Shukrani za Jamal Emil Malinzi kwa wana JF

Shukrani za Jamal Emil Malinzi kwa wana JF

Hongera mkuu, pamoja sana. Tunategemea utuwekee your priority interventions kufufua hili soka la Tanzania. Tuko tayari kukupa mawazo ya kimabadiliko.
 
Michezo ya UMISETA ilisaidia sana katika kukuza viwango vya uchezaji nchini na pia vilitoa wachezaji wengi sana ambao baadaye walikuwa nyota katika timu zao hata timu ya Taifa. Hii michezo iimarishwe ili kuwezesha kupata wachezaji wa Kitanzania. Hili la kuruhusu wacheza wa kigeni nchini mimi siafikiani nalo maana linaziba nafasi za Watanzania katika hizo teams ambao wangeweza kuzitumia nafasi hizo katika kuongeza vipaji vyao. Hili liangaliwe kwa karibu na ikiwezekana lisiruhusiwe.
 
Mission, vision na objective, long term and short term???

Labda anataka kujua watz kipaumbele kwao ni kipi zaidi. At the same time, kabla hajaja na sred hiyo, ni bora kujua kwanza aliyekuepo alikuwa anafanya nini na vipaumbele vilivyokuwepo ni vipi. Labda kuna miradi ilikuwa, iko kwenye hatua gani? Na kama gharama ya kubadili vipaumbele ni kiasi gani?

Kuomba maoni si kitu rahisi hivyo, lazima ujiridhishe kama kweli unahitaji aoni hayo kwa wakti huo, vinginevyo mwisho wa siku, tulinganisha utendaji wake na maoni tuliyotoa.

Hivi federation mpaka inaanzishwa kazi zake ni zipi????!!!!!!

Why vipaumbele tuweke sisi na Rais??!!!!!!

Ufafanuzi please
 
Mkuu Jamal Malinzi, kwanza nakupongeza sana kwa ushindi wako. Pili na-declaree interest kwamba mie ni Yanga hadi kufa. Kipindi ukiongoza Klabu yetu ulikuwa wa kawaida sana hata ulipoanza mbio za u'-tenga' nilikuona kama kenge kwenye msafara wa mamba! Hata hivyo unao uwezo wa kufanya mabadiliko, shirikiana na wenzako, usiwe na makundi, utafanikiwa Inshaallah, amen.
 
Last edited by a moderator:
NAKUPONGEZA SANA KWA USHINDI ULIOPATA. BILA SHAKA UTALIONGOZA VEMA JAHAZI LETU LA TFF. NA KUFANIKIWA KUTOA HUU UKIRITIMBA ULIOPO HAPO TFF.
Mfano; MAPATO YA MILANGONI HAYAGAWANYWI KWA USAWIA HATA KIDOGO, IWEJE KATIKA KILA MECHI MARA KUNA MGAO WA MATENGENEZO YA UWANJA?! HATA KAMA MECHI ZENYEWE ZIMEPISHANA SIKU 1, KAMA LEO HII MECHI YA SIMBA Vs AZAM, NA YA KESHO YA YANGA Vs MGAMBO.
NA MIGAWO YA WACHINA INABIDI ILEKEBISHWE, YAANI HAINIINGII KICHWANI HATA KIDOGO GAWIO LA O LINAKUWA KUBWA KULIKO WANALOPATA TIMU HUSIKA. NA GAWIO LENYEWE LITOLEWE UFAFANUZI NI LA KAZI GANI, AU BADO WANAENDELEAGA NA UJENZI?!!

PIA NA VIWANJA VYA MIKOANI UKU VIANGALIWE UBORA WAKE, NI VIBOVU SANA, MI NAONA KILA MUDA JINSI UNAVYOENDA NDO KADRI VINAVYODHIDI KUWA VIBOVU, MFANO HUU UWANJA WA MKOANI ARUSHA KWA SASA NI MBOVU KULIKO HATA WAKATI WA KIPINDI KILE AFC IKIWA BADO IKO LIGI KUU.

HALAFU KITU KINGINE HIVI INAKUWAJE HADI MECHI INAYOCHEZWA HAPA UWANJA WA ARUSHA KIINGILIO CHA CHINI KINAKUWA Tshs. 5000, JAMBO LINALOPELEKEA MTU MWENYE UWEZO WA CHINI KUSHINDWA KUGHARAMIA, KWANINI VIINGILIO VYAKE VYA CHINI VISIWE 2000 - 3000, KAMA MIKOA MINGINE?!!!
 
Mission, vision na objective, long term and short term???

Labda anataka kujua watz kipaumbele kwao ni kipi zaidi. At the same time, kabla hajaja na sred hiyo, ni bora kujua kwanza aliyekuepo alikuwa anafanya nini na vipaumbele vilivyokuwepo ni vipi. Labda kuna miradi ilikuwa, iko kwenye hatua gani? Na kama gharama ya kubadili vipaumbele ni kiasi gani?

Kuomba maoni si kitu rahisi hivyo, lazima ujiridhishe kama kweli unahitaji aoni hayo kwa wakti huo, vinginevyo mwisho wa siku, tulinganisha utendaji wake na maoni tuliyotoa.

