KERO Shule ya Sekondari Nsongwi Juu - Mbeya Vijijini imekuwa na changamoto ya utawala mbovu

KERO Shule ya Sekondari Nsongwi Juu - Mbeya Vijijini imekuwa na changamoto ya utawala mbovu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
photo_2026-08-12_16-09-38.jpg
Shule ya Sekondari Nsongwi Juu (Mbeya Vijijini) imekuwa shule yenye utawala mbovu imefikia hatua mpaka Walimu wanashindwa kufanya kazi kwa sababu ya utawala huo. Kesi zimekuwa nyingi zimefika mpaka kwa Afisa Elimu Kata na Afisa Elimu Wilaya lakini hazitatuliwi, sasa hatujui shida ni nini?

Utawala umeigawa staff, kwa hiyo kuna watu wengine wanaondolewa majukumu yao ya kiualimu wanabebeshwa wengine, mfano linapofika suala la usimamizi wa mitihani ya ndani kuna Walimu hawawekwi kusimamia na wale ambao ndiyo kundi la mkuu ndio hawasimamii.

Pili, Mkuu na kundi lake hawataki mtu yeyote ahoji mapato na matumizi ya kituo.

Tatu, Makamu Mkuu wa Shule amekuwa mtu wa kutoa vitisho kwa Walimu kwamba tutii kila kitu wanachoamua la sivyo watatuchomea ili tuhamishiwe vijijini zaidi.

Kulikuwa na miti ya shule wakaenda kuchonga meza na viti ambavyo havina hadhi kabisa tulipohoji tukaambia kama tunataka vizuri tutoke navyo nyumbani kwetu, kwa hiyo kiufupi utawala umekuwa na manyanyaso kwa walimu hasa ambao hawawaungi mkono kiasi kwamba hata kupata kiti cha kukaa kwenye ofisi ya staff napo ni jambo ya kupambania.
photo_2026-08-17_15-29-44.jpg

 
Polesana mwalimu. Changamoto kwenye vituo vya kazi zipo. Ila naajua wasafwa sio watu wa jambo dogo kabisa. Hivo fuata utaratibu wa kawaidq wako binafsi badalq ya kusema mwalimu mkuu kashitakiwq mpka kwa afisa elimu kata, wew nenda kashittaki. Yaan namaanishq anza wew kuwajibika nendq ngazi za juu natoa malalamiko yako. Ila kumbukq huwenda mkono wake mrefu na hali peke yake, hivyo kuwa makin kwa kila step utayokuw unapiga.
 
photo_2026-08-17_15-29-47.jpg
Shule ya Sekondari Nsongwi Juu (Mbeya Vijijini) imekuwa yenye utawala mbovu imefikia hatua mpaka Walimu wanashindwa kufanya kazi kwa sababu ya utawala huo. Kesi zimekuwa nyingi zimefika mpaka kwa Afisa Elimu Kata na Afisa Elimu Wilaya lakini hazitatuliwi sasa hatujui shida ni nini?

Utawala umeigawa staff kwa hiyo kuna watu wengine wanaondolewa majukumu yao ya kiualimu, wanabebeshwa wengine bila mpangilio maalum, mfano usimamizi wa mitihan ya ndani kuna walimu hawawekwi kusimamia, wale ambao ndiyo kundi la mkuu hawasimamii.
photo_2026-08-17_15-22-35.jpg
Pili, mkuu na kundi lake hawataki mtu yeyote ahoji mapato na matumizi ya kituo.

Tatu, Makamu mkuu wa shule amekuwa mtu wa kutoa vitisho kwa walimu kwamba tutii kila kitu wanachoamua la sivyo watatuchomea ili tuhamishiwe vijijini, kulikuwa na miti ya shule wakaenda kuchonga meza na viti ambavyo havina hadhi kabisa tulipohoji tukaambia kama tunataka vizuri tutoke navyo nyumbani kwetu kwa hiyo kiufupi utawala umekuwa wa manyanyaso kwa walimu hasa ambao hawawaungi mkono.
 
Back
Top Bottom