DOKEZO Shule Tusiime yadaiwa kuajiri walimu wa Uganda, Watanzania kuondolewa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Shule ya Tusiime iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam inadaiwa kuajiri walimu kutoka nchini Uganda (zaidi ya 50), kinyume na Sheria ya kuratibu ajira za wageni nchini ya 2015, lengo likitajwa kuwaondoa walimu wa Tanzania wanaofundisha shule hiyo.

Mmoja wa watoa taarifa katika shuile hiyo, amesema ajira za walimu kutoka nchini Uganda zimekuwepo kwa muda mrefu, huku ikielezwa kuwa hawana vibali vya kufanya kazi.

"Kwa sasa walimu hao wameongezeka na kuna mpango wa kutuondoa kazini ili wabaki wao."

"Maofisa kutoka Idara ya Uhamiaji wakifika hapa tunaona walimu wanakimbia na kujificha, halafu wakimaliza kuongea na mkuu, tunaona walimu wanarudi. Sio mara moja wala mara mbili, ni mara nyingi," alisema.

Mtoa taarifa huyo amesema kumekuwa na manyanyaso ya walimu wazawa, ambapo nyakati za sikukuu za kitaifa walimu hao hulazimishwa kuja kazini kwa madai ya kufanya vikao.

"Kwa mfano siku ya Mei Mosi tulilazimishwa kuja kazini, tulipokataa, kesho yake tuliwekwa kikao mpaka saa moja jioni."
 
"Hili nalo mkalitazame"
_______________________

Poleni sana,
Tatizo ni rushwa, mpaka mgeni anaingia nchini kuna mamlaka zinahusika kumruhusu, hakuna uzalendo na upendo wa kweli. Ni tamaa na rushwa.
Lakini kila jambo lenye mwanzo lina mwisho.
 
Mstari wa Mwisho una nguvu sana.
 
Hata Kampala university of Tanzania, ilikuwa na ujinga kama huu huu... Sasa hivi naona wameliweka sawa.
 
Katika waalimu wa hovyo ni hao wa Uganda. Hawawezi kwenda sawa na mitaala ya TZ. Management ya Tusiime imeamua kuimaliza kabisa shule kwa kuchukua cheap labour kutoka Uganda. Inasikitisha sana.
 
Kwani hiyo sheria ya kuratibu ajira za wageni inataka taasisi moja iajiri wageni wasiozidi wangapi?
 
Shule ya Tusiime iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam inadaiwa kuajiri walimu kutoka nchini Uganda (zaidi ya 50), kinyume na Sheria ya kuratibu ajira za wageni nchini ya 2015, lengo likitajwa kuwaondoa walimu wa Tanzania wanaofundisha shule hiyo.

Mmoja wa watoa taarifa katika shuile hiyo, amesema ajira za walimu kutoka nchini Uganda zimekuwepo kwa muda mrefu, huku ikielezwa kuwa hawana vibali vya kufanya kazi.

"Kwa sasa walimu hao wameongezeka na kuna mpango wa kutuondoa kazini ili wabaki wao."

"Maofisa kutoka Idara ya Uhamiaji wakifika hapa tunaona walimu wanakimbia na kujificha, halafu wakimaliza kuongea na mkuu, tunaona walimu wanarudi. Sio mara moja wala mara mbili, ni mara nyingi," alisema.

Mtoa taarifa huyo amesema kumekuwa na manyanyaso ya walimu wazawa, ambapo nyakati za sikukuu za kitaifa walimu hao hulazimishwa kuja kazini kwa madai ya kufanya vikao.

"Kwa mfano siku ya Mei Mosi tulilazimishwa kuja kazini, tulipokataa, kesho yake tuliwekwa kikao mpaka saa moja jioni."
Wahaya na waganda ni dugu moja. Usishangae ukakuta mmilki si raia au ana uraia pacha.
 
Back
Top Bottom