I dont buy the idea ya mtu kugombea na.kushinda position kubwa kwa nchi halafu yeye kabla hajakaa ofisini anauliza wadau wanataka nini!!!

Mathalani wengi waseme hatutaki timu ya taifa ya football na badala yake tuanzishe timu ya taifa ya sumo yeye anakaa upande upi wa mzani???!!!

Habu aende ofisini atuletee work plan na time schedule tutaweka michango!!!!

Wapemba wanasema nyongeza huwekwa juu ya fungu!!!!!
 
ndugu zangu nashukuru uchaguzi tumemaliza salama na mimi nimeshinda. Nichukue fursa hii kuwashukuru wapenzi na wadau wote wa mpira miguu ambao kwa namna moja au nyingine wameshiriki kwenye mchakato.
Siku chache zijazo nitafungua thread hapa nikiomba maoni na mapendekezo yenu kuhusu ni jinsi gani tutaimarisha timu yetu ya taifa kwa ajili ya afcon qualifiers novemba mwaka ujao.tafadhali jiandae kuchangia.
Malinzi
hongera sana mkuu
 
I dont buy the idea ya mtu kugombea na.kushinda position kubwa kwa nchi halafu yeye kabla hajakaa ofisini anauliza wadau wanataka nini!!!

Mathalani wengi waseme hatutaki timu ya taifa ya football na badala yake tuanzishe timu ya taifa ya sumo yeye anakaa upande upi wa mzani???!!!

Habu aende ofisini atuletee work plan na time schedule tutaweka michango!!!!

Wapemba wanasema nyongeza huwekwa juu ya fungu!!!!!

...na wote tuseme AMINA!!!
 
Hongera Jamal Malinzi na tunasubiri kwanza huo uzi wako tujue tunajipangaje na tunaomba vile vile uwe unatembelea humu mara kwa mara kutupa mrejesho wa yale utakayoulizwa
naunganga na gfsonwin katika kusubiri utupe mikakati uliyo nayo haswa kwa vilabu vyetu na timu ya taifa tuache kuwa wasindikizaji kila mashindano na tuone tunavuka kwenda hatua za fainali tuache kuishia huku chini kila mashindano

kweli kabisa mdau tumechoka kuwa wasindikizaji tunataka kuondokana na hali hii miaka nenda miaka rudi
 
kweli kabisa mdau tumechoka kuwa wasindikizaji tunataka kuondokana na hali hii miaka nenda miaka rudi

Kabisa Blaki Womani na atengeneze team ya viongozi wenye malengo na wenye nia haswa ya kuona taifa linasonga mbele kwenye mashindano yanayohusu vilabu na timu ya taifa.
Tusiendelee kuwa kichwa cha mwenzawazimu kila timu inakuja ikiwa na mategemeo ya kutufunga na kuchukua point tatu au moja
 
Last edited by a moderator:
uzi wa ushaur kuhusu tutafikaje afcon aufungue mapema
 
Sio mshabiki lakini nionavo Michael Wambura ni moja wa watu muhimu katika kuendeleza soka letu. Huyu awe katika moja wa kamati za TFF itakayomfaa.
 
Kila la kheri.

Kilio changu:

Naomba uwadhibiti walanguzi wa ticketi hasa katika mechi kubwa (mfano Yanga na Simba). Tiketi za sh. 5000/= watu tunalanguliwa hadi sh. 20000/=. Bila shaka hili unalijua vema Jamal Malinzi.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu nashukuru uchaguzi tumemaliza salama na mimi nimeshinda. Nichukue fursa hii kuwashukuru wapenzi na wadau wote wa mpira miguu ambao kwa namna moja au nyingine wameshiriki kwenye mchakato.

Siku chache zijazo nitafungua thread hapa nikiomba maoni na mapendekezo yenu kuhusu ni jinsi gani tutaimarisha timu yetu ya Taifa kwa ajili ya AFCON qualifiers Novemba mwaka ujao.

Tafadhali jiandae kuchangia.

Malinzi

hongera.
lakini ukianza mbwembwe kama za Jk hutafika mbali!
Piga kazi
 
I dont buy the idea ya mtu kugombea na.kushinda position kubwa kwa nchi halafu yeye kabla hajakaa ofisini anauliza wadau wanataka nini!!!

Mathalani wengi waseme hatutaki timu ya taifa ya football na badala yake tuanzishe timu ya taifa ya sumo yeye anakaa upande upi wa mzani???!!!

Habu aende ofisini atuletee work plan na time schedule tutaweka michango!!!!

Wapemba wanasema nyongeza huwekwa juu ya fungu!!!!!
Watanzania bwana. Wanapenda kumaliza hasira za matatizo yao kwa watu wengine.

Msiposhirikishwa lawama. Mtu kawashirikisha bado lawama.

Kwa haya uliyoyaandika hapa nadhani hujasoma Ilani yake ya uchaguzi. Kwa sisi tunaofatilia tunajua ipo kwenye mitandao ya kijamii. Itafute uisome kabla ya kuja na hizo lawama.
 
Karibu sana mkuu. Uwe tayari kupokea maoni mabaya na mazuri kama unavyojua hapa JF wengine ni watoto na wengine ni watu wazima. pamoja tuendeleze mpira wetu.
 
Back
Top Bottom