Siku ukijua dunia haihitaji ulelemama utafuta ulichoandika.
Yaani dunia haitaki umlaumu mtu au kitu, hairudi nyuma yenyewe ni mbelembele tu. Huko nyuma tumia kama historia na rejea tu huku ukiendelea kupiga kwata kusonga mbele.
Ukikaa kinyonge ati ujute na kusikitika, dunia inakuacha na haikupi support kukushika bega kukutia moyo badala yake inakulamba mikwaju ya kulala njaa, kuumwa, madeni na majanga ya kutia mimba mwanafunzi ili ushike tama na kujuta vizuri.
Wanaoshindwa na mikwaju kuwalemea unaona anajitundika au kunywa sumu ila options zipo ni vile akili unakua umeistakisha kwenye kuilaumu elimu ati haijakusadia.
Kijana AMKA.