Niko visiting day leo hapa shuleni nimekuta mwanangu wa grade 4 kapigwa sana sehemu za jichoni hadi kutafuta hawezi.
Ameibiwa mswaki, dawa, ndoo za kuogea, nguo za michezo nk, kwa kifupi hajaoga zaidi ya wiki mbili, alienda kushtaki kwa Mwl X akamjibu USINISUMBUE.
Mind you walikataa wazazi tusione mabweni wanakolazwa watoto na wakaweka sheria ya std 4 kuanza masomo saa kumi na mbili asubuhi na kutoka saa kumi na moja na nusu jioni kuanzia J3 - Jmosi.
Kwanini wachanganye wanafunzi wa Primary na Secondary bwenini? Kuna uovu mkubwa sana unaendelea pale, najua vyombo husika vifanye uchunguzi maana kwa majibu hayo ya huyo mwalimu inaonekana shule ya Kikatili sana ile.
Nampeleka mtoto hospitali hapa, naombeni msaada wa kisheria wanajukwaa.