui hiki kilichofanyika hapa ni matokeo ya ushamba, ujinga, ukafiri au ni nini. Huyu marehemu sijui ni wa jamii gani
Watanzania bhna..yani wanataka tuishi kwa kufanana kama mapacha..mtu akitenda tofauti anaonekana wa ajabu..kila mtu aishi maisha yake..mnaua uwezo wa kufikiri tofauti.
Hivi vifungu manavitumia sana kujitetea mtatafuta kokote viliko hata agano la kale..ila likija suala la kula kitimoto na bia..agano la kale mnalikataa na kuliona halifai..bure wa hedi ninyi.
Watanzania bhna..yani wanataka tuishi kwa kufanana kama mapacha..mtu akitenda tofauti anaonekana wa ajabu..kila mtu aishi maisha yake..mnaua uwezo wa kufikiri tofauti.
Hakuna jipya chini ya jua..yote anayoyatenda mwanadamu yalishatendeka ni marudio tu..kizazi kinazaliwa kizazi kinakufa..yote ni ubatili mtupu na kujilisha upepo.
Watanzania bhna..yani wanataka tuishi kwa kufanana kama mapacha..mtu akitenda tofauti anaonekana wa ajabu..kila mtu aishi maisha yake..mnaua uwezo wa kufikiri tofauti.