Shuhuda za waliofanikiwa kupunguza uzito kwa mazoezi na lishe

Shuhuda za waliofanikiwa kupunguza uzito kwa mazoezi na lishe

Hakika mimi ni mmoja ya wanaoshuhudia kwamba mazoezi na kujidhibiti kwenye chakula kunasaidia sana kupunguza uzito.

Mimi nimefanikiwa kupunguza uzito kutoka 92kg mpaka 71kg kwa kukimbia na kujizuia na ulaji wa hovyo.
Jitihada za kupunguza uzito wa mwili zimenifanya kuwa mpenda mazoezi na sasa mazoezi ni sehemu ya maisha yangu.

Cha muhimu kwa wadau ni kwamba vyote mazoezi na kujidhibiti na ulaji wa hovyo vinahitaji nidhamu ya hali ya juu na kujitoa sana lakini ni jambo linalowezekana ukiamua.
 
Tatizo sio kila mtu ni mtu wa mazoezi....mie kukimbia sipendi na huwa sikimbii,kutembea umbali mrefu ndio nilishashindwa
Kiufupi siwezi mazoezi

Nafikiri watu wanene wazingatie vyakula,japo kuna wale wanene wa kurithi

Hata kama sio wa mazoez jitahid ufanye kama una jali afya yako, jilazimishe.

Sawa sawa una umwa alafu hunywi dawa,

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
bisharo,
Wengi wanaotaka kupunguza mwili kwa kutumia lishe ni wavivu wa mazoezi,chunguza hiyo kitu.Na ni wachache sana wanaofanikiwa kupunguza uzito kwa njia hii,wengi wao huwa wanapungua kidogo kisha wanarudi palepale,utawasikia wanasema yaani mwili wangu umegoma kabisa.

Mazoezi ya kila siku kutembea kwa kasi kwa dkk 45,yanatosha sana,ukiweza kukimbia ni much better,kula usiache ila tu usile vitu vinavyoongeza mafuta mwilini,ukizingatia hayo ndani ya mwezi mmoja utakuja na shuhuda ya kupungua kilo kadhaa.

Tabia nyingine ya hovyo kabisa ni matumizi ya gari kila unapokwenda,lipe likzo hilo gari lako utapata matokeo mazuri,pia siku hizi bodaboda nazo ni shida hakuna tena wanaotembea umbali mrefu...
 
Ili kupungua uzito inatakiwa uwe na commitment ya hali ya juu kwenye upande wa mazoezi na lishe. Binafsi huwa nafanya mazoezi na kufuata lishe kwa kuacha sukari na wanga. Huwa napungua sana uzito lakini nikiacha hayo uzito unarudi pale pale. [emoji28]

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
nina kilo 57 mwili wa kawaida urefu 5'5 shida kakitumbo ka chini hakatoki natamani flat, mazoezi huwa naruka kamba kiasi na kutembea.
 
nilianza mazoezi nilinenepa kweli nmeacha mwili wangu umerudi
 
Ili kupungua uzito inatakiwa uwe na commitment ya hali ya juu kwenye upande wa mazoezi na lishe. Binafsi huwa nafanya mazoezi na kufuata lishe kwa kuacha sukari na wanga. Huwa napungua sana uzito lakini nikiacha hayo uzito unarudi pale pale. [emoji28]

Sent from my iPhone using JamiiForums
Asante
 
ingekuwa vema mkuu ungetuambia na aina ya vyakula au ratiba yako ya kula

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom