A
Anonymous
Guest
Utaratibu wa shule hiyo Wanafunzi wote uripoti asubuhi ambapo baadhi ya Wazazi wenye Watoto wanaosoma shuleni hapo wanadai Watoto wao ulazimika kwenda na mifuko au viroba kwa ajili ya kukalia chini ili wasichafuke kwa vumbi au matope.
Nimezungumza na mmoja wa wazazi shuleni hapo anasema "Shule ina Watoto wengi sana, Mwanangu yupo darasa la sita, huwa anaenda na mfuko autumie kukaa kwa kuwa wengi wao wanakaa chini, mfano darasa la sita nasikia wapo zaidi ya 400.
Pia mzazi mwingine ambaye ana Mtoto wa darasa la pili kwenye shule hiyo anadai mtoto wake wa darasa la pili kuna wakati alikuwa akimchapa kutokana na kuja nyumbani akiwa amechafuka, lakini baadae alikuja kugundua anamuonea baada ya kufika shuleni muda vipindi kujionea hali ilivyo.
"Nilichogundua Darasa la pili Watoto karibia wote wamekaa chini na wapo zaidi ya 600 nilipoingia darasani kwao madawati hayafiki hata 10.”
Uchunguzi unaonesha katika vipindi vya mvua zaidi ya nusu ya Wanafunzi huwa awaendi shuleni kutokana na maeneo ya wazi ya chini ambayo uyatumia kama darasa uwa yamejaa maji jambo ambalo linaongeza ugumu.
Vyanzo mbalimbali vinadai katika kipindi ambacho mvua zilikuwa zinanyesha hususani Aprili 2024 wazazi walikuwa hawawaruhusu watoto kwenda shuleni jambo ambalo wanadai linawaumiza lakini hakuna mbadala kwao.
Mwalimu ya shule hiyo anasemaje?
Mwalimu mmoja wa Shuleni hapo anasema "Kuna Watoto kama elfu nne au zaidi kidogo, tunawafundishia wakiwa chini ya miti mara kwa mara."
Pia kila mtoto kwenye shule hiyo anatozwa Tsh. 300 kwa ajili ya mitihani ya kila siku utamaduni ambao ni sehemu ya upigaji kwa kuwa asilimia kubwa madaftari ya Wanafunzi yamejaa mitihani ambayo uifanya kila siku bila kufundishwa kama ratiba zinavyoonesha.
Utamaduni huo umekuwa kama Sheria tangu Mwaka 2023, ambapo hata kipindi cha mitihani Watoto wanatozwa kiasi hicho ambacho udaiwa ni cha mitihani ya kila siku.
Kingine ni kuwa mitihani hiyo usahihishwa na baadhi ya Wanafunzi, ambapo chanzo rasmi kutoka kwenye shule hiyo kinadai kwamba hilo linatokea kutokana na uhaba wa Walimu ambao unaenda sambamba na idadi ya Wanafunzi wengi.
Ambapo baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba na la sita upewa jukumu la kusahisha mitihani ya Wanafunzi wa madarasa ya chini, ambapo mmoja kati ya walimu kwenye shule hiyo anakili uwepo wa suala hilo na kudai kuwa linachangiwa na uwaba wa walimu.
Baadhi ya wazazi wamewahi kuwadokeza baadhi ya viongozi ngazi ya Wilaya na Mkoa lakini limefumbiwa macho mpaka sasa hakuna jitihada za haraka zilizooneshwa wazi kuleta ufumbuzi wa changamoto hizo.
Hii ni aibu kubwa kwa shule iliyopo chini ya Halmashauri ya Jiji kuwa na changamoto kubwa ya aina hiyo, ambapo wametoa wito zaidi kwa mamlaka kuchukua hatua za haraka sana kuepusha changamoto hizo kwa maslahi mapana ya jamii.
Bila jitihada za haraka kufanyika kuna wanafunzi wengi wataacha shule au wengine kukosa kabisa kupelekwa shule kutokana na Mazingira duni yanayoikabili shule hiyo iliyopo jijini.