Shughuli za Misiba, Maziko na Maombolezo zimeanza kupoteza maadili ya asili na imani zetu, Utu na Ubinadamu katika jamii

Shughuli za Misiba, Maziko na Maombolezo zimeanza kupoteza maadili ya asili na imani zetu, Utu na Ubinadamu katika jamii

Nyakati Za Mwisho Maarifa Yataongezeka. Ndio Kama Hayo
 
Kwanza kabisa hakuna mtu kapiga marufuku. Tumehoji uhalali wa hicho kitendo kulingana na maadili yetu sisi wanajamii wa kitanzania.

Hivyo vitu umelist havina uhusiano na tukio hili la kustaajabisha.
Linastaajabisha kwako...ukienda mkoani huko ni kawaida..kwenye maziko kuna pombe na misos kama yote
 
Linastaajabisha kwako...ukienda mkoani huko ni kawaida..kwenye maziko kuna pombe na misos kama yote

Ni kawaida meza ya Pombe na misosi kuwa kaburi? Mikoa ipi mfano

Najua misiba mingi ina kula na kunywa
 
Kabisa.... Huku ni kukosa adabu na ni ibada za giza kabisa. Mtu mwenye akili timamu hawezi kula chakula na kufanya hafla ya Chakula juu ya makaburi.
Usikimbilie kuhumu , je? Kama dini yake ndiyo yenye kumruhusu hivyo?
 
Ni kawaida meza ya Pombe na misosi kuwa kaburi? Mikoa ipi mfano

Najua misiba mingi ina kula na kunywa
Huyo mtu alishazikwa kitambo hapo wanamkumbuka..its like celebrating tho ni weird in a way..maana nmewaza kama mi mtu wako wa karib mzaz or wateva huwez kua na guts hzo..mtu bak anaweza fanya hvo ila si watoto wake au mkewe..unless sjui iweje
 
Huu utamaduni wa kupangia Watu namna ya kuishi ikiwa hawavunji sheria za nchi ni upumbavu mkubwa.
Wakikuambia kwamba walikuwa wakinywa na kula na marehemu Labda msimu wa Sikukuu hivyo Kwa tamaduni zao hapo wamempa heshima ya kushiriki nao kula Siku kuu utakataa?

Wewe fanya kinachokupendeza wewe achia wengine wafanye yao, bia zao, chakula chao,marehemu wao, wewe Unawashwa washwa nini.
 
Huyo mtu alishazikwa kitambo hapo wanamkumbuka..its like celebrating tho ni weird in a way..maana nmewaza kama mi mtu wako wa karib mzaz or wateva huwez kua na guts hzo..mtu bak anaweza fanya hvo ila si watoto wake au mkewe..unless sjui iweje
Wewe kwa kuangalia unaona hao ni Watu baki Hawana ukaribu na marehemu? Kwao ni kawaida maana ni utamaduni wao
 
Ninavyojua mimi kwenye misiba huwa kuna utani kati ya watani ambayo inasaidia kupunguza uchungu na kubadili hali ya hewa kwa muda kwa kuwaondoa wafiwa kwenye tension ya msiba walau kwa dakika chache, bila kumvunjia marehemu heshma au kuleta taharuki

Lakini leo nimekutana na hii clip nikabaki na mshangao. Nimejiuliza kweli hii ndio style ya ku celebrate maisha ya aliyetangulia?

Huyu marehemu yawezekana akawa mzazi wa mtu, mtoto wa mtu, mume au mke wa mtu. Hivi watu wake wa karibu wanalichukuliaje?

Wengi wetu tuna imani zetu zinazotufundisha heshma na tararibu za kumhifadhi marehemu, maiti, taratibu za maziko, utunzwaji wa makaburi na mambo mengine yahusuyo.

Kwa hili lililotokea hapa sijui viongozi wa kiimani wanasemaje ila kwakweli ipo haja ya kujifunza na kuwafundisha vijana wetu mambo mengi ya kiimani na kijamii

View attachment 1888648


Mimi ninachojua ni kwamba watu huyazuru makaburi kufanya kumbukumbu ya wapendwa wao wakiwa na imani kwamba wanawapenda na wanawatendea wema kwa kuheshimisha hata pale walipohifadhiwa

Uislam​

Niliwahi kuambiwa na babu yangu kwamba Kwenye uislam tunayazuru makaburi ili yatukumbushe akhera kwamba ipo siku tutalala

Ukristo​

Hesabu 19 16
Mtu yeyote akigusa mwili wa mtu aliyeuawa au aliyekufa kifo cha kawaida nje ya nyumba, au akigusa mfupa wa mtu au kaburi, atakuwa najisi kwa siku saba.

Sijui hiki kilichofanyika hapa ni matokeo ya ushamba, ujinga, ukafiri au ni nini. Huyu marehemu sijui ni wa jamii gani
Unafahamu mila za maziko za kijaluo???
full dance na vinywaji vikali
 
Hii jamii itakua haina wakubwa!! Ni wahuni tuu
Kwanza Mungu aipumzishe roho ya huyo marehemu simon kama sijakosea ,pili yawezekana huyo alikua mgonjwa na hakuna aliyekwenda kumtizama wala kujua hali yake ila baada ya kifo wameamua kufanya karamu ambayo ni haramu maana haimsaidii chochote marehemu zaidi ya ufahari kwa wafu wa baadae ,tatu Niliwahi kusema wakati fulani kwamba social media ni janga kubwa baada ya covid19 ,ila kwa sasa yaweza ikashika hata nambari moja ,simu hizi zimeleta mengi ambayo yametuingiza katika kuishi maisha ya ubatili yasiyo na uhalisia,tumezoea kifo bila kuelewa juu ya fumbo hili ,psychologically maisha binafsi ya mtu ni usiri ila kwa sasa ukitaka kumjua mtu mtafute katika social media utamjua A-Z maana kiuhalisia binadamu anasahau ila technology haiwezi kusahau tuwe makini turudi katika asili yetu
 
Hapo kuna mambo mawili.

1. Aliyekufa ni dogo ambaye picha yake ipo hapo pembeni na hajazikwa hapo nyumbani. Yeye kazikwa huko makaburini, hapo ni nyumbani.

2. Hilo kaburi ni la baba yao lipo hapo nyumbani, alizaliwa 1947 akafariki 2019 na hao ni watoto wake.

Ushauri: Tusipende kuongea sana kwa mambo yasiyotuhusu. Hao ni watu wazima wenye akili timamu, wanajifariji kwa misiba waliyopitia.
Tuwape pole ila tusiwahukumu. Hayo ni mambo yao binafsi.
 
Kabisa.... Huku ni kukosa adabu na ni ibada za giza kabisa. Mtu mwenye akili timamu hawezi kula chakula na kufanya hafla ya Chakula juu ya makaburi.
Waacheni watu waishi maisha yao tusipangiane mnajikuta ibado ya giza mmezijuaje kama sio nyie ni wagiza
 
Let people live.....

Maisha yamekua magumu

Tukiweka makatazo kila kona nchi inakua haina ladha

Mara huku unaskia madada poa waamezuiwa
Mara baa mwisho sa sita
Mara wanawake wasivae nguo fup

Makatazo meng yasiyo na msing

Yabak makatazo yenye msing tu

Kama marufuk ya ushoga
Na imoralities nyingne

Mengne yaachwe ..watu wanamaisha magum sana.
Mara usifumanie bila cheti cha ndoa
 
Back
Top Bottom