Shule ya Mivumoni Islamic iliyoko Kinondoni yateketea kwa moto ikiwa ni mara ya tatu sasa!

Shule ya Mivumoni Islamic iliyoko Kinondoni yateketea kwa moto ikiwa ni mara ya tatu sasa!

Mkuu, kwa mtazamo wangu, yote yanawezekana kama ifuatavyo:

1. DHULUMA: Hapa yaweza kuwa kuna kuna vita miongoni mwa jamii za kiisla kama ambavyo hutokea mivutano mingine kati ya shiha na sun nk. Yafaa kuona ni shule zinazomilikiwa na nani ndizo zinazodhurika na moto huo.

Au migongano ya kimaslahi kati ya watumwa na watwana wao. Kulipiza kisasi wanachoma shule. Si jambo la kupuuza. Kuna shule moja ya serikali katika wilaya X iliwahi kuungua bweni wakati wanafunzi wakiwa darasani usiku. Eti eti zilikuwa ni mwalimu mmoja ambaye alikuwa anafundisha shuleni hapo akaondolewa kupelekwa kufundisha shule ya msingi na yeye hakuwa tayari. Alipolazimishwa akaamua kumkomoa mkuu wa shule kwa kuchoma bweni. Ushahidi haukukamilika kumtia hatiani mtuhumiwa.

2. UTUKUTU WA WANAFUNZI. Natoa pia ushuhuda. Baadhi ya wanafunzi wa bweni wakiwa chini ya uangalizi mkali lakini bado wanamiliki simu. Ili wazitumie wanahitaji kuchaji. Bwenini hakuna soketi. Wanafumua swichi na kuunga chaja kwa local circuit. Lolote laweza kutokea. Huenda pia kukawa na matumizi ya siri ya vifaa kama local hitters mabwenini.
Ingawa si ajenda sana, lakini si jambo la kupuuza pia. Kuna shule ilinusurika kwa tukio kama hili.

3. UCHAKAVU WA MIUNDOMBINU YA UMEME. Yafaa pia kuchunguza hizo shule zinazoungua mifumo yake ya umeme ina umri gani? Je, hakuna vihatarishi kama panya kutafuna rubber zinazofunika nyaya za umeme? Circuit breaker zilizofungwa zina uwezo kiasi gani? Kwa ujumla wataalam wa umeme wabobezi wangehusishwa kuangalia mifumo hiyo.

Sina imani na suala la ushirikina na majini. Kama vipo basi elimu hiyo imenipita mbali sana na sidhani kama nitajifunza kuhusu hilo.

USHAURI WANGU:
Serikali itumie vijana wake kwa kuwapandikiza mashuleni japo kwa muda mfupi ili watafute habari kamili juu ya hizo shule za kiislam zinazoonekana kuwa hatarini zaidi kuchunguza kwa kina kunani.
Shule zote zinaungua, lakini hizi za kiislam ni kama zinazidi hivi kiasi cha shule moja kuungua mara tatu ndani ya miezi miwili. Ni ajabu.


Ni kweli kabisa uchunguzi ungefanyika walau ijulikane tatizo ni nini.
 
Majini yamepigana hapo usiku kucha, Hadi moja likafa na kusababisha mlipuko mkubwa uliopelekea shule kuteketea kwa moto .
Majini Ni viumbe tu Kama ng'ombe, nao Wana hisia za hasira, furaha etc
Huna akili wewe na matako yako makubwa
 
Huu ndio ukweli...haiwezekani iwe hvi;
Kuanzia Kinondoni Muslim,Ubungo Islamic,Ilala Islamic,Kaloleni Girls na nyingi nyinginezo chini ya Bakwata.

Bila kuzungusha maneno ni vita ya wenyewe kwa wenyewe zinazoumia ni nyasi....
Ubungo islamic iko chini ya bakwata? Bakwata hawawezi kuwa na shule kama ile wewe, bakwata shule zao ni Al haramain na jamii hiyo, ubungo ipo chini ya IPC
 
Back
Top Bottom