Uchaguzi 2020 Shukrani za dhati kwa wote walioshiriki kusambaza taarifa za Kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu tangu mwanzo hadi mwisho

Uchaguzi 2020 Shukrani za dhati kwa wote walioshiriki kusambaza taarifa za Kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu tangu mwanzo hadi mwisho

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Wakuu, poleni sana na Majukumu yenu ya kila siku, Naomba kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote mliochangia kusambaza taarifa zote za uchaguzi za Chadema ikiwa ni pamoja na kusambaza kampeni kali za kiwango cha juu za Tundu Lissu Mgombea Urais wa Chadema, ambaye anatajwa kama Mgombea bora kabisa wa Urais kuwahi kutokea barani Africa tangu kuumbwa kwa Mbingu na Ardhi.

Wahenga walisema tangu awali kwamba kidole kimoja hakivunji chawa, bila mshikamano wa wadau wote nyinyi kampeni za Tundu Lissu zisingefikia mafanikio ya 96% ambayo ilifika tangu juzi, Kwa niaba ya Chadema na kwa niaba ya Lissu Mwenyewe nachukua nafasi hii bila kuwataarifu kushukuru kila mdau aliyejitolea fedha, muda, nguvu na bando lake ili kusambaza taarifa za kampeni za Lissu, ni imani yangu kwamba Mungu Mwenyezi atawalipa kwa kazi hii iliyotukuka.

Natambua mchango wa kila mmoja na nauheshimu sana, lakini Kipekee naomba kuwashukuru wafuatao kwa niaba ya wengi, JAMIIFORUMS pamoja na Moderator kwa masahihisho na miongozo, Mungu awalinde watu hawa na mabaya yote katika kipindi walichosaliwa nacho hapa duniani, Shukrani zingine ziende kwa CHADEMA Makao Makuu.

Si rahisi kushukuru watu wote kwenye andiko hili, bali shukrani zetu zimfikie kila mmoja aliyesambaza kampeni za Lissu popote alipo , mmefanya kazi ya kutukuka mno! Nina hakika Mungu atawalipa bila shaka.

Mungu ibariki JF, Mungu ibariki CHADEMA, Mungu mbariki Rais Mpya Tundu Lissu.

Chagua Chadema Chagua Tundu Lissu  Chagua wabunge wengi wa Chadema.   Chagua Mad ( 640 X 640 ).jpg
 
Mkuu, kwa kipekee sana na wewe umejitoa sana kutuhabarisha kila siku na tena pasipo kuchoka habari za kampeni za CHADEMA haswa mgombea wa nafasi ya uraisi TAL ktk kipindi chote cha kampeni za uchaguzi wa mwaka huu. Kongole nyingi sana zije kwako.
 
Yaaa moderators ni lazima muwashukuru kwa kweli, kwa maana wamejitahidi sana kusema ukweli, Mungu awabariki sana kwa kumlinda Tundu kwa hali na mali, BTW yuko wapi Tundu, atakuja Dar kumalizia Kampeni kama mlivyosema hapo mwanzo?
 
Tia sheria bila shuruti, utangolewa jino
Msaliti wa nchi na wananchi ni huyu aliyeamrisha majeshi yaue watu Zanzibar. Tayari tumeshapeleka ushahidi kunakohusika jiandae kwenda nae ICC muda si mrefu
 
Wakuu, poleni sana na Majukumu yenu ya kila siku, Naomba kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote mliochangia kusambaza taarifa zote za uchaguzi za Chadema ikiwa ni pamoja na kusambaza kampeni kali za kiwango cha juu za Tundu Lissu Mgombea Urais wa Chadema, ambaye anatajwa kama Mgombea bora kabisa wa Urais kuwahi kutokea barani Africa tangu kuumbwa kwa Mbingu na Ardhi...
Mtapata kura laki mbili?
 
Back
Top Bottom