Shuhuda adai Hayati Ali Kibao wa CHADEMA alipigwa kichwani na kutobolewa macho

Shuhuda adai Hayati Ali Kibao wa CHADEMA alipigwa kichwani na kutobolewa macho

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Msikilizeni huyo shuhuda.

Anadai Mzee Ally Kibao aliumizwa vibaya kichwani, na alitobolewa macho.

"Nilikuwa na abira wangu sasa wakati napita nilikuta watu wengi sasa hapa ilibidi nipaki nilikuja kuaangalia tulikuta mtu amakekufa, kapigwa kichwani, amevia damu, amaetobolewa macho unaona. Kwahiyo hile tafurani wengi wanalia wengine wanalalamika kwa sababu hili eneo kusema ukweli wangetuimarishia ulinzi, hili eneo sio mara ya kwanza mara nyingi na imeshakuwa kama dampo la kutupa watu. Shuhuda ameeleza"

"Kwa upande wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ununio Mwinijuma Shee amesema bwana mkubwa huu alitupwa siku ya tarehe 7 mwezi huu wa tisa nazani kati ya usiku mkubwa au alfajiri kwa sababu nilikuwa safarini mwenge nilipigiwa simu na mwananchi kwamba huku kuna marehemu au maiti."

"Sikuweza kurudi lakini na vijana wangu wanaweza kufuatilia masuala hayo kikubwa nikawapiga simu vijana wa polisi jamii na kuelekeza tukio lilipo na bahati nzuri wakaenda hapo wakashuhudia huyo walimkuta hawakumjuwa kwa jina wala kwa sura kuweza kumtambua kama moja ya mwananchi wetu. Lakini bahati nzuri Jeshi la Polisi nalo lilikuwa limeshafika kwahiyo Jeshi la Polisi wakaendelea kufanya kazi yao"

Mzee wa watu alipitia mateso makubwa sana.

Wahusika wanapaswa kushtakiwa.

Soma Pia:
 
..msikilizeni huyo shuhuda.

..anadai Mzee Ally Kibao aliumizwa vibaya kichwani, na alitobolewa macho.

..Mzee wa watu alipitia mateso makubwa sana.

..wahusika wa Task Force wanapaswa kushtakiwa.

View: https://m.youtube.com/watch?v=-85pFwuVncs

Kwanza kabisa, kama ambavyo Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu alivyosema kila mtu amehuzunishwa. Tusubiri uchunguzi. Pili, nakataa kunyooshea kidole mamlaka za dola kwa sababu ya baadhi ya matukio ya hivi karibuni.

Kuna watu walipotea kumbe walikuwq kwa waganga Singida. Wengine matatizo ya ndoa na wengine chuki za biashara na kifamilia na mapenzi kama yule dada kada wa CCM aliyekatwa katwa kama mbuzi na jamaa wake wa Sinza. Simaanishi na hili la Mtanzania mwenzetu mzee Kibao ni la aina hiyo kwani uchunguzi bado; ila nahofu tukinyooshea kidole polisi au mamlaka nyingine basi magenge ya kihalifu yanaweza kutumia mwanya huo kutimjza dhamira ovu. Tusimame pamoja na mamlaka za dola kusaidiana kujua tatizo tuendelee kuishi kwa amani.🙏🙏🙏
 
Nasikitika kusema "HUNA AKILI".
 
Back
Top Bottom