Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,210
<br />
<br />
Mkuu, kwan hukum ndio inatoa jibu sahii la nani ni mkosaji au si mkosaji? Ni wangap wanafanya makosa kweli lakin wanasalimika? Au ni wangapi wanakuwa hawana hatia lakini mwisho wa siku wanaozea jela? Wewe umesoma hukumu, ila mimi nimehudhuria kesi!
Katika baadhi ya shahid zao, mzee Nguza alisema kuwa ile bendi yake ya ACHIGO ilikuwa ikifanyia mazoezi nyumban kwake(hata mm mwenyewe nimewai kuishuhudia hiyo bendi ikifanya mazoezi sehem hiyo) na akawaita wenzake(bendi) ila cha ajabu ushahidi wao haukuzingatiwa! Pia kwa tarehe ambazo zilitajwa kwamba watuhumiwa ndo walitenda kosa, katika baadhi ya hizo tarehe Papii Kocha Mtoto wa Mfalme alikuwa ziarani sehemu za mikoa ya kaskazin ukiwemo arusha pamoja na lady jay dee! Pamoja na lLady jay dee kufika mahakamani na diary yake kuonesha jinsi ratiba ya ziara yao ilivyokuwa bado huo ushahidi ulipuuziwa!
kama vile haitoshi, moja ya shahidi za upande wa walalamikaji ni kwamba mtoto mmoja kati ya wale alisema kuwa aliona wadudu weupe wakirukaruka kutoka kwenye uume wa babu seya! Swali; je, shahawa za mwanaume ni mfano wa wadudu wanaorukaruka?
yaan nina fact kibao za kukufanya uone hii hukumu haikuwa ya haki! Mko sawa wazee niendelee?
Kilichopo hapa ni kwamba amewekwa gerezani, kama wewe unatafuta haki jaribu uone kilicho ndani ya kesi yake. Kosa la nguza linafahamika, jaribu kutumia muda wako ujue ni kwanini amewekwa ndani , na ni kwanini hatatolewa kwa msamaha wa mwaka mpya au wowote ule. At least for now. Ukumbuke kuwa Tanzania si nchi ya haki, nguza si wa kwanza. At least yeye yuko gerezani. Kuna wale waliopigwa risasi pale Sinza bila hatia, no body cares and life goes on.