Shukrani za Jamal Emil Malinzi kwa wana JF

Uchaguzi umekwisha,tulikupa imani na umeshinda! Ukiwa mdau wa michezo,hususan soka kwa muda mrefu nataraji uongozi wako utupeleke pale Tenga aliposhindwa kutufikisha! Ni imani yetu hutatuangusha kwa kulewa madaraka kama ilivyo kwa viongozi wengine wa kada tofauti na soka!
 

Pamoja sana mkuu.. Tusongeshe soka letu mbele...
 
hongera mkuu, sasa ni kazi tu safisha hapo ndani kina SUNDAY KAYUNI na wenzake. tenga kashindwa kuwatoa wakati anajua kabisa ni watu ambao wanamuhalibia lakini akaacha kwa kuwaogopa
 
Nikupe pole kwa kuchaguliwa kuwa rais wa TFF manake cheo ni dhamana. Nakutakia mafanikio katika kutekeleza Ilani yako ya uchaguzi!!!!!
 
sio unatafuta urafiki ili ukiharibu tusikuulize boresha mpira
 
Hongera sana mkuu Jamal Malinzi tunategemea utekelezaji na si ubabaishaji Congrats once again.
 
Ukileta usharobaro kwenye mpira au mambo ya kijinga tunakunyofoa betri upate akili.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mimi ni miongoni mwa wenye mashaka na uwezo wako, na hatua zako za kwanza za kusamehe waliofungiwa na kutumia kikao chako cha kwanza kulipiza kisasi kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF kimeniongezea hisia hiyo. Jitahidi kubadili mawazo yangu dhidi yako kwa kufanya kazi kwa bidii na imani, bila ya woga, huba, upendeleo wala chuki.
 
We Jamal vipi mbona unafanya hivi,unazungukazunguka nini?!,ok.tunashukuru pia kwa shukrani zako lakini unapaswa kwenda mbaali zaidi ya hapa ikibidi tuandalie hata LUNCH kwa sababu kazi tuliyofanya ni kubwa Mno!!

Hii ndio point sasa...
 
Tusubiri tuone vitendo, tathmini ya kina titaipata humuhumu ndani. Tutaiona hiyo miujiza kama si kutesa kwa zamu, maana watu wanataka kukumbukwa kwa bei ndogo tu ya lunch kwa maana wanajua panaujasiriamali mali pale.
 
sisi hatutaki asante, tunataka utendaji uliotukuka
 
Bravo le Boss........Tunataka mpira uchezwe uwanjani si vinginevyo....,period....
 
mrudishe Marcio Maximo kuwa kocha wa timu ya taifa
 
Haya malinzi tunasubili kuandaa AFRICON
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…